Daktari Temeke aacha mgonjwa theatre kufuata kifaa dukani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Daktari Temeke aacha mgonjwa theatre kufuata kifaa dukani

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Jan 9, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jan 9, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Kituko cha mwaka kimeibuka katika hospitali ya wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam, baada ya daktari mmoja wa upasuaji hospitalini kumuacha mgonjwa kwenye kitanda cha upasuaji na kukimbilia dukani kununua kifaa kilichokosekana kwa zoezi hilo.

  Ni tukio lisilo la kawaida pengine kutokea hapa nchini, likionyesha jinsi sekta ya afya ilivyoelemewa katika usambazaji wa vifaa muhimu vya huduma katika hospitali za serikali.

  Daktari huyo(jina linahifadhiwa kwa sasa), alibaini kukosekana kwa moja ya vifaa muhimu wakati wa upasuaji huku akiwa tayari ameshaanza upasuaji na haraka akatimkia dukani kununua kifaa hicho chenye thamani ya sh.1,000/ tu.
  Tukio hilo la kusikitisha lilitokea hivi karibuni katika hospitali hiyo, ambapo daktari huyo (jina limehifadhiwa) alichukua hatua hiyo

  baada ya juhudi za kupata kifaa hicho chenye thamani ya Sh.1,000/- kushindikana.
  Kituko hicho kiliibuliwa juzi na Mkurugenzi wa Manispaa wa Temeke, Magreth Nyalile baada ya kuitisha kikao cha dharura cha madaktari wa hospitali hiyo, akitaka maelezo ya kina kwanini utoaji huduma kwenye hospitali hiyo umedorora sana mwaka jana.

  Habari za uchunguzi kutoka kwenye hospitali hiyo zinasema daktari huyo siku ya tukio alikuwa kwenye chumba cha upasuaji kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa wa dharura.

  Akiwa katikati ya zoezi hilo, aligundua kifaa hicho kimekosekana ndipo alipotoa taarifa kwa mtu anayehusika na ununuzi wa vifaa vya dharura.

  Jambo la kusikitisha ni kwamba mfanyakazi huyo anayehusika na ununuzi aligoma kwenda kununua kifaa hicho kwa maelezo kwamba sharti kwanza apewe hati ya ununuzi (invoice) inayoonyesha gharama halisi ya kifaa hicho.
  Kufuatia jibu hilo, daktari huyo kwa ujasiri aliamua kumuacha mgonjwa wake kitandani na kisha alikimbilia moja ya maduka yaliyo nje

  ya hospitali hiyo kwenda kununua kifaa hicho na kuokoa maisha ya mgonjwa huyo.
  Akionekana kuchukizwa na tukio hilo, Nyalile alisema mtu aliyesababisha kutokea kwa tukio hilo hatakuwa na msamaha kwani lazima

  achukuliwe hatua kali ili iwe fundisho kwa wafanyakazi wasiowajibika.
  Hata hivyo alimpongeza daktari aliyechukua hatua hiyo na kumuelezea ni mtu ambaye anafuata maadili yake ya kazi na hakutaka mgonjwa apoteze maisha yake kwa kutokuwepo kwa kifaa chenye gharama isiyozidi Sh.1000/-.  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

  Kasheshe kweli Hospitali zetu tutakwisha sana namna hii Hata vifaa hakuna?


   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  Jan 9, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Aiseeee!!
  Kwani hua hawaandai vifaa na kuhakikisha kila watakachohitaji kinakuwepo kabla ya upasuaji?

  Kwa style hii siwezi kukubali kufanyiwa upasuaji kwenye hosp za nyumbani. Mtu unaweza ukachanwa kwa kutumia kisu cha jikoni hivi hivi.
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Jan 9, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,465
  Likes Received: 19,847
  Trophy Points: 280
  daktari yeye kazi yake ni kufika na kufanya upasuaji..kila kitu inabidi akikute pale..hao ndugu zako sasa ndio wenye nyodo na roho mbaya utafikiri hawana watoto
   
 4. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #4
  Jan 9, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Ndugu zangu tena?

  Nwy muandaaji awe daktari au nesi, walitakiwa wahakikishe kila kitu kipo kabla ya kumlaza mgonjwa mezani. Sio kitu hakipo hata ndani ya hosp na bado wanamweka mtu kwenye meza ya upasuaji.
   
 5. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #5
  Jan 9, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,465
  Likes Received: 19,847
  Trophy Points: 280
  ndugu zako ndio..manesi na wale wapiga domo wengine ndio wanatakiwa waandae...tukija kwenye hili tukio tunaon kabisa jinsi wafanyakazi wa serikalini walivyo .huu ni mfano hai.sasa sijui tubinafsishe serikali nzima au vipi
   
 6. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #6
  Jan 9, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,345
  Trophy Points: 280
  Nimecheka hiyo sentesi yako ya kuchanwa na kisu cha jikoni.

  Kwa utaratibu kuna wauguzi wanaotakiwa kuhakikisha kila kitu kipo na ni salama. Kazi ya daktari ni kutoa maagizo ya kile anachotaraji kukitumia kutokana na aina ya upasuaji. Ni kweli kuwa kuna uzembe lakini uzembe huo ni wa baadhi ya wahusika na si taaluma yote na tutakuwa hatuwatendei haki wengine.

  Tumpongeze dakatari japo kwa moyo wa kukimbia kutafuta kifaa. Alikuwa katika nafasi ya kulaumu bila ya yeye kulaumiwa. Hakusubiri maswahibu yafike ili apate pa kusemea bali ali act promptly kujali maisha ya mwanandamu.

  Hii pia inaonyesha hali halisi ya huduma za afya nchini mwetu. Kwa utaratibu wa kawaida hapo kungekuwa na mlolongo wa watu kupoteza kazi lakini kama ilivyo kwa viongozi wa juu kulindana basi mkondo huo upo hadi ngazi za chini.

  Nakusihi usiseme kuwa hutakubali operesheni nyumbani kwasababu wengi tumekulia nyumbani na tunategemea huduma hizo. Labda tuwashukuru wataalam wa afya kwani pamoja na yote wameweza kuokoa maisha yetu au ya ndugu zetu kwa namna moja au nyingine.

  Kwa bahati mbaya hakuna ajuaye ugonjwa utamkuta wapi na katika hali gani. Unaweza kusema hivyo na siku moja (mungu apishilie mbali) ukajikuta umeshatoka theatre kwasababu hata ulivyoingia hukujua. Muhimu ni kusisitiza uboreshaji wa huduma.

  Wingi wa mkosa haya ya kizembe unasikitisha lakini tuelewe kuwa procedure za operesheni zimeandikwa baada ya kutokea makosa mengi ya namna hiyo. Australia yupo mgonjwa aliachwa na mkasi tumboni, uingereza na Marekani pia yapo matukio. Hii haihalalishi uzembe kwa namna yoyote ni katika kubainisha tu kuwa matukio ya uzembe yapo kila mahali na tukio moja au lingine lisifanywe kama ndio utendaji wa taaluma yote ya afya.
   
 7. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #7
  Jan 9, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Nakubaliana na wewe kwamba daktari alitumia werevu na weledi wake kufanya kile alichotakiwa kufanya kwa wakati ule, kwa hilo nampengeza sana.

  Ila twende mbele , turudi nyuma huduma za afya kama zilivyo nyingine kwenye nchi yetu ni zaidi ya hovyo. Wanaojali wagonjwa kama huyo daktari ni wachache sana, wengi wanaangalia maslahi yao pekee. Kuna rafiki yangu daktari alinihadithia kitu kuhusu daktari mwenzake nilisikitika sana (sitoweka hapa mana sio mahali pake) ila inaonyesha ni kwa namna gani wataalam wetu wasivyoheshimu na kutendea haki taaluma zao. Kwahiyo narudia tena sina imani na madaktari wetu, kabla ya kukubali kunywa hata dawa ya malaria ntapima hata mara tano kujihakikishia hawataki kuniingiza gharama ya bure na kuniacha nikiendelea kuugua taratibu.

  Kwahiyo hiyo ya kisu ndio kabisaaa, ntafanya kila kilochopo ndani ya uwezo nilopewa na mwenyenzi Mungu isitokee. . . .naweza nikafa kwa hofu pekee.
   
 8. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #8
  Jan 9, 2012
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,078
  Likes Received: 1,813
  Trophy Points: 280
  Actually lizy surgeon akifika pale Kazi yake ni moja tu .. kusoma file la mgonjwa plus xray au ct anatakiwa afanye nini .. kuna watu behind the Scene Kazi yao ni kumtayarisha mgonjwa hapa nazungumzia anaesthisiologist , na ma nurse kuhakikisha vifaa vyote vipo .. sasa dactari anapoanza operation alafu yupo katikati akaomba scalpel ya aina flani akaambiwa hakuna .. kosa ni la nurse hapo ..

  Sent from my HTC Incredible S using Tapatalk
   
 9. n

  ngwana ongwa doi Member

  #9
  Jan 9, 2012
  Joined: Dec 26, 2011
  Messages: 75
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kwanza nampongeza huyo DK.kwa maamuzi magumu kufuata kifaa kuokoa maisha ya mgonjwa,nasema maamuzi magumu sababu DK.na wasaidizi wake wakisha kuvaa nguo sterile hawaruhusiwi siyo tu kotoka nje ya operating room bali hata kuzunguka kwenye chumba hicho mbali na alipo mgonjwa.

  Nina maswali naiuliza hapa ukiachia na nurse anayekaa na vifaa na kumpatia kifaa DK.kinachohitajika kuna watu wengine mfano mtoa dawa ya usingizi,assistant nurse,na runner nurse(huyu kazi yake ni kutumwa kuleta kifaa chochote kinachopungua kwenye pack ya vifaa) ikiwa ni ndani ya operating room au chumba kingine cha theatre na siyo kutafuta dukani.Kwani lazima kuwe na watu wengine nje ya oper.room wanawezatumwa sehemu nje ya theatre kama huko may be dukani japo ndo nasikia hii je walikuwa wapi au ndo nao walikataa.

  Nimefafanua ili angalau watu wasianze kumlaumu nurse wa vifaa kwani aliyekataa kwenda dukani ni mtu anyehusika na manunuzi na si nurse wa vifaa,yeye kazi yake akifungua pack nakukuta kifaa hakipo hutoa report kwa dk.anayepasua hapo wataamua cha kufanya,kumbuka wao wanakuta pack zilishafungwa tayari na watu wengine,wao ni kufungua tu nakuangalia kama kuna mapungufu na kuripoti kunakohusika.

  Tatizo naliona ni kufanya kazi kwakukariri sheria bila kujali utu mfano kulazimisha invoice wakati mgonjwa yuko mezani ni swala la utu zaidi kuliko kuangalia sheria za kazi.
   
Loading...