Daktari: Pigeni nyungu angalau mara 2 kwa siku

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,005
9,872
MKURUGENZI wa Taasisi ya Utafi ti ya Dawa Asili Muhimbili (MUHAS), Dk Joseph Otieno, amesema kujifukiza ni tiba ambayo ikitumika vizuri, inaboresha mfumo wa upumuaji na kuusaidia mwili kupata nguvu ya kupambana na maradhi.

Akizungumza na HabariLeo jijini Dar es Salaam, Dk Otieno alisema kwenye mlipuko wa virusi vya corona, ni vyema wananchi bila kujali kama wameathirika au la, wajenge tabia ya kujifukiza angalau mara mbili kwa siku ili kuukinga mwili usipate virusi hivyo. Kwa mujibu wa Dk Otieno, kujifukiza ni tiba iliyokuwa ikitumika katika jamii nchini na ilionesha matokeo chanya.

“Nasisitiza tena kama nilivyosisitiza mwaka jana wakati wa janga la corona lilipoingia nchini, kujifukiza kwa njia sahihi ni kinga dhidi ya maradhi haya, cha msingi ni kutumia viungo sahihi na kufuata maelekezo jinsi ya kuvichanganya na kujifukiza,”alisema.

Alizungumzia namna ya kudhibiti virusi vya corona kwa kutumia njia za asili ikiwemo ya kujifukiza maarufu kupiga nyungu, Dk Otieno alishauri kuwa kwa mazingira ya Tanzania, aina tatu za majani zinapatikana kwa urahisi na zimefanyiwa utafiti na kuthibitika ubora wake, lakini pia zina machapisho.

Alitaja majani hayo kuwa ni ya kivumbasi (kashwagala), mkaratusi na mchaichai. Alisema usalama wa majani hayo, umethibitika na yana mafuta tete yanayosaidia kufungua mfumo wa upumuaji ili mwili upate nguvu ya kupambana na maradhi.

“Nyungu inafaa sana kama virusi bado viko kwenye mfumo wa upumuaji havijaingia kwenye seli za damu, kwa sababu unapojifukiza kwa kutumia vitu hivyo vitatu kwa njia sahihi, hayo mafuta tete yanapenya vizuri na kuingia kwenye mfumo wa upumuaji na kuuzibua, hapo mwili unapata nguvu na kupambana vizuri’’alisema Dk Otieno.

Alisema, iwapo virusi vya corona vitakuwa vimeingia kwenye seli za damu, njia sahihi ya kuusaidia mwili kupambana navyo ni kutumia maji ya moto yaliyochanganywa na tangawizi ili kusaidia damu isigande kwenye mishipa wakati huo mwili ukipambana na virusi.

Dk Otieno alisema kiungo kingine kinachofanya kazi sawa na tangawizi katika kupambana na corona ni kitunguu saumu, ambacho kazi yake ni kusaidia damu isigande wakati mwili unapambana na maradhi.

Alisema kitunguu saumu katika tiba hii, kinatakiwa kisagwe na kuwekwa kwenye maji baridi au kukitafuna kibichi, kwa sababu ukikichemsha unaua nguvu yake na hapo hakitafanya kazi kusudiwa.

Kwa mujibu wa Dk Otieno, kwa kawaida virusi havina tiba na vinapoingia mwilini hupambana na kinga ya mwili na kama mwili ukiwa na kinga nzuri huvishinda na kuviua, lakini ukiwa na kinga dhaifu mwili hushindwa kupambana navyo na matokeo yake ni kifo. Alisema watu wengi hukosea namna ya kujifukiza, kwa kuwa wanachemsha majani ya mimea hiyo hadi yanapoteza mafuta tete yanayohitajika.

Dk Otieno alisema ili kujifukiza, inabidi kuchemsha maji hadi yatokote kisha unaweka majani ya mchaichai, mkaratusi na kivumbasi (kashwagala) na kukoroga, kisha kuyaepua na kuanza kujifukizwa kwa kujifunika na shuka zito au blanketi kwa dakika kati ya tano hadi 10 kulingana na uwezo wa mwili.

“Wengi wanakosea wanadhani unachemshia hivyo vitu huko wee, kufanya hivyo unaua mafuta tete yote yanayohitajika,”alisema.
Dk Otieno alisema kujifukiza si lazima mtumiaji atumie vitu hivyo vitatu, anaweza kutumia kimojawapo na kuzingatia maelekezo, afanye hivyo kwa mara mbili kwa siku na kusisitiza kujifukiza kuwa sehemu ya maisha ya wananchi kila siku.

Alisema mtu anayejifukiza anapaswa kufunga macho, kuachama mdomo na pua, kisha aendelee kuhema kawaida ili kuruhusu mvuke kupita kwenye mfumo wa upumuaji na akishaepua nyungu, akoroge mara moja ili ule mvuke mkali utoke kisha ndio ajifunike na shuka au blanketi.

Alishauri kuwa wagonjwa, wazee na watoto, wasijifukize ila wanywe maji ya moto yenye tangawizi, au iliki na mdalasini.

Chanzo: HabariLeo
 
Kwa hiyo wanataka kutuaminisha kuwa wazungu wanaokufa na corona huku hawajui kupiga nyungu au kutumia tiba asili?

Kwa wazungu mbali vipi hapo kwa jirani zetu Wakenya?
😃😃😃
 
Mbona jana kuna profesa kakanusha kuwa tupuuze uzushi wa mitandaoni Tanzania hamna Kovidi kumi na tisa?

Mnatuchanganya sasa, tushike lipi tuache lipi?
 
kila mtu apambane kivyake......ila ndo hivyo...hosptl zimejaa,,,,,,na huko kama huna pesa imekula kwako....unatoa advance ya 1m kwanza...Mungu usituache hakika......vipato vyenyewe vya kuunga unga.....
 
Mara tuambiwe kujifukiza sana kunaharibu mfumo wa upumuaji, mara tujifukize sana dah.....
 
Za kuambiwa changanya na zako. Kaka kama kusoma hujui, hata picha huwezi kuona?
 
MKURUGENZI wa Taasisi ya Utafi ti ya Dawa Asili Muhimbili (MUHAS), Dk Joseph Otieno, amesema kujifukiza ni tiba ambayo ikitumika vizuri, inaboresha mfumo wa upumuaji na kuusaidia mwili kupata nguvu ya kupambana na maradhi.

Akizungumza na HabariLeo jijini Dar es Salaam, Dk Otieno alisema kwenye mlipuko wa virusi vya corona, ni vyema wananchi bila kujali kama wameathirika au la, wajenge tabia ya kujifukiza angalau mara mbili kwa siku ili kuukinga mwili usipate virusi hivyo. Kwa mujibu wa Dk Otieno, kujifukiza ni tiba iliyokuwa ikitumika katika jamii nchini na ilionesha matokeo chanya.

“Nasisitiza tena kama nilivyosisitiza mwaka jana wakati wa janga la corona lilipoingia nchini, kujifukiza kwa njia sahihi ni kinga dhidi ya maradhi haya, cha msingi ni kutumia viungo sahihi na kufuata maelekezo jinsi ya kuvichanganya na kujifukiza,”alisema.

Alizungumzia namna ya kudhibiti virusi vya corona kwa kutumia njia za asili ikiwemo ya kujifukiza maarufu kupiga nyungu, Dk Otieno alishauri kuwa kwa mazingira ya Tanzania, aina tatu za majani zinapatikana kwa urahisi na zimefanyiwa utafiti na kuthibitika ubora wake, lakini pia zina machapisho.

Alitaja majani hayo kuwa ni ya kivumbasi (kashwagala), mkaratusi na mchaichai. Alisema usalama wa majani hayo, umethibitika na yana mafuta tete yanayosaidia kufungua mfumo wa upumuaji ili mwili upate nguvu ya kupambana na maradhi.

“Nyungu inafaa sana kama virusi bado viko kwenye mfumo wa upumuaji havijaingia kwenye seli za damu, kwa sababu unapojifukiza kwa kutumia vitu hivyo vitatu kwa njia sahihi, hayo mafuta tete yanapenya vizuri na kuingia kwenye mfumo wa upumuaji na kuuzibua, hapo mwili unapata nguvu na kupambana vizuri’’alisema Dk Otieno.

Alisema, iwapo virusi vya corona vitakuwa vimeingia kwenye seli za damu, njia sahihi ya kuusaidia mwili kupambana navyo ni kutumia maji ya moto yaliyochanganywa na tangawizi ili kusaidia damu isigande kwenye mishipa wakati huo mwili ukipambana na virusi.

Dk Otieno alisema kiungo kingine kinachofanya kazi sawa na tangawizi katika kupambana na corona ni kitunguu saumu, ambacho kazi yake ni kusaidia damu isigande wakati mwili unapambana na maradhi.

Alisema kitunguu saumu katika tiba hii, kinatakiwa kisagwe na kuwekwa kwenye maji baridi au kukitafuna kibichi, kwa sababu ukikichemsha unaua nguvu yake na hapo hakitafanya kazi kusudiwa.

Kwa mujibu wa Dk Otieno, kwa kawaida virusi havina tiba na vinapoingia mwilini hupambana na kinga ya mwili na kama mwili ukiwa na kinga nzuri huvishinda na kuviua, lakini ukiwa na kinga dhaifu mwili hushindwa kupambana navyo na matokeo yake ni kifo. Alisema watu wengi hukosea namna ya kujifukiza, kwa kuwa wanachemsha majani ya mimea hiyo hadi yanapoteza mafuta tete yanayohitajika.

Dk Otieno alisema ili kujifukiza, inabidi kuchemsha maji hadi yatokote kisha unaweka majani ya mchaichai, mkaratusi na kivumbasi (kashwagala) na kukoroga, kisha kuyaepua na kuanza kujifukizwa kwa kujifunika na shuka zito au blanketi kwa dakika kati ya tano hadi 10 kulingana na uwezo wa mwili.

“Wengi wanakosea wanadhani unachemshia hivyo vitu huko wee, kufanya hivyo unaua mafuta tete yote yanayohitajika,”alisema.
Dk Otieno alisema kujifukiza si lazima mtumiaji atumie vitu hivyo vitatu, anaweza kutumia kimojawapo na kuzingatia maelekezo, afanye hivyo kwa mara mbili kwa siku na kusisitiza kujifukiza kuwa sehemu ya maisha ya wananchi kila siku.

Alisema mtu anayejifukiza anapaswa kufunga macho, kuachama mdomo na pua, kisha aendelee kuhema kawaida ili kuruhusu mvuke kupita kwenye mfumo wa upumuaji na akishaepua nyungu, akoroge mara moja ili ule mvuke mkali utoke kisha ndio ajifunike na shuka au blanketi.

Alishauri kuwa wagonjwa, wazee na watoto, wasijifukize ila wanywe maji ya moto yenye tangawizi, au iliki na mdalasini.

Chanzo: HabariLeo
Shida yetu ni hii. Viongozi wanatoa majibu makavu. Kama kuna wimbi la wagonjwa wasiishie kusema ni uzushi, wataje hao waliyopo wana shida gani. Pili Covidi siyo swala la kusiasa kama wataalamu wapo kwani hili hao wataalamu wasipewe nafasi ya kulisemea kuliko kuwatumia wana siasa? Imefika mahala swala dogo tu la kuelimisha kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima bado watu wanataka wasikie sauti ya Rais. Sijui tunakokwenda. Mtu akisema jambo ni kuzomewa kisa mkuu hajasema kweli? Tanzania leo huwezi kupata takwimu za watu wangapi wamepatwa na dalili za Covid kwasababu, viongozi waandamuzi wametamku kuwa nyungu ni dawa pekee na watu wameamini. Nihahao wenye mamlaka ya kutaja huduma gani iwepo kwenye hospitsli zetu, nyungu haijapewa kibali hicho. Hivyo basi mtu ikiona dalili anakimbilia huko ambako ameaminishwa kuwa kuna tiba, siyo haspitali maana anajua huduma hiyo haipo. Anaekwenda hospitali ni yule tu ambaye amezidiwa hana namna. Kwa sababu hiyo hatuwezi kuwa na takwimu sahihi. Swala la maada hii ni zuri sana kama linajadiriwa na watu hadharani lakini wanosikiliza ni wachache wengi wanasubiri wanasisa watamke tutafika? Binafsi maada nimeipata vizuri sana.
 
Back
Top Bottom