Daktari Pekee wa upasuaji wa watoto wachanga Muhimbili aondoka

mangifera

Member
Oct 15, 2011
47
34
Katika kuonyesha kuitika mwito wa Rais kikwete aliyetangaza kuwa Madaktari wasioridhika na malipo kiduchu na mazingira mabaya wanayofanyia kazi hapa nchini waondoke, Daktari pekee bingwa wa upasuaji wa vitoto vichanga (paediatric surgeon) ameondoka muhimbili na kuhamia hospitali moja ya binafsi mikoa ya kaskazini.

Hili ni pigo kubwa sana kwa watoto wachanga na sisi wazazi. Sasa mtoto akiwa na tatizo la upasuaji sasa hana tumaini tena la kuishi maana daktari huyu alikuwa anawafanyaia upasuaji watoto wote kutoka nchi nzima.

Ubinafsi huu wa wanasiasa kujineemesha huku wakitukana na kuadharau wataalamu utatumaliza.

Imagine mwanao anazaliwa bila njia ya haja kubwa halafu anakosa kufanyiwa upasuaji wa kuifungua! Mungu atusaidie!
 
daktari huyo anaitwa nani?
ni kweli kuwa yuko peke yake mwenye ujuzi huo?
vipi kina dr Swai, fataki,Massawe,Namala nk hawana huo ujuzi?
 
daktari huyo anaitwa nani?
ni kweli kuwa yuko peke yake mwenye ujuzi huo?
vipi kina dr Swai, fataki,Massawe,Namala nk hawana huo ujuzi?

Anaitwa Dr. Mng'ong'o ..hapana, uliowataja mkuu ni Pediatricians ( Pediatric Physicians), na aliyeondoka ni Pediatric Surgeon...so hawawezi fanya upsauaji kwani si speciality yao...ila aliondoka zamani mkuu yapata miezi miwili sasa.
 
ni aibu, ni tatizo kubwa

haifai kabisa hali hii kuacha iendelee katika nchi inayosimamia misingi ya sheria na haki

haki ya kuishi, haki ya kulipwa ujira wako sawasawa na kazi ulofanya ni vitu vya msingi vinavyopaswa kuheshimiwa na kila aitwae binadamu

inauma sana japo huwezi huelewa au kupata uchungu wa hayo maumivu mpaka wewe binafsi au nduguyo au rafiki yajo akumbane na hali hii

Mungu isaidie nchi yetu Tanzania, tupatie viongozi wabunifu, wachapa kazi, waadilifu na wenye akili na hekima
 
kama aliweza kufuatwa Muhimbili, atafatwa huko huko kaskazini hata kama ni Seriani au KCMC
Watz wa kawaida hawazimudu huduma zam hospitali binafsi na ni wachache wenye bima. Kusema atafuatwa huko huko ni sawa na kuunga mkono kauli ya JK.
 
halafu mwinyi anasema Tanzania haina uhaba wa madaktari bingwa.!!??
 
daktari huyo anaitwa nani?
ni kweli kuwa yuko peke yake mwenye ujuzi huo?
vipi kina dr Swai, fataki,Massawe,Namala nk hawana huo ujuzi?

kuna tofauti kati ya paediatrician na paediatric surgeon. Hao uliowataja hawafanya upasuaji, wanatibu magonjwa yanayopona kwa dawa tu.
 
kuna madaktari wanaotembeza cv zao wanatafuta kazi,haya sasa mambo hayo.inaitwa bandua,bandika
 
halafu mwinyi anasema tanzania haina uhaba wa madaktari bingwa.!!??

-Neurosurgeons(4),

-Orthopeadic surgeons(15),
-Pediatricians(28),

-ObGynaecologists(35),

-Physicians(60) regardless of subspeciality ie Neurolgist, Gastroenterologist,etc.
-Psychiatrist(30)-not psychologist,
-Surgeons (40)-regardless of subspecialty like Cardiothoracic, Plastic surgeons, Pediatric Surgeon etc,

-Otorhinolaryngologist(15),

- Anaesthiologist 25(not anaeshetist),
-Opthamologist 30(not optician,optometrist)....NCHI NZIMA.

so kwa takwimu hizo W/Afya anasema wanatosha!!!
 
t2015 bora uandike watapatikana,,,maana wanahitajika wengi mikoa tofauti si muhi2 tu,wapo watanzania ambao hawana uwezo wa KUJA DAR,hata kama yupo
 
Back
Top Bottom