Daktari mmoja aanza kuhamasisha mgomo baada ya kufiwa na mwanawe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Daktari mmoja aanza kuhamasisha mgomo baada ya kufiwa na mwanawe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Determine, Aug 24, 2012.

 1. D

  Determine JF-Expert Member

  #1
  Aug 24, 2012
  Joined: Apr 27, 2012
  Messages: 257
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Haya hapa chini ni maneno yake aliyoandika kwenda jukwaa la madaktari:

  'Tuna sababu ya kuendelea kupigania haki yetu ya msingi ya huduma bora za afya,kukaa kimya tunadhurika wote na nasikitika kusema imeanzia kwangu na sikujua kuwa MNH ina ventilator moja kwa ajili ya watoto nayo haifanyi kazi.I lost my baby pamoja na jitihada za madaktari bingwa waliobobea zaidi ya 5 .Chonde chonde tupaze sauti zetu na maisha yanayoweza kuokolewa yaokolewe'
   
 2. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #2
  Aug 24, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Waswahili husema 'KAZI YAKE MOLA'
   
 3. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #3
  Aug 24, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Pole Sana kwa Dr huyo ukweli ni watu wanakufa sana tanzania kwa kukosa vifaa tu. Leo hii Ulimboka asienepelekwa South asingekuwepo....Lakini leo karudi na kuishia kwenye mikono mwa mafisadi.......


  Liwalo na liwe
   
 4. k

  kichenchele JF-Expert Member

  #4
  Aug 24, 2012
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 522
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Mabwepande
   
 5. f

  findu fiki JF-Expert Member

  #5
  Aug 24, 2012
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 431
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Pole sana Dr kwa yaliyokukuta.Ikumbukwe pia kuna watoto wengi sana wanaokufa kwa kukosa huduma ambao wazazi wao hwana pa kusemea
   
 6. M

  Msendekwa JF-Expert Member

  #6
  Aug 24, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 440
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Walipodai haya, ya mazingira bora ya kazi na vitendea kazi, hamkuwaunga mkono,
  Rais akakomalia kuwa wanadai posho na mshahara,
  mkamuunga mkono na kukaa kimya,
  enyi watanzania wanafiki!
  Ngojeni tufe taratibu kwa kukosa vifaa ambavyo vinapatikana kwa gharama ya ma Vx kadhaa.
  Na hakika nawaambieni,
  kwa uzembe wetu na ukimya wetu wa kikondoo, maovu mengi yanatendeka,
  roho nyingi zinapotea.
  Ipo siku wajukuu watafukua makaburi yetu wapate kuona mifupa yetu na mafuvu yetu yalikuwa yanafananaje, kabla ya kuicharaza viboko!
   
 7. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #7
  Aug 24, 2012
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  V8 moja ni ventilator ngapi? Unajua sipendi mgomo ila kwa hali ya hospital zetu za serikali ambazo ndizo zinapokea wagonjwa wengi sana hakuna vifaa na madawa pia. Kama kweli wewe ulishawahi kupeleka ndugu yako hospital kubwa kama MNH halafu unapata huduma duni basi utajua kitu ninasema hapa kuwa "hata kama madaktari wanagomea maslahi but pia hata vifaa ni sehemu ya madai yao, wanaona mgonjwa anakata roho simply kifaa fulani kimeharibika au ni vichache foleni ya kipimo ni kubwwa". Kwa mantiki hii ninaomba serikali ikae na madaktari waongee haya mambo. Mkiruhusu tena mgomo basi jueni hamtendei watanzania haki.
   
 8. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #8
  Aug 24, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Tatizo watanzania wengi hawana pakulinganishia huduma na bora huduma!! Waooo wakipewa 20% ya kile wanachotakiwa wapewe wanaona serikali inajitahidi, serikali ina mipango mingi, kila aina ya visingizio utasikia tena na wananchi wenyewe siyo viongozi. Watu wavivu wa kufikiri mwanzo mwisho. Kuna kizazi Tanzania ni cha ajabu sana!!
   
 9. a

  artorius JF-Expert Member

  #9
  Aug 24, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 758
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hapo ni MNH,je uko vijijini hali iko vipi?
   
 10. t

  thatha JF-Expert Member

  #10
  Aug 24, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  pole kwa kumpoteza mtoto lakini vitendea kazi na vifaa tiba haikuwa kipaumbele ktk madai yenu,acha uongo
   
 11. t

  thatha JF-Expert Member

  #11
  Aug 24, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Madr wanaiba madawa na vifaa wanapeleka kwenye hosppitali zao za binafsi
   
 12. Babarita

  Babarita JF-Expert Member

  #12
  Aug 24, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 374
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Dr kasema ukweli ila kwa watanzania hii ni sinema,sijui ni nani aliyeturoga sisi watz,yan tupo tayari kuukataa ukweli na kuukubali uongo tena kwa gharama kubwa.Huduma za afya kwa hospitali za serikali kweli zinasikitisha..Wito kwa watz tuungane kwa sauti ya pamoja kuokoa maisha ya watz wenzetu wanaopoteza maisha kwa kukosa huduma stahiki
   
 13. Tram Almasi

  Tram Almasi JF-Expert Member

  #13
  Aug 24, 2012
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 755
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Well said Mkuu
   
 14. kisugujira

  kisugujira JF-Expert Member

  #14
  Aug 24, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 769
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ama kweli mkuki kwa nguruwe,kwa binadamu ni mchungu! Lengo kubwa la Bwana mkubwa ni kuendeleza fani za wanafamilia. Mama alipoenda kwa Obama alipelekwa kutembelea na kutafuta vifaa na ufadhili wa vifaa vya meno toka kwa waliobobea katika tiba ya meno! Si unajua kuna daktari wa meno katika familia. Ni aibu kwenda ulaya kutibiwa meno. Vifaa kama vilivyotumika kurudisha uhai wa Dr.Ulimboka, kuja kuletwa hapa nchini kwa sasa ni ndoto ya Abunwasi.

  Pole sana Daktari kwa kufiwa na mwanao.Bwana alitoa na Bwana ametwaa.
   
 15. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #15
  Aug 24, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,540
  Likes Received: 10,467
  Trophy Points: 280
  pole sana dokta kufiwa na mwanao,afadhali wewe mtoto amefia mikononi mwa madaktari bingwa watano.wenzio kumwona daktari bingwa ni kama anasa.!
   
 16. M

  Makindo Member

  #16
  Aug 24, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pole sana Dr Mungu akutie nguvu kwenye hiki kipindi kigumu.Watanzania tuamke hapo ni MNH huko uswekeni hali inatisha jamani tuacheni mchezo,hawa watawala bila show ya maana hawatabadilika
   
 17. Tram Almasi

  Tram Almasi JF-Expert Member

  #17
  Aug 24, 2012
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 755
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hizo hospitali hazina dawa hazina vifaa sasa wanaiba nini,dawa na vifaa hewa? Hivi umeshatembelea hosp na kufanya utafiti wa kutosha? vifaa unavyosema wewe vinaibiwa ni ni vipi?Ultrasound?EEG?ECG?CT Scan? MRI? Echo?Ventilators?Xray machines?Endoscopy? Atrial fibrillator?haemoglobin machine? glucose machine?ICU monitors?Theater beds? C-Arm?Anaesthetic machine? Lab incubators? Blood pressure monitors? ETV machine?Image Intensifiers?theater microscopes?Just to name afew which are basic in a hosp.
  Sasa Mkuu sijui ni vifaa gani ambavyo unasema vinaibwa. Na je, umeshafuatilia kuona ni hospitali ngapi zina vifaa kama hivi na je vinafanya kazi?Na unajua athari za kukosa vifaa kama hivi kwa wagonjwa?
   
 18. B

  Bahati Risiki JF-Expert Member

  #18
  Aug 24, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 531
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli hii inasikitisha na inauma sana. Tunapoteza ndugu zetu kila siku. Hii mifisadi inakimbizana na pesa za walipakodi kwenda kujitibu nje. Kwa nini tugawe dhahabu yetu, mbuga zetu za wanyama zinavunwa, Tanzanite yetu inaondoka, gas yetu inavunwa kila kukicha. Mapato yanaliwa na Kikwete na mafisadi wenzake huku watu wetu wakifa kwa kukosa kifaa kidogo na cha bei ya kawaida kabisa.
  Tuache kupiga midomo tuwageukia hawa mafisadi na kuwaondoa madarakani. Kwa kitendo walichomtendea Dr. Ulimboka kwa kujaribu kutupigania kilitosha kutuamha tushike mapanga.
  Jamani tunaogopa nini? Hawa mafisadi hawana nguvu kiasi hicho. Tuzungumze kwa vitendo. Tuwaweke kapuni hata kabla ya 2015 kwani tunapoteza nguvu kubwa ya taifa hili.
  Angalieni mashuleni. Watoto wetu hawataweza kuumudu ushindani wa technologia katika hali ya kukosa hata dawati. Angalieni vyuo vyetu havina ubora wala havitoi elimu bora. Tunaishia kuchekewa. Jamaa bada ya kucheka anaingia kwenye ndege kwa garama ya kodi zetu kwenda kujivinjari na kutuuza kama maharage yasio ya msimu. Watanzania tunafanya nini? Kwa nini tumwachie Mbowe na Slaa peke yako? Tutoke wote kabisa, tukunje ndita na tulikomboe taifa letu. Hawa mafisadi wanastahili kunyongwa tena hadharani.
   
 19. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #19
  Aug 24, 2012
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Hii ni elimu ya madrasa tu inakusumbua kaka/dada
   
 20. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #20
  Aug 24, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Determine acha hao Madaktari waendelee na mgomo, leo ndio wanaona umuhimu wa kuwahudumia wagonjwa
  kwanza nampa pole huyo aliyepoteza Mgonjwa MUNGU alitoa na MUNGU ametwaa jina la BWANA lihimidiwe
  Pili Kifo kinamkuta yeyote hata mkiweka CT-Scaner Mao aliondoka na wao ni wataalam Hapa tulimpoteza Baba wa Taifa na tulimpenda kuliko MaDaktari
  ukweli Madr iko siku MUNGU atawonyesha kuwa UHAI wa Binadamu sio wa kuuchezea na kumgomea mwenzako asitibiwe eti mpaka milioni 7 wakati mlishaapa kutetea maisha yao
  Kumuona Dr tu ofisini kwake ni TIBA sasa unaingia unakuta wamenuna sasa wanini bora waende huko Botswana kuliko kuendelea kugoma Jamani ondokeni humo Mahospitalini hamjalazimishwa, tutakufa taratibu lakini msijilinganishe na wengine na kujiona bora, Hivi na waJWTZ au POLISI au Walimu nao wakidai au waingie mgomo nani atasalimika
   
Loading...