Daktari Kitila Mkumbo haya ndiyo uliyoyatabiri Uingereza au kuna Mengine Yaja.....

Utoto huu!
Hii ni thread aliyopandisha mwanajamvi hapa!
Kinachotakiwa ni Kauli original, au HyperLink inayoquote alipoongea Live toka huko alikokuwa!
Uswazi wa nini?

Too demanding ulisema watu WaPASTE aliyoyasema Kiltila KIM kafanya hivyo umerudi tena unahitaji KAULI khaaaa muda si mrefu utahitaji na picha ya kikao chenyewe.............
 
dua la kuku,hata uchaguzi uliopita mlisema hapiti ubunge kisa alimtest mchagga mwenzenu mbowe kwenye uenyekiti wa chama...!acheni ukabila nyie,fanyeni siasa.
What a comment!!!

Akili za akina Nape hizi!
 
Zitto, Mbowe, Slaa etc..wote ni CDM na watapita kwenye mchujo kwa kanuni na taratibu za CDM kwa wakati muafaka utakapofika, atakayeshinda ndie atagombea sasa kuna kipi kigeni hapo? CCM wanahangaika sana kutaka kuwagombanisha au kuanzisha mgogoro ndani ya CDM kwa mbinu hizi za kipuuzi na kitoto na sidhani kuwa watafanikiwa kwani CDM ni makini kwa hilo
Mkuu, one thing about CCM ni kwamba wanapenda sana siasa za kuongelea watu!!

Eti ZItto sasa hivi ndio agenda ya kuongelea.........kweli?
Tunamuongelea Zitto?
Kama wao wanavyomuongelea Lowasa??

Huu ni upuuzi wa hali ya juu!
 
Haihitaji degree kujua Zito anamtumikia CCM. Coverage za leo zikishafika Arumeru zitasema kumbe hiki chama wanagombana basi wanapiga kura za hasira kwa CCm. zito anajua fika mwisho wa huu mchezo ni nini! J.K nyerere hakuhitaji kutumia nguvu ili awe Rais. Wazee waliona kijana anafaa. Ukiangalia average age ya kina nyerere wakati wanashika nchi ilikuwa ni miaka 40 kushuka. Ndio maana waandishi wa riwaya za WILLY GAMBA na JORAM KIANGO walipokuwa wakiwakilisha lugha ya picha ya TISS walikuwa wanawaonesha wapelelezi wao kama vijana wa miaka 28 tu! Leo vijana wanaomba kwa nguvu kupewa madaraka huku masikioni wameweka IPOD!

Nakubaliana na wewe 100%. Zitto anamekuwa akionyesha vituko visivyoisha ndani ya CDM. Tukirejea nyuma tunakumbuka matukio kama; 1. kugombea uenyekiti wa CDM huku Mh. Mbowe naye alikuwa akiomba kutetea nafasi yake. Zitto aliwatumia sana kina Kafulila wakati ule kumpigia debe na kwa upande mwingine akipewa coverage na vyombo vya habari. Hatimaye kina Kafulila walifukuzwa kazi pale kwenye Sekretariat ya CDM kwa kitendo kile cha kujitokeza wazi wazi kumpendelea mgombea mmoja (Zitto). Hatimaye Zitto alijitoa dakika za mwizho bila kutueleza kwa sababu gani. Lakini inasemekana alikuwa na fedha zilizoingia katika akaunti yake katia nyakati zile za harakati za kuwania. Mazingira yale ya mikakati ya Zitto yalikuwa yanaonyesha kuwa hakuwa peke yake pale alikuwa na watu nyuma yake na wasi wasi mkubwa ni kuwa alikuwa anasaidiwana CCM kupitia vyombo vyake.


2. Mawasiliano yake ya simu na Zoka (naibu mkurugenzi wa TISS) na Rostam Aziz. Mawasiliano hayo kama sikosei yalikuwa katika kipindi kile cha uchaguzi wa 2010 au kabla ya hapo. Tukujmbuke kuwa Dr. Slaa aliituhumu sana TISS kwa kuisadia CCM katika mikakati ya kuhujumu uchaguzi wa 2010. Je, Zitto ukaribu wake na watu hao yaani TISS na Rostam ulikuwa kwa ajili ya mema kwa CDM na mgombea urais kupitia CDM?


3. Tukio la wabunge wa CDM kususia hotuba ya JK katika kikao cha uzinduzi wa bunge baada ya uchaguzi wa 2010. Katika kadhia ile kabla ya kufikia uamuzi ule wabunge wa CDM walikaa kikao na kupigia kura azimio ile la kutoka bungeni pale JK atakapoingia ukumbini. Hvyo, Zitto siku hiyo hakuhudhuria kabisa kikao kile na hivyo kwenda kinyume na maamuzi wa wabunge wenzake wa CDM kwa kigezo kuwa yeye hawezi kumvunjia heshima rais (JK). Hilo lilikuwa dhahiri kuwa hakuwa pamoja na wabunge wenzake, sasa tujiulize alikuwa upande gani? Hatuna shaka kuwa katika jumuiko lolote la watu hasa katika chama upo ukweli kuwa kutakuwepo na mitazamo tofauti. Tofauti za kimtazamo linaweza hata likawa katika hali ya kuwepo makundi, lakini hayawezi yakawa makundi ya kudumu kama hapatakuwa na maslahi binafsi zinazoleta tofauti hizo.


Tukurejea katika suala la Zitto aliyeungana na Janury Makamba katika hoja ya umri katika kuwania urais, ni wazi kuwa Zitto ana lake jambo. Wazo la Zitto halina ubaya wowote lakini wazo lake hilo naliona kama lina nia nyingine na si la kwake peke yake. Kwanza, wakati huo CDM linapigania utaratibu mzuri na wa haki unaoweza kutupatia Katiba Mpya. Hilo si jambo dogo kwa sababu liliwafanya viongozi wa CDM kwenda hadi Ikulu na hatimaye muswada wa mabadiliko ya sheria ya mapitio ya katiba ukapelekwa bungeni. Hayo mabadiliko bado hayajakidhi hoja zote ambazo CDM walitaka zizingatiwe katika mchakato wa kupata katiba mpya. Pili, CDM wakati huo wapo katika harakati za kushinda katika uchaguzi mdogo wa Arumeru na chaguzi za madiwani. Katika wakati mgumu kama huo kwa CDM, Zitto anapata wapi muda wa kusema anataka urais tena kwa kupewa coverage na magazeti kiasi kile?


Najua Zitto unapenda urais lakini sidhani kama umejitafakari kwamba utauweza urais. Urais utaweza kuupata lakini hautakufaa wewe wala wananchi. Umedhihirisha kwa kiasi kikubwa kwamba ndani tu ya CDM wewe umeonekana kama sababu ya mgawanyiko kulilko kuunganisha. Unachokitafuata katika urais ni nini kama tayari umeonekana kama sababu ya mgawanyiko kuliko kuunganisha? Kuna siku ulitoa maelezo kuwa Marehemu Regia Mtema kuwa ndiye aliyetoa wazo la kumwona rais kuhusu sheria ya mapitio ya katiba, lakini baadaye CDM ilikana kauli yako kwa kusema kuwa wazo lile lilitoka katika kamati kuu ya CDM na Regia Mtema hakuwa mjumbe katika kamati kuu. Ulileta ule uwongo kwa sababu gani? Huaminiki ndani ya CDM wananchi watakuaminije? Kama kweli unautaka urais kwa dhati tafadhali mbinu unazozitumia tunazijua na walio nyuma yako tunawafahamu na huwezi kutudanganya lolote. Rais anayetufaa si wa aina yako. Bado hujatulia.
 
Hizi ni porojo na propaganda za ccm. Dr Kitila ninayemjua mimi angehisi kitu kama hicho angepeleka hoja ya hiyo kwenye vikao vya Chama kama kamati kuu ambavyo yeye ni mjumbe. Mengine story za kujaza server za JF bure.
Mkuu hizi si porojo kama unavyotaka kuiaminisha nafsi yako, nyinyi kama CHADEMA mnapaswa kuwa makini sana na Zitto huyu jamaa yuko behind all this, sidhani kwa mtu mwenye akili timamu CHADEMA iko vitani halafu anatokea kiongozi wa Kitaifa anatangaza habari za kuutaka Urais!! hivi CCM wakitumia hii weakest point yenu kuwamaliza kule Arumeru mtasema CCM wanaiba kura?....
 
sioni hata hoja ya msingi hapo jamani, ninge-comment kama ningeona comment ya Dr Mkumbo mwenyewe juu ya hili.
 
Hizi ni porojo na propaganda za ccm. Dr Kitila ninayemjua mimi angehisi kitu kama hicho angepeleka hoja ya hiyo kwenye vikao vya Chama kama kamati kuu ambavyo yeye ni mjumbe. Mengine story za kujaza server za JF bure.


Kama ulifuatilia thread ile mtoa hoja alikuwa anawasilisha jambo ambalo Kitila Mkumbo analiona mbele ya chadema si kwamba alikuwa anazungumza kwa kuiponda chadema.

Wasomi kama Kitila hawezi kusita kuchanganua changamoto zinazoweza kukikabili chama katika hali ya kawaida bila kupitia vikao hasa kama akiulizwa swali kuhusu changamoto kubwa zilizo mbele ya chadema kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015.

Si kweli kwa chama makini kama chadema kwamba kila jambo litazungumzwa kwenye vikao.
 
- better late than never.....



- "Ukweli una tabia moja nzuri sana. Haujali mkubwa wala mdogo; haujali adui wala rafiki. Kwake watu wote ni sawa. Pia ukweli unayo tabia ya kujilipiza kisasi kama ukipuuzwa. J.k. Nyerere ....Tujisahihishe 1962.


chadema chunga sana kukataa ukweli
 
- better late than never.....



-
“Ukweli una tabia moja
nzuri sana. Haujali mkubwa wala mdogo; haujali adui wala
rafiki. Kwake watu wote ni sawa. Pia ukweli unayo tabia ya
kujilipiza kisasi kama ukipuuzwa. J.k. Nyerere
....Tujisahihishe 1962.

chadema chunga sana kukataa ukweli

Duh! I feel like naming you "The Wise One"
 
Kitila huwa namuona sana kule kwenye jukwaa la wakubwa!! Jamaa anapenda sana yale mambo.
 
... WaTanzania sote TUMESHAAMUA kwamba mambo yote ni kwa CHADEMA, je ni nani tena wa kutuzuia?????????????

Wazee maarufu ndani ya Chama cha Mapinduzi, Dr Hassy Kitine,Mzee Ibrahim Kaduma na Mzee Joseph Butiku wametoa ya mwaka walipokuwa wakihojiwa katika luninga Channel 10, jumamosi.
Habari hii imejirudia katika gazeti la Mwananchi leo(Machi ,26, 2012) ikisema:

"Na Elias Msuya,

Makada watatu wakongwe wa Chama cha Mapinduzi( CCM), Ibrahim Kaduma,Dk Hassy Kitine na Joseph Butiku wameibuka na kukutabiria anguko chama hicho tawala kwa kile walichosema, kwenda kinyume na misingi ya kuasisiwa kwake.

Kauili za makada hao maarufu, zinakuja kipindi ambacho upepo wa kisiasa umekuwa ukivuma vibaya ndani ya chama hicho kikongwe nchini na barani Afrika, kutokana na vita ya makundi kati ya watuhumiwa wa ufisadi na wale wanaojipambanua kwamba ni wazalendo na wapinga."


Maoni Yangu:
Asiyesikia la mkuu huvunjika guu!
 
Back
Top Bottom