Meitinyiku L. Robinson
JF-Expert Member
- Aug 29, 2011
- 412
- 90
Ikiwapendaza wakuu;
Magazeti ya leo yamesheheni juu ya Kauli ya Zitto Zuberi Kabwe na nia yake ya Urais ikielezwa kuwa kauli hiyo inaelekea kukigawa Chama Binafsi bado sijaona tatizo lolote liwalo lile kwa kauli hiyo manake kimsingi kinachoonekana kukwaza ama viongozi wa chama au makada ni swala la muda. Ati huu si muda muafaka nimejaribu kujiuliza muda muafaka ni upi aidha ulioainishwa ndani ya Katiba ama kwenye Sheria nyinginezo ni upi bila kupata majibu.
Ushawishi unaojengwa ni kwamba ati muda huu Chama kiko busy na Kampeni Arumeru Mashariki bado hii haiwezi kuwa hoja manake kama ushindi ni wa Chadema basi utakuwa na kama si Chadema bado itabaki kuwa hivyo hakuna haja ya kuendekeza woga mtu mmoja alishawahi kusema mtu mwoga hufa kabla hata ya siku yake kufikia. Labda ingejengwa hoja kwamba Zitto hashikiri Kampeni na badala yake anajikita na vyombo vya habari hapo tungeweza kufikiria mara mbili lakini Zitto alikuwa Mwanza, Arumeru amekuwepo, sijui Uzini na kwingineko.
Hili ndilo lililonifanya kuwaza na kufikiri kuwa labda yale aliyoyasema Dr. Mkumbo kule Uingereza yakawekwa humu juu ya mpasuko ndani ya Chama ndiyo hayo yanayoanza kuonekana manake tatizo si nia ya Zitto bali Kauli na majibu kutoka kwa viongozi wengine; mathalan Katibu Mkuu ambaye naye anajitahidi kujificha chini ya Mwamvuli wa muda akisema huu si muda muafaka. Yeye anaonekana kuwa mmoja kati ya wanaoungwa mkono kugombea sasa hizi kauli angeacha zitolewa na wanaowatazama manake ni rahisi sana kufikiri kuwa kaamua kusema hivyo kwa sababu naye ni mmoja kati ya wanaoutaka.
Ni wazi kwamba Mshauri Mkuu wa CHADEMA anajua mengi na nahisi aliamua kusema hayo huko kwa sababu yalimfika shingoni aidha kuna ushauri aliotoa juu ya pande hizo zitakazo Uraisi ila ushauri wake ukapuuzwa ama naye kaanza kuandamwa baada ya watu humu kumshauri naye agombee Uraisi.
WanaCDM mtakuwa wakali ila mazee mpende msipende lazima changamoto mzipata, mzikubali na mtafute namna ya kuzitatua lakini mkijifanya kila kitu kiko sawa ama hamtaki yenu yajadiliwe madhara yake ipo siku ya Sirini yatatandazwa nje mchana kweupe......... Na huo ndio mwanzo tu!
Accept critiques and let the same be your best friend and consequently your fault will be easily determined