beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,877
- 6,326
Jeshi la Polisi jijini Mbeya linamshikilia Abdallah Bushiri (42) kwa tuhuma za kujifanya daktari wa binadamu wakati hana taaluma hiyo, baada ya kumkuta nyumbani kwake akiwa na wagonjwa zaidi ya 100 wakisubiri kupatiwa matibabu.
Kamanda wa polisi jijini Mbeya Ulrich Matei amethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo Mkazi wa Igodima jijini humo ambaye anafanya kazi hiyo kinyume na sheria za nchi huku akiwataka wananchi kuchukua tahadhari na kuhakikisha wanaenda kupata tiba sehemu rasmi ili kunusuru maisha yao.
Kamanda Matei amesema daktari huyo feki amekuwa akiwafanyia watu upasuaji ambapo wamemkuta akiwa na fomu za maabara, vipimo vya kupima ujauzito, dawa za kusafisha vidonda, chupa za kuongezea wagonjwa maji na mikasi na dawa zimekwisha muda wake wa matumizi.
Kwa upande wa Mganga mkuu wa halmashauri ya jiji la Mbeya, Bwana.Jonas Lurandala amesema mtuhumiwa Abdallah Bushiri hana taaluma ya udaktari na kuwataka wakazi wa jiji la Mbeya kutoa taarifa za wenye tabia kama hiyo ili kuokoa maisha yao.