Daktari feki akamatwa hospitali ya Amana Dar

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,497
index.jpeg

Mtu mmoja anayejifanya ni daktari katika hospitali ya Amana Ilala jijini Dar es Salaam anashikiliwa katika hospitali hiyo baada ya kukutwa akifanya huduma kwa wa gonjwa bila kibali cha hospitali hiyo hapo. Na pia anawatapeli kwamba atawatafutia ajira.

======

Mkaazi wa jiji la Dar es Salaam, Abdallah Juma aliyewahi kukamatwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) akidaiwa kujifanya daktari amenaswa tena katika Hospitali ya Rufaa ya Amana kwa kufanya kazi katika hospitali hiyo wakati sifa za udaktari hana.

Juma alinaswa jana ndani ya Hospitali ya Amana, majira ya mchana, akijifanya daktari, baada ya kuwekewa mtego na uongozi wa hospitali hiyo.

Kukamatwa kwa Juma kunakuja ikiwa ni miezi mitatu tu imepita tokea Juni 19 mwaka huu alipo kamatwa katika hospitali ya Muhimbili kwa kujifanya daktari.

Katika hospitali ya Muhimbili kijana huyo alijifanya kutoa huduma katika maabara kuu huku uongozi ukiwa hauna taarifa ya kuwepo kwa huduma aliyokuwa akiitoa kitu ambacho kilisababisha kushtukiwa na kukamatwa.

Baada ya kukamatwa Uongozi wa hospitali hiyo ulifanya uchunguzi na kubaini kuwa kijana huyo hakuwa daktari bali daktari feki kama alivyokuwa akijitambulisha na kwamba amekamatwa mara baada ya kuwekewa mtego na askari wa hospitali hiyo. Daktari wa Kitengo cha Watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (WAVIU), Shani Mwaruka alikiri kukamatwa kwa kwa mtuhumiwa huyo.

Alisema, Juma alinaswa baada ya uongozi kupata malalamiko kutoka kwa watu waliokuwa wakihitaji huduma katika hospitalini hiyo.

Alisema tayari hospitali hiyo iliweka mtego imara wa maofisa wake, ambapo Juma aliingia bila hofu yeyote na kukutana na watu ambao alitaka wampe fedha ili awahudumie ndipo aliponaswa.

Baadhi ya watu waliodaiwa kuombwa fedha na daktari huyo feki, wamesema aliahidi kuwatafutia kazi mbalimbali katika hospitali hiyo.

Nae mwananchi aliyekwenda kupata huduma hospitali ya Amana Cecilia alisema Agosti 9 mwaka huu, kijana huyo aliwaeleza kuwa kuna kazi katika hospitali ya Amana na yeye kama daktari bingwa anayefanya kazi hapo anaweza kuwasaidia.

“Alituambia kuwa fomu zinatolewa katika hospitali ya muhimbili sh. 150,000 lakini kwakuwa wao ni madakatari atatufanyia kwa sh. 100,000 tu. Tulichanga fedha hiyo na ilifikia 800,000 tukampatia,”alieza Cecilia.

Aliongeza,Juni 19 mwaka huu aliwaita katika hospitali ya Amana ili kufanyiwa usahili lakini hakutokea na simu akawa hapokei.

“Tuliamua kuuliza kwa madakatari kama wanamfahamu lakini hakuna aliyemfahamu ndipo tulipobaini kwamba tumetapeliwa na kuamua kufanya mtego kwa kushirikiana na uongozi uliofanikisha kumnasa leo ,”alieleza.
 
Back
Top Bottom