TANZIA Daktari Bingwa wa Mifupa MOI na Mwenyekiti wa Kamati ya Tiba TFF, Dkt. Paul Gasper Marealle afariki dunia

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,391
2,000
Tanzia, Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface anasikitika kutangaza kifo cha Mtumishi wa MOI Dkt Paul Gasper Marealle (Daktari bingwa wa Mifupa) kilichotokea usiku wa kumakia tarehe 14/10/2020 katika Taasisi ya MOI. Apumzike kwa Amani

Ma.jpg

Kwa masikitiko makubwa napenda kuwajulisha umma wa watanzania na wadau wa masuala ya afya kuwa Daktari Bingwa wa Tiba ya Mifupa pale MOI, Dkt. Paul Gasper Marealle amefariki dunia usiku wa jana kuamkia leo.

Dkt. Marealle pia alikuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka nchini, Mwenyekiti wa Kamati ya Tiba TFF na Mjumbe wa Kamati ya Tiba.

Binafsi nimemfahamu Dkt. Marealle pale MOI kama Daktari wangu baada ya kufanyiwa upasuaji wa mkono ili kuunganisha mifupa ambayo ilikuwa imevunjika vunjika baada ya kupata ajali mbaya. Aliendelea kunihudumia mpaka pale niliporidhika na maendeleo yangu na kuacha kwenda MOI. Pia alinishauri kutokutoa vipande vya vyuma vilivyokuwa vimeshikilia mifupa ili iunge.

ajali.jpg

Kwaheri Dkt. Marealle
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom