singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza kusimamishwa kazi kwa Daktari wa Kitengo cha Upasuaji katika Hospitali ya Mkoa wa Mtwara ya Ligula, Dk Fortunatus Namahala kwa tuhuma za kumdai mgonjwa rushwa ya Sh 100,000.
Daktari huyo aliibuliwa kwenye kikao kati ya Waziri Mkuu na watumishi, ambako mama mmoja anayedai kudaiwa fedha hizo, aliitwa afanye utambuzi ndipo akaenda kumshika mkono Dk Namahala.
Aidha, Waziri Mkuu ameagiza maduka yote ya dawa yaliyo nje ya hospitali hiyo ya mkoa yafungwe kuanzia jana huku akimtaka Katibu Tawala wa Mkoa huo, Alfred Luanda asimamie suala hilo mara moja.
Daktari anayetuhumiwa
Baada ya Majaliwa kutembelea maeneo kadhaa ya hospitali hiyo na kupokea malalamiko kutoka kwa wagonjwa na ndugu zao, miongoni mwa waliowasilisha kero ni Tatu Abdallah.
Mama huyo alimwambia Waziri Mkuu kwamba amelazimika kuuza shamba la baba yake ekari 2.5, apate fedha za kulipa gharama za kufanya upasuaji kwenye hospitali binafsi baada ya baba yake kutimuliwa kutoka Hospitali ya Ligula; jambo ambalo lilimgusa Waziri Mkuu.
“Februari mosi nilimleta baba yangu hapa nikaambiwa anatakiwa kufanyiwa upasuaji. Nikaandikiwa ninunue dawa za Sh 85,000 hapo nje, pia uzi wa kushonea kwa Sh 25,000. Lakini pia daktari akasema anataka shilingi laki moja ya kwake. Lakini hadi Februari 7 hakufanyiwa huo upasuaji,” alisema Tatu.
Aliendelea kusema, “Tarehe 12 Februari baba alitolewa wodini na kuambiwa arudi tarehe 16 Februari. Niliumia sababu kijiji tunachotoka ni mbali na hali ya baba ilizidi kuzorota. Ndipo baba akaniambia nirudi kijijini kwetu Kilomba nikauze ekari 2.5 za shamba lake ili tulipie matibabu. Niliuza na kumpeleka baba katika katika zahanati ya Sajora. Huko nililipa Sh 560,000 na baba akafanyiwa upasuaji sasa hivi yuko nyumbani”. “Leo nataka huyu daktari aje achukue boksi hili la dawa alizoniandikia na pia anirudishie hela yangu iliyopotea bure. Mie sijazitumia, ni kwa nini aliniandikia wakati baba hajampa huduma yoyote?” Alihoji.
Alipoulizwa kama anaweza kumtambua daktari huyo akimuona, mama huyo alikiri kuwa anaweza.
Akiwa katika kikao na watumishi hao, Waziri Mkuu aliwainua madaktari wote ili wajitambulishe, ndipo akamuomba mama aliyedaiwa rushwa aende kumshika mkono daktari mhusika.
“Gwaride la utambuzi ni jambo la kawaida. RPC hakikisha huyu mama hasumbuliwi. Lakini leo nitaanza na huyu daktari kwa sababu rushwa haivumiliki. RAS simamia suala lake, lakini pia shirikiana na Takukuru na Polisi kufanya uchunguzi wa jambo hili hadi mwisho,” alisema.
Kabla ya kufikia uamuzi wa kumsimamisha Dk Namahala, Waziri Mkuu alitumia muda mwingi kuwaelezea watumishi hao jinsi walivyo na umuhimu katika huduma zao na kwamba nafasi yao ni nyeti kwa maisha ya binadamu, hivyo wanapaswa kuwa na huruma na siyo kuwaumiza wananchi wa kipato cha chini, ambao hawana uwezo wa kumudu gharama za matibabu.
Aliwataka waache tabia ya kuwatoza fedha watoto wanaolazwa hospitalini hapo na wanawake wanaojifungua, kwani wanapaswa kutibiwa bure kwa mujibu wa sera ya Serikali.
Kasoro mapokezi
Awali, Waziri Mkuu aliamua kwenda mojamoja mapokezi, badala ya wodini kama alivyopangiwa.
Alihoji sababu za kuwa na dirisha moja la kupokea wagonjwa wote. “Dirisha la wazee lipo?” alihoji na kujibiwa kuwa halipo. Pia alihoji kama lipo dirisha la wagonjwa wanaotumia kadi za Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), lipo pia akajibiwa kwamba halipo. “Je, wazee wana daktari wao?” alihoji bila kupata jibu.
“Mganga Mkuu ni kwa nini hujatenga dirisha la wazee wakati haya maelekezo yalishatolewa siku nyingi? Tengeni dirisha la wazee na uhakikishe wana daktari wao. Siyo kuwaleta huku ili waje kusukumana na wagonjwa vijana,” alisema wakati akimwagiza Mganga Mkuu wa Mkoa huo, Dk Shaibu Maarifa.
Akiwa njiani kwenda wodi aliyopangiwa kuiona, Waziri Mkuu alikutana na kundi la wagonjwa waliokuwa wakiimba ‘tuna jambo, tuna jambo’ wakiashiria kutaka kusikilizwa.
Miongoni mwa watu wanaouguza wagonjwa wao hospitalini hapo aliowasikiliza, walilalamikia kero za kuuziwa dawa kwa bei ya juu kwenye maduka ya dawa binafsi, lugha mbaya za madaktari na wauguzi, uchafu wa vyoo na uhaba wa maji.
Waziri Mkuu alitembelea pia wodi ya akinamama waliojifungua na kukuta wakiwa wametandikiwa shuka moja na wagonjwa kulazimika kuweka kanga juu ya mipira wanayolalia wodini, ambayo pia wanaambiwa wajinunulie kabla ya kwenda hospitali kujifungua.
Akiwa njiani kwenda chumba cha upasuaji, Waziri Mkuu alipata kilio cha wagonjwa wengine ambao walisema hospitali hiyo haina maji, choo kinachotumika ni kimoja na usafi ulifanyika jana waliposikia kuwa atatembelea hospitali hiyo.
Kuhusu madai na stahili za watumishi, Waziri Mkuu amemwagiza RAS, RMO (Mganga Mkuu wa Mkoa) na Ofisa Utumishi wa mkoa, wafanye kikao na watumishi wote wa hospitali hiyo jana kisha wampelekee taarifa.
Sakata la Hospitali ya Ligula lilianza Februari 27, 2016 wakati Waziri Mkuu alipowahutubia mamia ya wakazi wa Mtwara kwenye mkutano wa hadhara, uliofanyika katika Uwanja wa Mashujaa.
Baadhi ya wananchi walikuwa wakichomekea kuwa aende hospitalini hapo kwa kuwa kuna majipu ya kutumbua. Waziri Mkuu aliwajibu kuwa amesikia ujumbe wao na atakwenda huko, lakini alishindwa kutokana na ratiba za siku hiyo kumalizika jioni. Waziri Mkuu alirejea jijini Dar es Salaam jana.
habari leo