Daktari ashauri msichana wetu wa kazi abebe mimba ili apone...!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,807
2,000
Nina msichana wa kazi anayemsaidi mama Ngina shughuli za nyumbani, tumeishi naye kwa takriban miezi mitatu sasa, ni binti wa miaka 16. Lakini tangu aje amekuwa akisumbuliwa na maumivu makali sana ya tumbo kila mwezi, na maumivu hayo yanadumu kati ya siku nne hadi tano na humlaza kitandani akiwa hajiwezi na hawezi kufanya kazi yoyote. Kila tukimpeleka hospitali alikuwa akipewa vidonge vya kutuliza maumivu, lakini kila mwezi hali hiyo imekuwa ikijirudia.

Sasa jana tulimpeleka kwa daktari mmoja wa bingwa wa magonjwa ya wanawake, ndio akatoa huo ushauri kwamba ili binti wetu wa kazi aondokane na maumivu ya tumbo inabidi azae, la sivyo atakuwa akiumwa kila mwezi........

Sasa sijui tumrudishe tu kwao ili akaolewe azae, lakini hayuko tayari kuondoka anasema hawezi kuondoka mpaka atakapotimiza malengo yake ya kukusanya mtaji wa biashara. Kwani anataka akirudi kwao Mbeya akaanzishe biashara ili aweze kuwasidia wazazi wake.

Hebu nishaurini tumsaidieje huyu binti....?
 

Toria

JF-Expert Member
Aug 1, 2012
1,178
0
Kubalianeni na hiyo off yake ya siku 4-5 kila mwezi,chonde gramps asikwate mshahara kwa hilo!!
 

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,807
2,000
Kubalianeni na hiyo off yake ya siku 4-5 kila mwezi,chonde gramps asikwate mshahara kwa hilo!!
Tatizo akiumwa hapo ndani inakuwa ni kimbwaimbwai maana analia na kuugulia mpaka kero, analalamika sana na sauti yake ilivyo eh.........
 

mwallu

JF-Expert Member
Sep 5, 2013
6,782
2,000
ndio
i have a friend ambae alikua anaumwa hiyo chango..alikua anumwa,anatapika,na anatetemeka baridi mpaka siku zaa hedhi yake zinaisha...alipoolewa na kuzaa tu hiyo hali imekoma
Chango ni ugonjwa au?
 

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,807
2,000
ndio
i have a friend ambae alikua anaumwa hiyo chango..alikua anumwa,anatapika,na anatetemeka baridi mpaka siku zaa hedhi yake zinaisha...alipoolewa na kuzaa tu hiyo hali imekoma
Na yeye anaumwa hivyo hivyo hakuna tofauti kabisa........
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom