Daktari asema Nyama, maharage mekundu hatari kwa afya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Daktari asema Nyama, maharage mekundu hatari kwa afya

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Dec 3, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Dec 3, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,600
  Trophy Points: 280
  ULAJI wa nyama nyekundu hasa ya ng'ombe, pamoja na maharage mekundu ni sababu kubwa zinazosababisha magonjwa ya magoti na viungo.

  Sababu nyingine zinazo sababisha ugonjwa huo, ni pamoja na kuwa na uzito mkubwa pamoja na kutofanya mazoezi.

  Hayo yamesemwa juzi na Mtaalam wa Mifupa na Viungo wa Hosptali ya Aga Khan ya jijini Dar es Salaam Dk Sohail Panawala alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

  Tofauti na imani ya watu wengi kuwa nyama ya Mbuzi ndiyo husababisha magonjwa ya miguu, Dk Panawala alisema, "Ulaji wa nyama nyekundu na hasa nyama ya Ng'ombe uwezekano wa kuwa na matatizo ya miguu ni mkubwa sana,".

  Mtaalam huyo ambaye toka aingie nchini mwezi Februari mwaka huu, ameshafanya upasuaji kwa zaidi ya wagonjwa 100 na wengine wengi kupatiwa matibabu yasiyo husisha upasuaji.

  Alisema kutokana na ukubwa wa tatizo la miguu na viungo nchini, mara kadhaa hulazimika kuwa na kliniki ya bure ya mifupa na miguu, ili kutaka kubadilishana mawazo na wagojwa pamoja na matibabu.

  Dk Panawala pia alionya juu ya matumizi ya madawa ya kupunguza maumivu, kuwa ni hatari na kuwa huzalisha magojwa mengine.

  "Unajua madawa yote yana kemikali na kawaida ya kemikali huwa na madhara (side effect) katika mwili wa binaadamu, tatizo la watu kutumia madawa ya kupunguza maumivu lipo duniani kote lakini ni bora mtu ukiumwa mara moja aende hospitalini ama katika kituo cha afya apate matibabu," alisema Dk Panawala.

  Hospitali hiyo ya Aga Khan pia, imefanikiwa kuwafanyia upasuaji wa ubongo, zaidi ya wagonjwa 20 kwa kipindi cha miezi minne.
  Mbali na wagonjwa hao, waliopatiwa fanyiwa upasuaji pia wagonjwa wengine zaidi ya 200, wamefanyiwa vipimo mbali mbali vikiwemo vya ubongo na uti wa mgongo.


  Chanzo: Mwananchi
   
 2. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #2
  Dec 3, 2009
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  huyu dokta anataka kuuwa soko la maharage. acha nitafte wafuasi tuandamane.
   
 3. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #3
  Dec 3, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  That being the case vijana waliopitia boarding wote wangekuwa na hayo matatizo bse maharage nod ilikuwa daily
   
 4. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #4
  Dec 3, 2009
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mwishowe atatokea mwingine atasema kuishi ni hatari kwa afya! Too much wanataka tunywe maji tu tulale....inawezekanaje? Maharage ndio mboga yetu ya kujidai uswazi..........wanataka tule nini?
   
 5. Bernard Rwebangira

  Bernard Rwebangira R I P

  #5
  Dec 3, 2009
  Joined: Feb 15, 2009
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Maharage yajulikana kama Mboga ya Taifa maana mashule yoooote, magereza, na hata mahospitali ya G ndo mboga yao. si tulikuwa twala maharage mara saba kwa wiki shuleni, ikibadilishwa basi ni mapande ya kabichi ya kwa taaabu sana "SUPU" sio nyama ni supu maana ikiwa siku ya nyama (ambayo ni mara moja kwa mwezi ama kwa temu) ni kasheshe, labda tatizo kubwa lilikuwa ni kuona usiku maana kuna jamaa ilikuwa ikifika jioni tu basi inabidi umshike mkono kumrejesha bwenini, ila sijawai kuona ama kusikia magonjwa ya miguu.

  Huyu Dr ataka kutuulia mboga zetu, maana uswazi mbali ya sukuma wiki ni nyama na maharage tu ndo zinatamba.
   
 6. bht

  bht JF-Expert Member

  #6
  Dec 3, 2009
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  Labda angeenda mbele zaidi kwa kutuambia madhara hayo yanaanza kujitokeza baada ya mda gani vinginevyo mi nahisi analake jambo....tumekuzwa na maharage wengi wetu na bado ndo mboga kubwa kwetu so far!!!

  nyama naweza kukubaliana nae...si nzuri kwa afya!!!

  MAHARAGE MEKUNDU......MMH atanisamehe
   
 7. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #7
  Dec 3, 2009
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,468
  Likes Received: 4,127
  Trophy Points: 280
  Kama ni kwenye suala la maharage nadhani tungekuwa na matatizo hayo muda mrefu, kwani maharage imekuwa ni sehemu ya maisha kama gesi ya oksijeni ilivyo ya muhimu.
   
 8. s

  superfisadi JF-Expert Member

  #8
  Dec 3, 2009
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 552
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  duh kila kitu hatari ndani ya ulimwengu huu
   
 9. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #9
  Dec 3, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  maharage mekundi tena sasa naona kila chakula ni hatari na kina madhara

  Tufanyeje sasa ?
   
 10. bht

  bht JF-Expert Member

  #10
  Dec 3, 2009
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  apparently kila tulacho ni sumu mi naona tuendeleee kula kula vyote tu...matokeo mbele kwa mbele. maan utaacha hiki kinadhuru mifupa , kingine kinaleta kansa, kingine swane flu, liver/kidney failure and so much more!!
   
 11. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #11
  Dec 3, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  kweli bht naona kila tunachokula hakipo salama hata kidogo
   
 12. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #12
  Dec 4, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Tunywe na kula LOSHORO tu sasa
  I think hiki chakula ndio solution pekee ya matatizo haya
   
 13. L

  Lady JF-Expert Member

  #13
  Jul 19, 2010
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 280
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Thanks for information, Dr. Panawala bado yupo Aga Khan Hospital?
   
 14. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #14
  Jul 19, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  vegeterianism..............??!!!
   
 15. w

  wasp JF-Expert Member

  #15
  Jul 19, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 206
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wamasai, Wahadzabe etc wanakula nyama ya kuchoma miaka nenda rudi na bado hawalalamiki kuhusu gonjwa la gout. Tatizo linatokana na watu kutofanya mazoezi.
   
 16. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #16
  Jul 19, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Sawa nyama nyekundu na maharage (Leave alone mekundu) yana hatari kwa afya ya binadamu. Mganga wako huyo mkuu Mzizimkavu ama anakosea kuharamisha jumlajumla au waliomnukuu walinukuu jumlajumla.

  Hakuna kizuri kisichokuwa na ubaya; kama vile hakuna kibaya kisichokuwa na uzuri kabisa. Hata shetani pamoja na ubaya woooote tunaomsukumia, wapo wanaouona uzuri mwingi tu, japo kwa masharti pengine magumu kwa walio wengi kuyafikia.

  Nilitegemea kuelezwa kwa kina juu ya ubaya huo na pia nielezwe uzuri wake ili jamii isichanganyikiwe, kwani kumwambia mtoto sukari ni tamu haitoshi bila kumweleza hatari za sukari hiyo. Sawa na kuwaambia watu wasijamiiane usiwaambie hata mbadala ili wanachokipata katika kujamiiana wanawezaje kukipata kwa mbadala. Kuwaambia watapia mlo wale nyama kwa wingi na mayai na samaki ili kupata protein wni vema kabisa, hapo panatakiwa kuwaambia pia kwamba kiasi gani kinafaa. Hata ugali ukiula kupita kiasi ni sumu. Anything in excess is harmful, hata chai ukinywa kupita kiasi utalewa - cumulative effect ya constituents.

  Sukari ni nzuri na muhimu sana ikiwa frequency of intake is moderate. Ukitumia sukari kilo moja mara moja kwa siku uko salama zaidi kuliko anayetumia kilo moja hiyohiyo spread over 24 hours - mfano kutoboka meno (Dental caries). Wataalam watafiti wanasema sukari ikitumiwa zaidi ya mara tano kwa siku ni hatari kwa afya ya meno yako. lakini sukari ni carbohydrate inayohitajika sana kwa kuupa mwili nguvu. Mwenye kisukari ni hatari kutumia sukari aina ya sucrose au yoyote yenye kuongeza calories nyingi mwilini.

  Nyama na maharage ukiacha kula unapata utapiamlo wa aina ya protein. Kwashiokor ni jina walilopewa watapia mlo wa protein kule west Africa na likachukuliwa jumlajumla kwa watu wa aina hiyo wa duniani kote kwa marejeo ya bara la Afrika ambako watu wa aina hiyo ni wengi zaidi. Ukila kupita kiasi nyama nyekundu unajihatarishia gout na matatizo kadha mengine, maharage ukizidisha unajihatarishia ukubwa wa tatizo la vidonda vya tumbo (Peptic ulcers) inayochangiwa pia na ugumu wa gastric acid kuyeyusha maganda hayo ya maharage, inapotokea acid hiyo kutengenezwa kwa wingi ili kuyeyusha maharage hayo hujikuta mucus membrane ya njia ya chakula inadhoofishwa na hapo ni tatizo.

  Nimesema kwa kifupi tu kusisitizia kwamba wataalam tunawapotosha jamii tunapofyatua single sided maelezo juu ya vitu tunavyoelezea. Tujifunze basi kuelezea faida na hasara ya kila tunachokisemea ili watu wanaotusikiliza wapate nafasi ya kuchagua in a radical manner.

  Taarifa hiyo iliyoletwa ni nzuri kwa kuwa inatufanya kupata kitu cha kujadili, lakini inawavua nguvu ya kutafakari walioko nje ya fani ya afya ambao tunayo dhamana kwao kuwaelimisha na wala sio kupigia debe upande mmoja kama vile wanasiasa wanavyotaka tumchague mmoja tu anayeelezwa kwa uzuri wake na wala hajisemei ni mbaya kiasi gani ili tumpime kwenye mizani kabla ya kumchagua. Ndio maana siasa sio professionalism ya ukweli japo nayo ni science.
   
 17. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #17
  Jul 19, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Huyo mhindi si anaabudu ng'ombe? Watu wamekula nyama na maharage miaka nenda rudi na wameishi miaka kibao. Cha msingi kile ulacho ukifanyie kazi. Huyo dokta anasema kafanyia upasuaji watu zaidi ya mia. Aangalie aina ya hospitali na wanaoenda hapo kupata tiba atagundua ni vibosile wenye muda wa kula tu lakini hawana muda wa mazoezi. Nyama na maharage vitaliwa siku zote. Kesho watasema samaki si wazuri sababu maji ya bahari si salama
   
 18. u

  urassa Member

  #18
  Jul 19, 2010
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inatisha, lakini ni bora kusikiliza ushauri wa Dr kwa sababu siyo lazima uishi kwa kula nyama.
   
 19. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #19
  Jul 19, 2010
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mi sijui lkn sijawahi kuona masai alie ugua ugonjwa wa miguu wakati wanakula nyama mbichi,cha msingi mazoezi nduguzanguni
   
 20. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #20
  Jul 19, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  Mwandishi kaandika habari ndefu bila kuandika kwa nini nyama na maharage mekundu ni hatari.
   
Loading...