Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,805
- 4,484
Daktari kutoka nchini Zambia Joseph Kabungo ambae jana alikuwa ofisa wa CAF katika mchezo wa kufuzu kombe la Dunia baina ya Nigeria dhidi ya Ghana amepoteza maisha kutokana na vurugu zilizofanywa na mashabiki wa Nigeria mara baada ya mchezo huo kuisha kwa sare ya 1-1 na Ghana kufanikiwa kufuzu kombe la Dunia.
Kutokana na vyanzo mbalimbali vinaripoti kuwa mashabiki wa Nigeria walimpiga wakati wakilazimisha kuvamia ndani ya eneo la kuchezea kitu kilichompelekea apoteze fahamu na baadae kufariki.
===
Chama cha Soka cha Zambia (FAZ) kimethibitisha kifo cha Ofisa wa Afya, Joseph Kabungo ambaye alipoteza maisha katika vurugu zilizotokea katika mchezo wa Nigeria dhidi ya Ghana, jana Machi 29, 2022 kwenye Uwanja wa MKO Abiola Jijini Abuja, Nigeria
Vyanzo mbalimbali vinaripoti kuwa mashabiki wa Nigeria walimpiga wakati wakilazimisha kuvamia ndani ya eneo la kuchezea kitu kilichosababisha apoteze fahamu na baadaye kufariki
Nigeria ilipata sare na hivyo kukosa nafasi ya kucheza Kombe la Dunia 2022, hivyo mashabiki wakawa wanaingia uwanjani kuonyesha hasira zao mara baada ya fiimbi ya mwisho
Source: African Football Greats.