Daktari anapotumia muda mwingi kutibu dalili kuliko chanzo cha maradhi... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Daktari anapotumia muda mwingi kutibu dalili kuliko chanzo cha maradhi...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ntemi Kazwile, Jul 4, 2011.

 1. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #1
  Jul 4, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Taarifa ya serikali kuwalipa fidia wafugaji wa Longido, Monduli, na maeneo mengine ya mkoa wa Manyara ni kielelezo kingine kuwa uchaguzi ulitakiwa ufanyike tena mwakani, ili tupate serikali itakayotutoa hapa tulipo kutupeleka nchi ya ahadi.

  Vifo vya mifugo hutokana sana sana na ukosefu wa malisho na maji, siamini kuwa watendaji wetu wanaruhusu wanasiasa wachote Tzs8-9 Billions kulipa kifuta jasho kwa waliofiwa na mifugo yao kutokana na ukame (hapa bado sijatamani kujua namna hawa walengwa watapatikana bila kiasi kikubwa cha fidia hii kuishia mikononi mwa wachache).... mwaka huu kuna janga jingine la ukame mkali mikoa ya Shinyanga, Mwanza, Singida na kwingineko na huenda nao wakadai fidia, hapa kabla hatujapata maombi ya fidia kutoka kwa wakulima ambao mazao yao yameharibiwa na mvua au mifugo yao kupigwa radi.... hapa kabla hatujapata tiba ya kansa inayoitwa umeme...

  Ukiona serikali inatoa fidia, ni dalili kuwa kuna mambo hayako sawa... kwa nini wasijenge mabwawa kukinga mifugo isikose malisho na maji kwa mfano? Au kwa nini wasiwekeze kwenye kuzuia ukame kwa kupanda miti?

  Ni Kikwete na serikali yake tu ndio wanaweza kuyajibu maswali haya machache na mengine ambayo yapo kuhusu kadhia ya fidia kwa wafugaji.... nchi hii inahitaji serikali mpya! CCM na Kikwete wameshindwa na tunahitaji timu nyingine haraka kabla ya 2015, ikiwezekana uchaguzi ufanyike 2013 ili tuepuke fedheha ya maamuzi haya ya kishetani!
   
 2. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #2
  Jul 4, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Walilipa stimulus package kwa wakulima wa pamba lakini hakuna mkulima aliyenufaika na hiyo package, sasa wanahamia kwenye mifugo
   
Loading...