Faith
Member
- Jul 9, 2008
- 52
- 11
Daktari asakwa kwa kumbaka mgonjwa
2008-08-12 11:13:27
Na Lulu George, PST Tanga
Daktari wa zahanati ya Manundu iliyoko katika Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga, anatafutwa na polisi kwa tuhuma za kumbaka mgonjwa wake.
Daktari huyo aliyetambulika kwa jina moja la Mkenga, anadaiwa kumbaka binti mwenye umri wa miaka 19 ambaye alikwenda katika zahanati hiyo kwa matibabu.
Akitoa taarifa hiyo ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Bw. Nyakoro Sirro alisema tukio hilo lilitokea Agosti 9, mwaka huu saa 6:00 mchana.
Kamanda Sirro alisema inadaiwa kuwa, siku ya tukio, msichana huyo ambaye ni mfanyakazi wa ndani, alifikishwa katika zahanati hiyo na mwajiri wake kutokana na kusumbuliwa na tatizo la kuchekacheka ovyo.
Hata hivyo, alisema baada ya mgonjwa huyo kupokelewa katika zahanati hiyo, daktari alimtaka mwajiri huyo aondoke na amwache mgonjwa kwa madai kuwa, tatizo lililokuwa likimsumbua ni dogo tu ambalo angeweza kulipatia tiba ya haraka.
Kwa mujibu wa Kamanda Sirro, mwajiri wake aliondoka na kurejea baada ya saa nne na kumkuta binti huyo akiwa ameacha kucheka cheka na hivyo waliondoka na kurudi nyumbani.
Hata hivyo, alisema binti huyo alianza kulalamikia kupata maumivu makali sehemu zake za siri akidai amebakwa na daktari wa zahanati alikopelekwa kwa tiba.
``Baada ya kufika nyumbani, inaonekana binti huyo alianza kulia maumivu makali na baada ya kuhojiwa na mwajiri wake ndipo alipoeleza kitendo alichofanyiwa hospitalini,`` alisema.
Alisema walienda polisi na daktari alipofuatwa kazini kwake, hakupatikana na inavyoelekea alitoroka.
Wakati huo huo, Khalfani Ali, mkazi wa kijiji cha Kiruku, Wilaya ya Tanga, anashikiliwa na polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi mwenye umri wa miaka 17 anayesoma darasa la saba katika Shule ya Msingi Kiruku.
Kamanda Sirro alisema tukio hilo lilitokea Julai 30, mwaka huu saa 6:01 mchana katika kijiji cha Kiruku ambapo mtuhumiwa alimvizia njiani binti huyo wakati akitokea shuleni.
Alisema mtuhumiwa huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya polisi kukamilisha upelelezi.
SOURCE: Nipashe
http://ippmedia.com/ipp/nipashe/2008/08/12/120412.html
hii ni hatari kwa kweli au ndo alikua anamtibia?