Daktari aliyetoa mimba ashtakiwa kwa kutakatisha fedha

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Dar es Salaam . Daktari, Awadhi Juma (40) kutoka Hospitali binafsi ya Dental Clinic, iliyopo Sinza Mori, Dar es Salaam na muuguzi mmoja, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashtaka saba likiwamo la kutoa mimba wagonjwa na kutakatisha fedha kiasi cha Sh260,000.

Mbali na Juma, ambaye ni mkazi wa Kunduchi Salasala, mshtakiwa wa pili ni Kidawa Ramadhani (26) ambaye ni muuguzi na mkazi wa Manzese.

Washtakiwa hao wamefikishwa mahakamani hapo leo Ijumaa Desemba 27, 2019 na kusomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi, Vicky Mwaikambo.

Kabla ya kusomewa mashtaka yao, Mwaikambo amesema washtakiwa hawatakiwi kujibu chochote kutokana na Mahakama ya Kisutu kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi za uhujumu uchumi isipokuwa kwa kibali maalumu kutoka kwa DPP.

Akiwasomea hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon akisaidiana na Glory Mwenda, amedai washtakiwa hao wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 139/2019.

Pia, katika tarehe tofauti, Agosti 2002, jijini Dar es Salaam, mshtakiwa Juma kwa lengo la kudanganya, alighushi cheti cha Diploma cha Utaalam wa tiba ya Kinywa akionesha ni halali na kimetolewa na chuo cha tiba cha Muhimbili wakati akijua si kweli.

Katika shtaka la kutakatisha fedha, Juma anadaiwa kati ya Mei 2015 na Desemba 4, 2019 alijipatia Sh 260,000 wakati akijua fedha hizo ni zao la kosa la jinai la kugushi.

Simon alidai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na Hakimu Mwaikambo, aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 10, 2020 itakapotajwa.

Washitakiwa wamerudishwa rumande kutokana na shtaka la kutakatisha fedha kutokuwa na dhamana kwa mujibu wa sheria.

MWANANCHI
 
Kwa hali hii hakuna Mtanzania ambaye si mhujumu uchumi na mtakatishaji fedha. Ni suala la muda tu. Huenda siku za usoni iwapo mambo yataendelea hivi, basi watanzania tulio wengi tutaonja tu machungu ya hii sheria tatanishi.
 
Kuna haja ya kuchora mstari kisheria juu ya money laundering, pesa yoyote iliyopatikana kwa njia isiyo halali kisha ikaingizwa kwenye mfumo halali inakuwa imetakatishwa.... kama ni hivyo basi hata pesa ya WIZI inaingia hapo..?
 
kesi za money laundering ni chanzo cha mapato cha serikali ya awamu ya tano.
Ña nyinyi Kwa kulaumu mmedhidi kwakweli, mmekuwa mazuzu, we unaona alichokuws anafanya uyo dokta fake ni sawa??? Mí nna ndugu yangu aling'olewa jino kimakosa akafariki,
sasa ivi amuoni alichokuwa anafanya uyo daktari fake ni ni hatari katika , unachezea ña afya au uzima wa raia ni sawa umehujumu uchumi. Uchumi ni watu tena wenye afya njema, sasa yeye ni daktari feki, ña alikuwa analipwa ela halali Kwa njia haramu, kwaiyo uyo ni mtakatishaji fedha ña muhujumu uchumi,,,, tuache ujinga wa kukosoa kila kitu hata ambacho hatuna elimu nacho ,Lol
 
Kwanza, punguza jazba alafu kunywa maji robo lita, alafu washa feni upumue vizuri.
Pili, hakuna popote nilipolalamika bali nimetoa maoni yangu na pia sijamtetea daktari huyo mtoa mimba.
Tatu acheni kuliwa bila condom na ikitokea mmebeba mimba zaeni acheni kuuua viumbe vya Mungu visivyo na hatia.
 
😂😀😁😁
 
Mimi nilidhani angeshitakiwa kwa kosa la kutakatisha CV na tumbo la demu!!! Utakatishaji pesa unaingiaje hapo?
Mkuu hili neno wengi linawatiza.

'Kutakatisha' ni kukifanya haramu kiwe halali.

Sasa kujipatia pesa kwa kutoa mimba ni kujipatia kipato kwa njia haramu.
Na huyu bw mdogo kalibeba isee!

Wamempekenyua hadi mavyeti! Nadhani aliwaletea ujuaji, loh!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mi mpaka leo sijaelewa kutakatisha fedha ni nini mwenye uelewa anisaidie
 
Back
Top Bottom