Daktari aliyeishi na mzoga kwa miaka saba

Acha porojo saivi kikosi kazi tuko busy na ajenda moja tu
FB_IMG_15890502447690498.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Heshima shukrani,na utukufu kwake yeye aliyeumba mbingu na dunia
Hapa namuongelea Mwenyenzi Mungu siyo (Allah)
Pili niwape pole kwa wiki nzima ya kunawa mikono na kuvaa barakoa bila kuchoka...

Hii yote ni kujikinga na janga la Dunia la Covid-19

Nitoe pole pia kwa we wenzangu tuliokunywa chai bila sukari takribani wiki sasa

TWENDE....
Bila shaka umeshakutana na vioja vingi sana ila ki ukweli hiki ni bab kubwa yani
Unakataa???? acha ufala yani
Kama chako kinatisha zaidi basi weka tulinganishe

Huyu Dactari sijui nini kilimtesa ila
Tusichoshane funga
Fuatilia mwenyewe ujue alikuwa na tatizo ganiii

Mzgo unaanza hivi..
Uko tayriiiiii......


Miaka miwili tu ilitosha kwa Maria kukaa kaburini. Jioni moja bwana Tanzler alienda na toroli pale kaburini, akauchukua mwili wa Maria...kisha akarudi nao nyumbani, aliuhifadhi kwa madawa na vinukishi..na kisha akaishi nao kama mme na mke
Mnajiauliza ilikuwaje kuwaje kinjekitile70 ???
mimi pia sijui
Ila tushuke tuuu


Huyu dactari aliyekuwa amechukua maamuzi hayo aliitwa Carl Tanzler huku akifahamika kwa majina mengine kama Count Carl Von Cosel,
Alizaliwa mnamo mwaka 1877 nchini ujerumani kabla ya kuhamia nchini marekani ilipofika mwaka 1926. Amapo mauti yalimkuta mwaka 1952 akiwa na umri wa mika 75(alitumiza miaka yaahadi ya biblia na kichele yani) .

Akiwa kijana mdogo tu nchini ujerumani…Carl Tanzler anapata pigo la kumpoteza mpenzi wake.. ambae binafsi aliamini atakua ndiye mwanamke wake wa maisha. Taswira ya binti huyu alokua tulizo la nafsi yake..ilimtesa kwa muda mrefu, kwani mara kwa mara ilimtokea machoni kwake.

Akiwa anafanya kazi katika.


hospitali ya Marine nchini Marekani…. Mwaka 1930, Tanzler anakutana na binti mdogo mwenye umri wa miaka 22mtoto mbichi kabisaa.

Binti aliyeletwa hospitalini na mama yake kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya ugonjwa wa kifua kikuu.
Urembo wa binti huyu ulichagizwa na nywele nyeusi zilizojaa kichwani kwake


tena zilizokoza haswa, machoni mwa Tanzler binti huyu alikua ni kama yule mpenzi aliempoteza akiwa kijana mdogo kabisa katika nchi ya Ujerumani. Binti ambaye taswira yake ilimtesa Tanzler kwa miaka. Binti huyu Aliitwa Maria Elena Milagro de Hoyos.

Kwa wakati huu (sema ennhee syo kukaa kimya tuuh)


ilikua ni kama Tanzler ameokolewa katika kifungo cha kutokewa na taswira ya mpenzi wa zamani. Kila alipomuona Elena de Hoyos ilikua ni kama anamuona mpenzi wake aliefariki miaka mingi iliyopita(mirror image).

Alihisi kama dunia imempatia nafasi ya pili….

Maskini Tanzler, kwani kwa wakati huu
pia bahati haikua yake, Maria Hoyos alisumbuliwa na ugonjwa wa kifua kikuu..ugonjwa ambao ulionekana kuwa ni hatari Zaidi duniani kwa kipindi hicho..ulisababisha vifo vingi na ulikua ngumu kutibika (kama Corona sahvi).

Kwa kuvutiwa na uzuri wake Tanzler alitumia ujuzi wake wote alokua nao katika taaluma ya utabibu.
Aliomba ridhaa ili aweze kumptia Elena De Hoyos matibabu maalumu nyumbani kwao. Alimpatia matibabu Maria de Hoyos nyumbani kwao kwa wazazi wake..kwa madawa tofauti tofauti alitumia,vifaa vya umeme na X-ray ambavyo vyote aliomba vipelekwe nyumbnai kwao Maria de Hoyos.


Kwa kipindi hiki cha matibabu, Tanzler alimpatia Maria de Hoyos zawadi mbalimbali, mikufu, mavazi na mapambo mengi ya maua. hakutaka kubaki kuwa mzembe, alikiri hisia zake kwa dada huyu ambaye siku zake duniani zilikua ni zenye kuhesabika..

lakini hakuna ushahidi wa kuwa maombi yake haya yalikubaliwa.

waswahili waliwahi kusema, juhudi za mwanadamu kamwe haziwezi kupangua mipango ya mwenyezi.

Ilipofika Oktoba 25 mnamo mwaka 1931, nyumbani kwa wazazi wake..Maria de Hoyos alipoteza maisha (tuweke msiba kwanza ama vepee)
Ngoja niliee

.

Bwana Carl Tanzler alilipia gharama zote za mazishi na kwa ruhusa ya wazazi wake alijenga kijumba kidogo ambacho ndani yake ndipo mwili wa Maria de Hoyos uliweza kuzikwa.

Baada ya kuzikwa, Tanzler alionekana akiingia ndani ya chumba hicho cha kaburi karibu kila siku.
Alitumia kemikali za kitabibu(sijui kama formalin pia ilihusika) na madawa mengine kuuwekea mwili huu wa binti mrembo aliepoteza maisha katika umri mdogo tu.

Lengo lake ni kuusaidia uweze kudumu kwa muda mrefu lakini, jioni moja mwezi April mwaka 1933 miaka miwili baada ya mazishi ya Maria, Tanzler aliingia ndani ya kijumba cha kaburi la Maria de Hoyos na akautoa mwili wake mahali ulipolazwa
kisha kigiza kilipoingia aliubeba kwa kutumia kitoroli na kuupeleka hadi nyumbani kwake ambapo aliulaza katika kitanda ambacho yeye alitumia kulala siku zote.

Nimechoka kuelezea mambo ya msiba
Sijaona hata mtu anatoa rambirambi yani
Tuache usenge...

Oky tuendelee



Mifupa ya marehemu Maria de Hoyos alianza kuiunganisha kwa waya,
kisha macho aliyafunika kwa mfano wa miwani ndogo zilizoonesha mfano wa macho yaliyofumbua.

Kadiri ngozi ilivyozidi kuoza na kupukutika..bwana Tanzler aliirudishia kwa kutumia nta na vitambaa vya hariri na hivyo kuendelea kulilinda umbo la marehemu Maria ,jamaa alikuwa na moyo mgumu sana yani
Mimi kuangalia maiti tuu siwezi yani......

Nywele ziliponyonyoka kutoka kichwani kwa marehemu, Tanzler alizikusanya na akatengeneza wigi kisha akalivalisha katika masalia ya fuvu la Maria de Hoyos. Na Kwa kutumia vipande vya gunia, Tanzler alizifunika na kushindilia sehemu za mwili wa Maria ambazo zilionekena kutengeneza vijishimo ama kusinyaa..kama kifuani na tumboni.

Akiwa kama mtu aliechizika na pepo la mapenzi Tanzler aliuvalisha mabaki ya mwili wa Maria de Hoyos mavazi mazuri na vito vya thamani tena vya kuvutia, gloves katika mikono na viatu katika miguu.

Kwa kiasi Fulani alilirudisha umbo la Maria katika uhalisia na kisha vizuuri akaulaza mwili huu katika kitanda chake huku akitumia Pafyumu, na dawa za kuua wadudu na kuzuia harufu kali ili kutuliza harufu ya mabaki ya mwili wa binti huyu ambae alikua anaoza.
Na hapo akaanza kuishi nao kama mtu anavyoishi na mke wake,yaani jamaa alianza kumtafuta utamu marehemu,daa hizi nyege jamani nyie

Kiufupi mwenendo wake ulikua kama wa mtu aliechanganyikiwa, alionekana akinunua mavazi na mapambo ya kike na huku alikua akiishi mwenyewe nyumbani kwake, na baada ya muda kazini pia alifukuzwa.

Uvumi wa kuwa bwana huyu alikua akiishi na
mwili wa mwanamke ulienea. Kuna kijana mmoja aliwahi kumuona bwana Tanzler akicheza mziki na kile kilichoonekana kama ni mdoli mkubwa wa mwanamke huku dirisha lake likiwa wazi (inasemekana walikuwa wanacheza wimbo YOPE).

Ilipofika mwezi wa 10 mnamo mwaka 1940, mwanadada Florinda ambaye alikua ni dada wa marahemu Maria de Hoyos alisikia uvumi wa kuwa bwana Tanzler alikua akiishi na mwili ambao ulifanana Dhahiri na mdogo wake Maria.
Alienda nyumbani kwa Tanzler kwa kushitukiza na alipokagua alikuta ni kweli Tanzler aliishi na masalia ya mwili wa mdogo wake Maria de hoyos.

Florinda alitoa taarifa kwa mamlaka husika na bwana Tanzler alikamatwa na kufikishwa katika vyombo vya dola.
Kabla ya yote walimfanyia vipimo vya akili na walipogundua ni mzima..alisimamishwa mahakamani kwa kosa la kuvunja kaburi na kuutoa mwili bila ruhusa za mamlaka.
Jamaa atachomoka kweli kwa hii kesi?




Baada ya kesi kusikilizwa octoba 9 mwaka 1940, Tanzler alijibu mashitaka yaliyowekwa juu yake na hata hivyo kesi hii ilitupiliwa mbali na mahakama.

Mwili wa maria ulifanyiwa uchunguzi na madaktari na punde, habari za chizi huyu wa mapenzi bwana Tanzler zilienea maeneo yote katika nchi ya marekan.

suala hili lilifanya Zaidi ya watu 6800 kuhudhuria kuona mwili wa Maria ulipotolewa kuonwa watu kabla ya kufanyiwa maishi ya siri katika kaburi ambalo halikutambulika ili kuepusha uharibifu mwingine.

Kwa mujibu wa maoni ya madaktari walioufanyia uchunguzi mwili wa Maria mwaka 1940 walisema mfano wa bomba fupi liliweza kuingizwa katika sehemu za ukeni za Maria na hivyo kuwezesha tendo la ndoa kufanyika. Ambapo inaaminika bwana Tanzler alifanya tendo la ndoa na masalia ya binti huyu maria. Hata hivyo, hakushitakiwa kwa makosa ya udhalilishaji kwakua.

hakuna picha iliyopigwa wakati mwili huu wa Maria ukiwa unafanyiwa ucunguzi na madaktari hivyo madai haya yalikosa ushahidi.

Nimechoka kuandika wakuu
Ngoja kwanza nikazie swaumu
Si unajua mimi KOBE

ntakuja badaye kumalizia huu mkaa

Angalizo

Kama nimekukera katika uandishi
Wewe kereka tuuh mpaka siku ulete uzi wako prefect hapa......

Kuhusu mambo ya dini hapa si mahali pake walahi

Pia msisahau kunawa mikono na kuvaaa barakoaĂ a

Hizi ni baadhi ya picha View attachment 1445826View attachment 1445827View attachment 1445828View attachment 1445829View attachment 1445830View attachment 1445831View attachment 1445832View attachment 1445833

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakyanani
 
Back
Top Bottom