Daktari alipotoa simu yake na kuanza kuchat nikimwelezea shida yangu

Lumbi9

JF-Expert Member
Oct 12, 2014
8,547
11,766
Nimeingia kanikaribisha kwa bashasha, nikaketi nikampa kadi kaweka mezani katoa simu, nikatulia nikijua labda anaweka silent, kama dakika moja ikapita nikamshtua "dokta", akasema ongea nakusikiliza.

Ikabidi niongee tu japo namuona kabisa mtu 'amekosentreti' kwenye simu yake, hanisikilizi wala haandiki, ikabidi nami nitoe simu yangu, baada ya kimya kama cha sekunde 20 kashtuka, ananiuliza mbona huongei, nikamwambia nishaongea nilifikiri unaandika kwenye simu, akajishtukia, kaweka simu kwenye koti

Ananiambia unajua nina matatizo flani, nikammwambia kawaida (sikutaka ku-argue naye sana as long as ujumbe kashaupata) kaweka kadi vizuri kaanza kuandika, moyoni najisemea dokta leo umetoa boko.
VITU VINGINE HAVITAKAGI UJUAJI
 
Wewe Dk mm mahakamani nipo anasikiliza kesi huku anachat yani within 3mins kashaandika kila kitu

Kashaandika kila kitu na tarehe ya kusikiliza tena..jamani we Acha tu!

kamaliza anaendelea tena kuchat
kama wamerogwa
 
Ulikuwa na nafasi nzuri ya kumpiga picha kama ushahidi

Hapa kwenye thread yako bila uthibitisho wa picha uliyo yasema ni changamsha genge
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom