Daktari afukuzwa kazi kwa kumfanyia upasuaji mgonjwa ‘guest’

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
3,385
2,000
Madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro wamewafukuza kazi daktari na muuguzi wa hospitali ya wilaya hiyo kwa tumuma za kumtoa mgonjwa wodini na kumpeleka nyumba ya kulala wageni na kumfanyia ya upasuaji wa tezi dume.

Wakizungumza leo Jumanne 9 katika baraza kikao cha baraza la bajeti ya Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2021/2022, madiwani hao walifikia uamuzi huo baada ya kamati ya maadili kukaa na kuona wanastahili adhabu .

Mwenyekiti wa baraza la Madiwani, Yusto Mapande, amesema, daktari huyo aliyefukuzwa (jina linahifadhiwa) hayuupo katika kitengo cha upasuaji na kwamba alimrubuni mgonjwa huyo na kwenda kumfanyia upasuaji katika nyumba ya kulala wa geni iliyopo wilayani humo kwa garama za Sh50,000.

Amesema daktari huyo alishirikiana na muuguzi wa kitengo cha usingizi (jina linahifadhiwa) ambaye anadaiwa kuiba dawa za usingizi bila ridhaa ya mkuu wa idara na kwenda kumpa mgonjwa huyo.

Amesema daktari huyo alikuwa anatumikia adhabu ya kukatwa mishahara wa asilima 15 kwa miaka mitatu kwa makosa mbalimbali ya kinidhamu na ndiyo alikuwa na mwaka mmoja tangu kuanza adhabu hiyo.

Mkukurugenzi Mtendaji wa halmashauri halmashauri ya Same , Anastazia Tutuba amesema ndugu wa mgonjwa walifika ofisini kwake kulalamika, kuwa ndugu yao alitolewa wodini na kwenda kufanyiwa upasuaji katika chumba cha kulala wageni.

"Baada ya taarifa hizo nililipeleka kwenye kamati ya maadili kwa ajili ya uchunguzi, na baadaye kamati ilibaini ni kweli daktari na muuguzi huyo walimfanyia upasuaji mgonjwa huyo," amesema Tutuba.

Chanzo: MWANANCHI
 

mmteule

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
3,682
2,000
Madiwani wanapata wapi jeuri ya kunifukuza kazi daktari, kweli siasa imekuwa popobawa!
Madiwani hawajamvua taaluma ya Udaktari, bali wamesitisha Ajira yake kwa Mujibu wa Sheria za Serikali za Mitaa. Tujiffunze kusoma sheria na miongozo mbalimbali ili tusiwe vipofu wa maongezi/mijadala. Diwani awe la 7, 8, Vidudu nk ndio ashapewa nguvu kisheria huna budi kuendana na taratibu zilizowekwa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom