Daktari abaka mtoto wa ofisa usalama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Daktari abaka mtoto wa ofisa usalama

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Saint Ivuga, Nov 7, 2010.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Nov 7, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,315
  Likes Received: 19,478
  Trophy Points: 280
  Daktari abaka mtoto wa ofisa usalama


  na Christopher Nyenyembe, Mbeya


  [​IMG]
  DAKTARI wa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya, Haruna Nyagoli, anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani hapa, kwa kosa la kumbaka mtoto wa kike ambaye baba yake ni Ofisa Usalama wa Taifa wa Wilaya ya Mbeya.
  Binti huyo, ambaye jina tunalo, alipatwa na mkasa huo baada ya kutishiwa silaha, kabla ya kumuingilia kinguvu.
  Habari ambazo Tanzania Daima imezipata na kuzifanyia uchunguzi wa kina zinaonyesha kuwa tukio hilo lilitokea Novemba 3 umbali wa kilometa zipatazo 30 kutoka katikati ya Jiji la Mbeya, baada ya daktari huyo kutumia nguvu na kumteka binti huyo anayetarajiwa kuanza masomo katika Chuo Kikuu cha Tumaini.
  Habari ambazo zimethibitishwa na baba yake mzazi (DSO) wa Wilaya ya Mbeya, alikiri kutokea kwa tukio hilo na kutaka sheria ichukue mkondo wake.
  Tanzania Daima ilipofuatilia kwa undani tukio hilo ilibaini kuwa lilitokea Novemba 3, majira ya saa 9 alasiri katika hoteli moja inayomilikiwa na Kanisa la Uinjilisti la Mbalizi (MEC), ambako huko kuna hosteli na kwamba kwa ushawishi alimshawishi binti huyo kwa kumpa lifiti, lakini alikijuta akipelekwa nje ya mji.
  Mashuhuda wa tukio hilo na habari za uhakika ambazo Tanzania Daima imezipata kutoka ndani ya Jeshi la Polisi zinadai kuwa daktari huyo baadaye kumfikisha binti huyo kwenye hoteli hiyo, alimlazimisha kufanya naye mapenzi kwa kutumia bastola yake yenye namba za usajili MD/IR/9571/2010, kisha alifanikiwa kutimiza azima yake.
  Mganga Mkuu wa Hosiptali ya Mkoa wa Mbeya, Haruon Machibya, alipohojiwa akiri kuwapo daktari huyo katika hospitali yake na kudai hivi sasa yuko safarini mkoani Morogoro.
  “Hivi sasa nipo Morogoro, ni kweli Dk. Nyagoli tunaye katika hospitali ya mkoa lakini sina taarifa za tukio lolote linalomhusu, nitafuatilia ili kuweza kujua ni kitu gani kimetokea huko,” alisema Dk. Machibya.
  Baba mzazi wa binti huyo ambaye ni Ofisa Usalama wa Wilaya ya Mbeya, alipohojiwa alikiri kutokea kwa tukio hilo na kuomba sheria ichukue mkondo wake na kwamba hawezi kuliongelea kwa kina suala hilo akihofia litamchanganya binti yake. “Tukio hili limetokea, tupo kwenye vyombo vya dola, naomba tuiachie sheria ichukue mkondo wake, sipendi jambo hili tuliingize kwenye vyombo vya habari linaweza kumchanganya zaidi binti yangu,” alisema ofisa huyo na kuthibitishiwa na Tanzania Daima kuwa haitatumia majina yao. Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Advocate Nyombi, alipotafutwa kuelezea tukio hilo, simu yake haikuweza kupatikana kutokana na kuita bila kupokewa.


  chanzo:Tanzania daima
   
 2. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #2
  Nov 7, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Duh.
  Ni kweli kambaka au huyo afisa usalama alistukia uhusiano akaamua kumuuzia kesi jamaa????
  wanafahamiana vipi na binti mpaka ampe lift??
  daktari kutumia bastola kumbaka binti wakati anauwezo wa kumlalia mgonjwa wake baada ya kumuoverdose?? binti aliisomaje namba ya bastola ktk state of fear in kubakwa?
  binti amepimwa na daktari akakutwa kaingiliwa???
  mtuhumiwa alikamatwa kwenye tukio au baada ya kubaka akaamua kujipeleka polisi???
  walakini walakini walakini walakini
   
 3. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #3
  Nov 7, 2010
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Nasikia harufu ya ubambikaji!
   
 4. K

  Kahinda JF-Expert Member

  #4
  Nov 7, 2010
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 849
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 60
  Mkuu
  Kweli hii bado imekaa kinamna yake, je mtoto huyo alitekwa?,mbona inasemekana tendo hilo lilifanyika kwenye hostel iliyoko Mbalizi kilometa kadhaa toka Mbeya mjini? aliingizwaje chumbani kwani nina imani kuwa lazima tararibu zote za kupata chumba hapo zilifuatwa?. Alipiga kelele wakati gani kuomba msaada?.

  Kwa vile tumezoez watu kutumia nyadhifa zao kubambikiza kesi kwa watu hasa kunapokuwa na uhasama fulani hata mimi naitilia mashaka kesi hii.
  Walio na taarifa zaidi watujulishe, lakini hadi sasa nina wasiwasi kuwa hii kesi inaweza ikawa ya kubambikiziwa kwa misingi kwamba aidha dktari huyo alikuwa na mapenzi ya muda mrefu na binti huyo baba mtu alipoinusa akaweka mtego wa kumnasa na kisha asingiziwe kuwa amembaka. Kwani binti ambaye ana tarajiwa kwenda chuo kikuu huyo ni mtu mzima aliye na maamuzi ya binafsi.
   
 5. C

  Crooked I Member

  #5
  Nov 8, 2010
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii kesi ni ya kupika OForensic haionyeshi kabisa kama kuna ishara ya ubakaji...M/Mungu amewajaalia wanawake nguvu nyingi za kumshinda hata simba anapokuwa kwenye hatari....iweje mtu atolewe umbali mrefu ivyo pasipo kujaribu kujiokoa?then wakafika mpaka kwenye hostel ambapo chumba kililipiwa...hapo binti bado alikuwa kaonyeshewa bastola?na taarifa zilipatikanaje kuhusu tendo hili?vithibitsho vya kubakwa viko vingi na vyote vinatakiwa viwe vinaoana na sio vya kutengeza...medical examination na investigations ni vipimo vya kati kabla ya treatment...haijulikani uyo binti amethibitishwaje kubakwa na kama amepewa treatment yoyote na ni ipi?a bit of science.
  Mzazi hakukubaliana na mahusiano ya wawili hawa,my conclusion!!
   
 6. B

  Bi. Mkora JF-Expert Member

  #6
  Nov 8, 2010
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 375
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Story yenyewe kidogo haijakaa vizuri. Umesema alimteka, hapohapo ukasema alimpa lift. Na alipofika hotelini ni kwamba alishuka akiwa at the gun point? Kulikuwa hakuna watu? Yeye baba alijuaje binti yake kabakwa? Huyo binti alikubali vipi kupanda gari ya mtu ambaye hamfahamu?
   
 7. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #7
  Nov 8, 2010
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ....kweli. walakini, walakini na walakini. uwezekano mkubwa ni kuwa huyu Dingi aliishamkanya Dokta kuhusu kumlalia Binti yake lakini inawezekana Binti ndio alikuwa haoni hasikii mbele ya mtarimbo wa dakitari! Kilichofuata ni huyu Mdingi kutumia wadhifa wake serikalini kumfanyizia jamaa. Haya ndio matumizi mabaya ya madaraka tuliyodhamiria kuyaondoa na Dr Slaa (samahanini kwa mtakao udhika).
   
Loading...