Dakika za lala salama, Mwana mabadiliko umejipanga vipi?

Attachments

  • 1445620390414.jpg
    1445620390414.jpg
    21.4 KB · Views: 96
Mm mshua wangu ni ccm. Naona anaingia chumbani kwangu nakutoka alaf nakuta vitu vimeparanganyika mara droo zimefunguliwa na hanaga hzo. NAona anatafuta kichinjio changu atokomee nacho mana kanishindwa kijana nataka #mabadiliko na kichinjio natembea nacho. Ushauri tunzeni saaana hvyo vichinjio vyenu muda wa lala salama usiamini mtu.

Hahahahahahahahahah

Mkuu BansenBurner Umenivunja mbavu.
Siyo Mchezo yaani. Mshua anataka upoteze kura yako.
Hiyo akili nzuri sana ya kutembea nacho mfukoni.
 
Habari zenu wakuu?

Ni muda umepita sasa tokea purukushani za kampeni zianze mnamo mwezi Agosti mwaka huu.
Mengi tumesikia,mengi tumeona na mengi yametokea.

Hapa tulipofikia sasa ni dakika za lala salama.
Nawauliza nyie mnaojiita wanamabadiliko mmejipanga vipi?

Binafsi pamoja na umasikini wangu hivi ninavyoandika hapa nimesafirisha jamaa zangu wawili kutoka mikoani huko warudi huku Dar walikojiandikishia.

Wengi tunataka mabadiliko,lakini tujiulize tunashiriki vipi kwenye kuyaleta hayo mabadiliko?
Nitamshangaa sana yule ambaye ushiriki wake kwenye mabadiliko ni kupiga kelele huku JF na kwenye mitandao mingine ya kijamii au vijiweni.

Wakati huu tuliofikia sasa sio wa kuangalia/kujadili porojo za nani kasema nini bali kuunda mikakati mizito ya ushindi.
Kila mmoja ajiulize hapo nyumbani unapoishi wote wapo kwenye maeneo/karibu na walipojiandikishia?

Kama kuna ndugu yako kajiandikishia kijijini arudi alikojiandikishia n.k

Tukumbuke kuna wengine hawana hata shida ya nauli,hawa tuwape elimu na hamasa ya kwenda kupiga kura.
KURA YAKO PEKEE HAITOSHI KULETA MABADILIKO.

Mimi nimejitahidi kuwatafutia kazi flan ya tempo wanaCCM wanne wasiwepo maeneo ya kuipigia kura siku ya kura, nimeficha kadi ya kura ya king'ang'anizi mmoja wa CCM..., so nimehakikisha kura tano za CCM hazipo
 
Mimi nimejitahidi kuwatafutia kazi flan ya tempo wanaCCM wanne wasiwepo maeneo ya kuipigia kura siku ya kura, nimeficha kadi ya kura ya king'ang'anizi mmoja wa CCM..., so nimehakikisha kura tano za CCM hazipo

Hahahahahaaa mkuu nimecheka sana.
Hii mbinu yako nimeipenda.
ZUIA KURA YA GAMBA,WEZESHA YA MWANA MABADILIKO.
 
Kuanzia tarehe 28 utarudi kwenye jukwaa lako la kina Ali Kiba na Diamond baada ya bakora za CCM.

Hahahahaaa na utasubiri sana,nimehamia huku mazima na hakuna cha kunitoa maana wakati huo nitakuwa nasherehekea ushindi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom