Dakika za lala salama, Mwana mabadiliko umejipanga vipi?

Nifah

JF-Expert Member
Feb 12, 2014
31,492
65,103
Habari zenu wakuu?

Ni muda umepita sasa tokea purukushani za kampeni zianze mnamo mwezi Agosti mwaka huu.
Mengi tumesikia,mengi tumeona na mengi yametokea.

Hapa tulipofikia sasa ni dakika za lala salama.
Nawauliza nyie mnaojiita wanamabadiliko mmejipanga vipi?

Binafsi pamoja na umasikini wangu hivi ninavyoandika hapa nimesafirisha jamaa zangu wawili kutoka mikoani huko warudi huku Dar walikojiandikishia.

Wengi tunataka mabadiliko,lakini tujiulize tunashiriki vipi kwenye kuyaleta hayo mabadiliko?
Nitamshangaa sana yule ambaye ushiriki wake kwenye mabadiliko ni kupiga kelele huku JF na kwenye mitandao mingine ya kijamii au vijiweni.

Wakati huu tuliofikia sasa sio wa kuangalia/kujadili porojo za nani kasema nini bali kuunda mikakati mizito ya ushindi.
Kila mmoja ajiulize hapo nyumbani unapoishi wote wapo kwenye maeneo/karibu na walipojiandikishia?

Kama kuna ndugu yako kajiandikishia kijijini arudi alikojiandikishia n.k

Tukumbuke kuna wengine hawana hata shida ya nauli,hawa tuwape elimu na hamasa ya kwenda kupiga kura.
KURA YAKO PEKEE HAITOSHI KULETA MABADILIKO.
 
Mi kuna jamaa yangu yupo Mtwara anataka kuja R ila hana nauli nimkopeshe ila nimemtosa bz ni linyinyiemu, akae huko huko nitamtumia jpili jioni.

Hilo popoma ni la kulipotezea bro,tafuta jamaa yeyote mwanamabadiliko umpe.
Hakikisha hiyo nauli haikosi mtu.
 
Unatakiwa kutusisitizia pia tupime sera za kila mgombea kabla ya kufanya maamuzi sahihi.Kama unadhani mabadiliko ni kubadilisha chama pole sana maana ushindani mkubwa mwaka huu ni baina ya CCM Original (DR. MAGUFULI) na CCM B (CHADEMA - LOWASA).Mgombea wa Chadema amekulia na kulelewa na CCM na alishakuwa mtendaji mkubwa.Ukilitambua hilo pima sera zaidi za viongozi wanaogombea kwa maana mara baada ya uchaguzi kuna miaka mitano ndio tena tupige kura.Miaka mitano inatosha kabisa kutumaliza kwa kupoteza rasilimali zetu kama tutapata kiongozi goigoi.
 
Kama kuna mtu ambaye hajafanya maamuzi mpaka sasa kuwa kura yake atampigia nani huyo sijui nimuweke kwenye kundi gani.
Hapa nipo kwa ajili ya kusisitiza wenzangu kufanya mikakati mizito ya ushindi.
Sio vibaya na wewe ukianzisha uzi wako kuwasisitiza wenzio wafanye maamuzi sahihi.
 
Mkuu kwa upande wangu chama kilinipa jukumu la kuratibu mawakala, zoezi limeenda vizuri kabisa na mimi ni miongoni mwa mawakala, naahidi kukitendea haki chama changu.

Sasa wewe ndio utabeba lawama endapo utaratibu mawakala wasio na misimamo ambao wataweza kulaghaiwa wakasababisha goli la mkono.
Hakikisha unawapanga vijana wako vyema,ushindi ni lazima.
 
Kama kuna mtu ambaye hajafanya maamuzi mpaka sasa kuwa kura yake atampigia nani huyo sijui nimuweke kwenye kundi gani.
Hapa nipo kwa ajili ya kusisitiza wenzangu kufanya mikakati mizito ya ushindi.
Sio vibaya na wewe ukianzisha uzi wako kuwasisitiza wenzio wafanye maamuzi sahihi.

Mimi binafsi kura yangu ni kwa DR. MAGUFULI na hakuna wa kunibadilisha kwa kuwa nina sababu nyingi sana kwa nini nampa kura yangu jamaa huyu.Baadhi ni hizi zifuatazo:

1. Ni muadilifu na mchapa kazi.
2. Naamini Magufuli atawawajibisha watendaji wa serikali wazembe.
3. Mabadiliko hayawezi kuletwa na Chadema maana wamekuwa vigeugeu mwaka huu, maana yule walituaminisha kuwa ni fisadi papa leo wanasema anatufaa, sikuwa na option zaidi ya kumuamini DR. MAGUFULI.
4. Kwenye kampeni za chadema kwa sasa sijasikia wakitoa mikakati ya kuwashughulikia mafisadi kama ilivyokuwa zamani zaidi ya kung'ang'ania mabadiliko.

Zingatia: Kampeni zinaisha jumamosi, siku zilizosalia maamuzi yanaweza yakafanywa na ndio maana kila mgombea amejikita kwenye eneo ambalo linaweza kuleta kura za kutosha.
 
Sasa wewe ndio utabeba lawama endapo utaratibu mawakala wasio na misimamo ambao wataweza kulaghaiwa wakasababisha goli la mkono.
Hakikisha unawapanga vijana wako vyema,ushindi ni lazima.

Yap mkuu, nimejipanga vyema hakuna shida
 
Unatakiwa kutusisitizia pia tupime sera za kila mgombea kabla ya kufanya maamuzi sahihi.Kama unadhani mabadiliko ni kubadilisha chama pole sana maana ushindani mkubwa mwaka huu ni baina ya CCM Original (DR. MAGUFULI) na CCM B (CHADEMA - LOWASA).Mgombea wa Chadema amekulia na kulelewa na CCM na alishakuwa mtendaji mkubwa.Ukilitambua hilo pima sera zaidi za viongozi wanaogombea kwa maana mara baada ya uchaguzi kuna miaka mitano ndio tena tupige kura.Miaka mitano inatosha kabisa kutumaliza kwa kupoteza rasilimali zetu kama tutapata kiongozi goigoi.

Kweli NCHI hii kuna watu waajabu sana yaani mpaka leo hujajua mwenye SERA zinazofaa watu km nyie ndio mtaji wa CCM
 
Kamanda nifah Pamoja sana ktk kutafutaa KURA za mabadiliko kwanza mimi ni WAKALA kwenye KATA yangu Semina tulizopata zimetujengea uwezo wakutoruhu GOLI la MKONO iwe MVUA au JUWA tunataka kufikia saa4 Asubuhi CCM itakuwa chama cha Upinzani kwa lengo lakupunguza KURA za CCM...MKE wangu ni GAMBA sasa nimepanga kuficha kikatio chake na kwakua nitakuwa nahesabua KURA home nitarudi usiku Kikatio chake atakutana nacho usiku mwingi hii ndio DAWA ya watu wanaochelewa kuelewa madhara ya hili JOKA linaloitwa CCM
 
Last edited by a moderator:
Unatakiwa kutusisitizia pia tupime sera za kila mgombea kabla ya kufanya maamuzi sahihi.Kama unadhani mabadiliko ni kubadilisha chama pole sana maana ushindani mkubwa mwaka huu ni baina ya CCM Original (DR. MAGUFULI) na CCM B (CHADEMA - LOWASA).Mgombea wa Chadema amekulia na kulelewa na CCM na alishakuwa mtendaji mkubwa.Ukilitambua hilo pima sera zaidi za viongozi wanaogombea kwa maana mara baada ya uchaguzi kuna miaka mitano ndio tena tupige kura.Miaka mitano inatosha kabisa kutumaliza kwa kupoteza rasilimali zetu kama tutapata kiongozi goigoi.

Mwaka huu tuna option moja tu ya kuchagua, nayo ni Edward Lowassa.
Hao wengine ni sawa na kupoteza kura.
 
Nyumbani kwangu kuna kura 8 za Rais Lowasa, Mbunge Mnyika na Diwani Kolimba.

Hatutaenda kanisani siku hiyo na tutakuwa wa kwanza kufika kituoni.

Nimetoa usafiri kwa majirani ambao wanaenda kumpigia kura Lowasa.

Majina yao nimeyakusanya, yanakaribia 30 nawaletea coaster kabisa. Wasipotosha nawapakia kwenye pick up.

Na uzuri pembeni ya kituo kuna bar kama mita 40 hivi, tutakuwa tunaangalia mechi ya Man Utd vs Man City huku macho yapo kituoni.

Bili ya walinda kura nitalipa mimi.
 
Mimi nimetoka kijijini nilikokuwa nimeenda kuja kuhakiki jina langu na nimeliona. Nimeongea na wadogo zangu namna ya kuwapigia kura majirani ambao hawana uelewa wa kupiga kura wakawasaidie kupiga kura kule kwenyewe...........
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom