Dakika tano na Rais John Pombe Joseph Magufuli

Cesar Saint

JF-Expert Member
Nov 18, 2016
263
500
Wasalaam,
Awali ya yote ningependa kutanguliza salamu kwako Mheshimiwa Raisi na kukutakia heri ya mwaka mpya 2020.

Mheshimiwa Raisi siwezi kusema nafahamu ugumu wa dhamana uliyobeba kutuongoza Watanzania tukiwa kama taifa lenye mchanganyiko wa mamilioni ya watu wenye mtazamo na malengo mbalimbali kimaisha na kitaifa kwa ujumla hivyo Mwenyezi Mungu azidi kukutia nguvu na kukuwezesha katika yote uyafanyayo.

Kwa dakika hizi chache naomba kusema haya machache yafuatayo;

Mosi:
Napenda kutambua juhudi zako za kufanya mageuzi katika sekta ya miundombinu na utawala na kila mara umekuwa ukisema unawaza siku ukiondoka itakuwaje!? Napenda nikwambie nafasi ya kutengeneza mfumo huru wa kujenga na kusimamia zaidi ya hapa ulipofika ni sasa.Huu ndio wakati wa kujenga mfumo wa Serikali inayoweza kujisamia na kujikosoa pale inapolazimika kufanya hivyo,Huu ndio wakati wa kuimarisha uongozi unaojali watu na taifa kwa ujumla.Kuna deni la Katiba na kuondoka katika mfumo wa Serikali ya mazoea Mheshimiwa Raisi Nafasi hii unayo sasa .

Pili:
Mheshimiwa Raisi Huruma ya Serikali kwa watu wake iko wapi? Mpaka wakati huu naandika haya kuna mambo mengi ambayo ni “Pending Issues” na Serikali kama Mama wa taifa haijaonyesha huruma yake .Utawala bora ni pamoja na “Leadership Empathy”kuna mambo ambayo Serikali ni vizuri ikifanya kusudi kugusa mioyo ya watu wake vinginevyo hutengeneza chuki na kupoteza tunda la uzalendo kwa watu wake.

Mheshimiwa kuna watu mpaka leo hii hawana makazi baada ya tetemeko la Kagera. Kuna kundi la watu mpaka leo hii wameondolewa kazini kimakosa wakati wa operation ya kutoa wafanyakazi hewa na hawajarudi makazini mpaka sasa huku wakipoteza stahiki zao katika mashirika na mifuko ya hifadhi ya jamii fedha ambayo walikatwa kipindi chote wakiwa wafanyakazi wa Serikali ya nchi yao na ghafla mfumo mzima wa maisha yao umevurugika.

Kuna wastaafu mpaka leo hawajalipwa malipo stahiki na mambo mengine kadha wa kadha ambayo Serikali inapaswa kuangalia kwa jicho la upekee kwani yanagusa kundi kubwa la watanzania.

Tatu:
Mheshimiwa Raisi Serikali yetu mbona imetusahau vijana!? Hapa si katika nafasi za uongozi La hasha! Naongelea sera za maendeleo ya vijana,Ajira na uwezeshaji.Mheshimiwa kuna kundi kubwa la vijana wasomi wasio na ajira wala hawana mazingira ya kuwawezesha kujiajiri hii inapelekea hata kushindwa kulipa mikopo yao ya elimu ya juu (hivi Serikali kupitia wizara ya vijana/ajira inashindwa kuanzisha mfuko wa kutoa mikopo(grants) za vijana wenye mawazo yatakayojenga uchumi wa taifa hili na kuwawezesha kujiajiri) Pia kuna kundi hili jingine lilijiajiri katika sekta zisizo rasmi Mheshimiwa kodi na matozo(ushuru)unatuumiza sana kwani hauakisi uhalisia wa biashara zetu na uchumi.

Nne:
Mheshimiwa Raisi sisi watanzania wa hali ya chini tunaona juhudi zako katika kuleta maendeleo katika sekta mbalimbali (ujenzi wa miundombinu,manunuzi ya ndege na mengineyo) Lakini niwasilishe kwako ombi moja tafadhali,Ni wakati wa kuanza kushughulikia maswala yanayogusa maisha yetu sisi watanzania wa chini moja kwa moja kuanzia kwenye Afya(upatikanaji wa vifaa tiba na dawa kuanzia hospitali za kata) Elimu(kuboresha miundombinu na maslahi ya walimu) Nishati (Mheshimiwa gharama za mkaa,mafuta na gesi ziko juu sana Serikali itufikirie)Huduma nyingine za kijamii kumekuwa na ongezeko kubwa la watu mijini huduma ya masoko,takataka,usafi wa miji,maji safi,usafirishaji(miundombinu ya barabarani) Mifumuko ya bei za mazao ya vyakula,uboreshwaji wa zana za kilimo na pembejeo Hebu weka nguvu na hapo.

Tano:
Mheshimiwa Raisi Hali ya usalama na uongozi nchini inahitaji kisemewa neno! Serikali inawajibu wa kukemea,kusemea na kutoa mwongozo kwa matukio mbalimbali yanayochafua taswira ya nchi yetu na si kukaa kimya kuacha upepo upite.Ni vizuri Serikali ikijipambanua msimamo wake na kuondoa maswali kwenye maswali yanayochukua “Public Attention” Wananchi tunaimani na Serikali yetu hivyo tungependa kuona ikiwajibika kutoa maelezo,kujibu na kujipambanua pale inapobidi kufanya hivyo .kwa mfano nafasi ya Serikali kwa Ndugu Azory ni ipi!?

Mwisho Mheshimiwa Raisi naomba nikuachie Swali ambalo jibu lake litaishi miaka mingi zaidi hata pale ambapo mimi au wewe tukiondoka juu ya uso wa dunia.

Mheshimiwa Raisi John Pombe Joseph Magufuli unaacha legacy gani itakayoishi na kukumbukwa pale utakapomaliza uongozi wako?

Asante .
 
Zambotti

JF-Expert Member
Jul 2, 2016
1,545
2,000
Na wanaimla wengi huwa wanatuona watu wengine vichwa maji.

Eti siku akiondoka itakuaje, kwani alitukuta wapi mzee
 
Mag3

JF-Expert Member
May 31, 2008
11,023

Maguful.jpg
Maguful.jpg
 
Top Bottom