Dakika 45 ITV na Profesa Ndalichako: Hakuna jiwe litakalobaki bila kugeuzwa

Ki Mun

JF-Expert Member
Oct 6, 2014
3,443
4,386
IMG_20160613_214812.JPG

Prof. Ndalichako atakuwa ndiye mgeni mwalikwa leo kwenye kipindi cha dk.45 ITV, saa 3 usiku.

Stay tuned!

----------- Updates ------------

Waziri Wa Elimu Mh. Joyce Ndalichako asema hakuna aliyesababisha uzembe wowote katika kuwadahili wanafunzi wasio na sifa pale UDOM atakayeachwa asema "Hakuna jiwe litakalobaki bila kugeuzwa "

Chanzo: ITV
 
Ukijiingiza kwenye siasa Tz utachafuka tu... Huyu mama Ndalichako alijijengea heshima kubwa alivyokuwa mtumishi wa kawaida mpaka wadau wakampigia chepuo kuwa waziri..

Yawezekana hata tunachompinga au kumkosoa hapa sio kwa utashi au makosa yake ila yeye anabeba tu zigo alilobebeshwa na boss wake..

Hii imemtokea Prof Tibaijuka ambaye pia alijijengea heshima kubwa tu kule UN
 
Hatutaki maneno masikio yetu tiyari yameshiba, macho ndiyo tumeyakodoa tuone hayo mawe yaliyo ibuliwa pale UDOM ka atathubutu kuyapindua.
Chonde mwanetu, usijegusa mboniiii huku ukasahau kuwa umeteuliwa tu
 
Namsikiliza profesa Ndalichako ITV, yaani huyu mama amekomaa sana kuliko alivyokuwa nacte, anajieleza kwa ufasaha na anaongea point kwa point kweli anahaki ya kuitwa Profesa Ndalichako.
 
swali la watoto wa vigogo amelikwepa kabsaaaaaaa lakini pia mzigo wa uwajibikaji umetwishwa kwa wanafunzi ilihali akikiri wazi kwamba hawakua na makosa hasa lile lililosemwa kwamba ati waligoma
 
Kama kweli profesa anyoyasema juu ya st.joseph basi profesa mgaya anapaswa kupandishwa kizimbani, haiwezekani umdahili form four asome digirii tena na mkopo juu halafu aachwe tu huru uraiani hapana kabisa.
 
Ukijiingiza kwenye siasa Tz utachafuka tu... Huyu mama Ndalichako alijijengea heshima kubwa alivyokuwa mtumishi wa kawaida mpaka wadau wakampigia chepuo kuwa waziri..

Yawezekana hata tunachompinga au kumkosoa hapa sio kwa utashi au makosa yake ila yeye anabeba tu zigo alilobebeshwa na boss wake..

Hii imemtokea Prof Tibaijuka ambaye pia alijijengea heshima kubwa tu kule UN

acha unafiki ww, kilakitu nyie lawama tu na kulalamika utadhani d*m
 
Namsikiliza profesa Ndalichako ITV, yaani huyu mama amekomaa sana kuliko alivyokuwa nacte, anajieleza kwa ufasaha na anaongea point kwa point kweli anahaki ya kuitwa Profesa Ndalichako.
acha uongo hajui kujieleza anazunguka zunguka tu kuna maswali anapotezea
 
Kama hakuna aliyegoma ,mbona mweshimiwa alisema walianza migomomigomo?nani tumwamini
 
Back
Top Bottom