Daima na milele, Taifa la kulindana haliwezi kuendelea.

Mchokoo

JF-Expert Member
Jul 28, 2015
1,179
1,579
Ukistajabia umaskini wa Tanzania utauona wa DRC Congo!

Haiwezekani sisi kama taifa tuwe wakali kwa wale wanaoisababishia serikali hasara ya pesa kiduchu wakati wale waliolisababishia taifa umasikini wa kutupwa kupitia mikataba ya kinyonyaji na kifisadi tukiendelea kuwahakikishia ulinzi kwa mujibu wa katiba tuliyonayo!
Sio bure huenda ni kweli aliyeturoga kafa!

Nataka kuwahakikishia watanzania wenzangu kwamba; iwapo hatutastuka mapema kuiondoa kinga ya kutoshtakiwa kwa marais wastaafu, kuhusiana na makosa waliyoyafanya wakati wakiwa madarakani, basi, ni heri tukaitangazia dunia rasmi kwamba; sisi na umaskini, tumekuwa mume na mke, hivyo kama wanandoa; na tuzae watoto wetu mafukara tena wenye maradhi, mpaka kifo kitakapotutenga!

Katika uongozi wa nchi hii ukimuondoa baba wa taifa mwalimu Nyerere ambaye hakuitumia kinga hii ya kikatiba vibaya, je ni yupi kati ya marais wastaafu ambaye hana kosa katika haya masuala ya mikataba mibovu iliyoingiwa kwa msukumo wa maslahi binafsi?
Ni vizuri tukajiuliza swali hili tunduizi.

Iwapo kwa sasa tumesha kuwa na marais watano tangia uhuru, ambapo wote hao wana kinga ya kutoshtakiwa ilihali katika hao tu tayari tumeshuhudia majanga mengi ya kimikataba tena kifisadi.
Sasa sijui itakuwa vipi nchi hii ikifikisha idadi ya marais wastaafu 10 au tuseme 46 kama USA. Na wote hao wawe na kinga ya kutoshtakiwa!
Hukumuni ninyi wenyewe!

Si watakuwa wamegawana kila mtu mkataba wake tena kwa maslahi yake.
Mfano.

AHM-- Loliondo
Bwm -- madini
Jku --- gesi.
Smw-- mlima Kilimanjaro.
Mzt-- Mbuga ya Serengeti
FAM-- mbuga ya Mikumi

Na kadharika na kadharika

Swali.
Sasa basi, iwapo bado tutaendelea na hali hii ya kurindana tena kikatiba.
Kwa nini sasa tusione sababu ya kuoana kabisa na umasikini kuliko kuendelea kuziniana nao kwa kuiba?
 
Back
Top Bottom