Elections 2010 Daily News: Slaa will not be the fifth president of Tanzania!

It is high time that section of the media learnt its lessons and returned to professional practice. We think there is nothing particularly wrong in covering presidential aspirants favourably, but the reports must at least be true. And the truth is that Dr. Willibrod Slaa will not be the fifth president of Tanzania.


Source: Dailynews Online[/QUOTE]

This Daily News Editorial has me full of rage!
They have stooped so low. And they have the audacity of telling others 'to return to professional practice' while they have proved to be very unprofessional.
It seems that when poll was conducted, the results were apparently not to Daily News' and their masters' liking. They stopped it but the results were out.

And the most dangerous thing they wrote is that 'And the truth is that Dr. Willbrod Slaa will not be the fifth president of Tanzania'.

The big question is that have the Daily News got information of who will be declared the winner of the presidential position regardless of the wish of the people according to the ballot count?

The National Electoral Commission should make a firm stand on this and sanction the Daily News. Strong action should be taken against them.

I call upon lawyers such as Professor Issa Shivji, Mabere Marando, Tundu Lissu as well as human rights advocates to open a court case against the Daily News, its Managing Editor, its publishers and its printers.

Fellow Tanzanians, MAKE SURE YOU VOTE ON 31st OCTOBER!

2010 Watanzania hatudanganyiki!
 
Naona hawa daily newz wamelewa maana hawajui kwamba wao kazi yao ni kutujulisha habari kwa jinsi zinavyotokea bila kujali inamuhusu nani? Baada ya kuona bwana mkubwa anagaragazwa wao wameamua kukana maoni waliyokuwa wanayakusanya na kwa lengo la kumplizi bwana mkubwa wameamua kujiunga na shehe Yahaya kwa kumtaja mshindi kabla hata Tume ya Uchaguzi kufanya kazi yake. Mi niwaambia kuwa km wao wanafaidika kwa namna yoyote ile, basi wanapaswa kuwakumbuka watu wa Nyamongo ambao wao ni wahanga wa serikali mbovu tuliyonayo, watu wa Kipawa ambao leo hii wengine hata hawajui watalala wapi? vijana wamachinga ambao wanataman mwaka mzima uwe wa kampen angalau na wao wapumzike kufukuzana na polisi, binti zetu ambao kutokana na sababu moja au nyingine wamejikuta wajawazito na bwana mkubwa akasema wanajitakia, wazee wa East Africa ambao walidhalilishwa pale surrender na wengine wengi kama hao ambao tunasubiri muda ufike tukaonyeshe kwa vitendo tumechoshwa na sasa tunataka mabadiliko. Hatutaenda kuchagua viongozi bali tutakwenda kubadilisha viongozi! CCM mwaka huu ushindi si lazima!!!!!
 
Mimi nasema sisiem na vyombo vyake vinafanya mzaha, na mwisho wake watatusababisha wengine tulio na UWEZO WETU wa kuwashughulikia kwa njia MBADALA tukafukue tulivyo vihifadhi natuwa wajibishe, enough is enough ! kama ustaarabu hauwezekani basi hatutatumia vurugu wala kumwaga damu za wasio na hatia, ila wao madarkani hawata kaa, wao siyo miungu na wala sio buleti prufu.
 
Nafikiri hii tahariri ni mojawapo ya utekelezaji wa ule waraka uliokamatwa na dk slaa. Hakika watu ni watumwa katika uhuru wao
 
EDITOR,
23rd September 2010


A vividly pro-Willibrod Slaa weekly tabloid has used our name in a shameful attempt to prop up the Chadema presidential candidate’s campaign, suggesting that he was being backed by three quarters of local internet surfers.

In its lead story on Tuesday, the September 22-28 edition of the tabloid deliberately misused an online poll involving a mere 161 visitors to purport that the whole nation was behind Slaa. While noting the tabloid editors’ virtual confession that they cannot be believed without quoting the Daily News, we abhor the unprofessional decision to use our name to lend credence to their wildly hopeless adventure.

The editors of the tabloid know that the figures they used are quoted out of context and are absolutely unrealistic. That is why they confess in the fabricated report that very few Tanzanians have access to the internet and that the purported poll results do not reflect what will come out of the October 31 ballot.

So why would they venture out with old poll results today? Vicious anti-establishment fervor at best and malicious conspiracy to settle old scores at worst. That is typical activist journalism practiced by a section of the media, which has openly identified with the opposition and plays down any positive achievement of President Kikwete’s government while orchestrating purported failures, mostly made up ones.

The attempt to enlist the support of the Daily News was apparently meant to save another tabloid blushes after carrying an equally wild fabrication to the effect that Synovate had censored results of a poll showing Slaa leading president Kikwete by four points in popularity. The pollster has publicly derided the tabloid and lodged a complaint with the Media Council.

It is high time that section of the media learnt its lessons and returned to professional practice. We think there is nothing particularly wrong in covering presidential aspirants favourably, but the reports must at least be true. And the truth is that Dr. Willibrod Slaa will not be the fifth president of Tanzania.

The Chadema candidate has a lot of issues to settle, beginning at family level, from which he will need to practice leadership upwards. He will, indeed, garner some votes in October, just like Augustine Mrema in 1995, but that will be it, and the media behind the former priest can quote us on that.



Source: Dailynews Online


The TRUTH according to whom? Kwani Daily News ndio MUNGU mpaka waweze kutabiri kitakachotokea siku thelathini na saba kuanzia leo?

Acheni UCHURO!
 
Mwaka huu kwa Kweli CCM wamebanwa kisawasawa, Kinachonifurahisha ni njia ya Kisayansi ambayo CHADEMA wameitumia kuwakimbiza mchakamchaka CCM ,kiasi cha kwamba mpaka vyombo vya serikali na dola kama vile Polisi na Magezi ya serikali ,Redio na Television,Ikulu na wafanyakazi wa serikali.

Hawajajua kwamba wamevuliwa nguo naCHADEMA mbele ya wapiga kura,chochote wanachofanya sasa hivi inaonyesha wapinzani wanaonewa,kunyanyaswa na CCM na serikali kitu ambacho kinawapatiana wafuasi wengi wale wasio na vyama kwa sababu wanataka kuungana nao ili kukomesha maonezi.
CCM wamesukumwa sasa kiasi cha kwamba kila siku kazi yao ni kujitetea tuu hawana cha kuzungumza zaidi ya kubaki watoto wanolialia tuu pamoja na kuwa na vyombo vyote nilivyotaja hapo juu.

Mhariri wa daily news hakatai kwamba hawakufanya utafiti wa sample ndogo,hatuelezi kwamba hao watu 161 walitoka mikoa gani kwa sababu hata mimi niliona hiyo poll yao na nikavote japo siko Dar es Salaam
Hatuambii ni kwa nini walisimamisha hiyo poll kwa sababu ni gazeti la serikali na sio la chama.

Mahariri nadhani ameandika taarifa aliyotumiwa na Salva kutoka Ikulu mada yake ni ya hasira na wala sio ya kupinga taarifa,hawezi kupa kabisa kwamba Dr Slaa hatakuwa Raisi, hivi ni vielelezo ambavyo vinaonyesha jinsi CCM isivyotumia busara katika kujibu hoja.

Anapozungumza Tabloid sielewi anazungumzia mtandao au gazeti gani, jamani wamebanwa kibano kigumu mwaka huu mpaka kieleweke,tunaanza kukusanya akili kujiweka tayari kupambana na wezi wa kura hasa serikali na chama chake cha CCM hamtatudanganya safari hii kweli kabisa moto utawaka tuuuuuuuuuu sisi sio mandondocha aibu kwa mhariri wa Daily News .

Hivi "njia za kisayansi" ni zipi vile? Au tuchomeke buzz words ili ujinga wetu ukubalike tu?
 
Wanajamii,
Nimepata mshtuko mkubwa baada ya kuisoma hiyo tahariri.Ninadhani huyu mhariri labda anaelewa kinachoendelea kuhusu wizi wa kura ama ana matatizo ya akili apelekwe hospitali apimwe.Ni lazima wananchi wote wapenda haki na amani tuchukue hatua dhidi ya huyu mhalifu.Ninamfananisha huyu mhariri na Samwel Kivuitu aliyechakachua matokeo ya urais huko Kenya,pia naweza kumfananisha na Interahamwe wa Rwanda waliotumia vyombo vya habari na kufanya maangamizi ya kutisha huko Rwanda.Huyu mhariri si kwamba afukuzwe kazi tu hapana bali akamatwe na kufunguliwa mashtaka ya kuchochea umwagikaji wa damu nchini.
Ni wazi kama matokeo ya ushindi wa daktari Slaa yatakuwa tofauti na matarajio ya wananchi basi mhariri huyu atakuwa shahidi wa kwanza wa jinsi matokeo yalivyochakachuliwa.
Ni aibu mno kwa gazeti la serikali kuandikwa ushenzi wa namna hii.
Ni wazi mapokezi ya daktari Slaa huko Mwanza,Arusha,Musoma na Moshi yamewaacha mhariri huyu na hao wanaomtuma wameficha nyuso zao kwa aibu.Natamani siku atakayoapishwa daktari Slaa kuwa Rais basi nimtafute huyu mhariri nimuone ameficha wapi sura yake.
Hili linawezekana tu kwa sababu mwamko wa Tanzania sasa hivi baada ya Kiboko cha mafisadi kuingia uwanjani umezidi hali ilivyokuwa Kenya,Zambia,Malawi nk.
Nawasilisha.
 
Siku ya kutangazwa matokeo tutazingira ofisi za Daily News kumsaka mhariri huyo mpumbavu. Sisi tunajua kwamba watanzania wameichoka CCM na mafisadi wao, na wanataka kuwang'oa madarakani ifikapo Oktoba 31. Sasa huyu mhariri mbumbumbu anatuambia nini? Ebo!
 
Yeye anasema media wawe professional, wakati yeye mwenyewe ana declare kuwa Slaa hatakuwa rais wa Tanzania, is this professional? Who is empowerd to declare winners and losers? Daily News or NEC.

Hahaaaaaaaaaaaaaaah heeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeooohooooooooooooooooooooooooooooooooooooohahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

Jamani nakufa kwa kicheko. Kumbe ku-declare kuwa Slaa hawezi kuwa Rais ni kosa.Haaaaaaaaaaaaaaaaah.Mbona nyie mnasema kuwa Slaa ndiye atakuwa Rais.

Mimi nilishawaambia kwenye mtandao huu kuwa you guys, you are just wasting wasting your time. Slaa will never never never be the President of the United Republic of Tanzania (RRT). NEVER. Urais siyo jambo la kujifunza kuongoza.
ukishamaliza kufa kwa kicheko, fufuka uje kutuambia kuwa kikwete aliwahi kuwa rais wapi tena kabla ahajaingia kwa hila ikulu yetu? mbona yeye mwenyewe anakiri kwamba miaka mitano ilikuwa ni ya kujifunza?
tatizo ninyi mliozalowa kabla ya uhuru ndio mnaoturoga tusifikie uhuru wa kweli.
Kizazi chenu kikishamalizika nakuapia kwamba TANZANIA yenye neema inawezekana. Tanzania bila ccm ndiyo bora zaidi
 
Siku ya kutangazwa matokeo tutazingira ofisi za Daily News kumsaka mhariri huyo mpumbavu. Sisi tunajua kwamba watanzania wameichoka CCM na mafisadi wao, na wanataka kuwang'oa madarakani ifikapo Oktoba 31. Sasa huyu mhariri mbumbumbu anatuambia nini? Ebo!

Usije ukajifungia tu chumbani na kuona aibu kutoka nje wakati hayo matokeo yanatangazwa. Nakushauri ujilazimishe kutoka nje kwani ukiendelea kujifungia kwenye chumbani unaweza kupata mawazo ya kutaka kujinyonga.
 
ukishamaliza kufa kwa kicheko, fufuka uje kutuambia kuwa kikwete aliwahi kuwa rais wapi tena kabla ahajaingia kwa hila ikulu yetu? mbona yeye mwenyewe anakiri kwamba miaka mitano ilikuwa ni ya kujifunza?
tatizo ninyi mliozalowa kabla ya uhuru ndio mnaoturoga tusifikie uhuru wa kweli.
Kizazi chenu kikishamalizika nakuapia kwamba TANZANIA yenye neema inawezekana. Tanzania bila ccm ndiyo bora zaidi

Ikulu yenu? Mna hati miliki na hiyo ikulu ehh?
 
Mganyizi, Ahsante sana kwa taarifa, nimekugongea li ahsante lako!

It is a shame that the author of the below sentences is paid from my contributions to the government. I will stop reading this Newspaper forthwith until the management of the paper is changed. So partisan and so biased

ndugu yangu, vipi akibadilishiwa nafasi then ukasikia ni mkuu wa wilaya unayoishi? maana watu hupozwa kwa ukuu wa wilaya siku hizi wapo tunawaona.....
 
Chadema kulishtaki gazeti

Fredy Azzah na Exuper Kachenje

UONGOZI wa Chadema umefikia uamuzi wa kuishtaki Daily News kwenye Tume ya Uchaguzi (Nec) baada ya gazeti hilo la kila siku la serikali kuandika tahariri inayoeleza kuwa mgombea urais wa chama hicho hatashinda kwenye uchaguzi mkuu.

Katika toleo lake la Alhamisi, gazeti hilo liliandika kwenye tahariri yake likisema "na ukweli ni kwamba Dk Willibrod Slaa hatakuwa rais wa tano wa Tanzania" huku likitaka magazeti ambayo limedai yanamuunga mkono mgombea huyo kukanukuu msimamo huo.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya uongozi wa juu wa Chadema kukutana jana na kujadili kwa kina suala hilo, huku wanasheria wa chama hicho shindani wakifikiria uwezekano wa kufungua kesi mahakamani dhidi ya gazeti hilo la Kiingereza.

Mkurugenzi wa kampeni za Chadema, Profesa Mwesiga Baregu aliliambia gazeti hili jana kuwa chama hicho kimefikia uamuzi huo kwa kuwa msimamo wa gazeti hilo la serikali ni uchochezi unaoweza kusababisha umwagaji damu.

"Chama kimekutana kujadili hilo suala na kwa hivyo kwa vyovyote tutapeleka malalamiko Nec na bado mawakili wetu wanaendelea kuangalia uwezekano wa kulifikisha mahakamani," alisema Profesa.

"Katika sheria za kawaida tu ukiachilia mbali sheria hii mpya ya uchaguzi, huu ni uchochezi unaoweza kusababisha mgogoro wa umwagaji damu."

Profesa Baregu, ambaye hakusema lini watalifikisha suala hilo Nec wala muda wa kufungua kesi hiyo, alibainisha kuwa hatua hizo zitachukuliwa mapema iwezekanavyo ili waweze kupata haki yao.

"Tutafanya haraka iwezekanavyo ili tutetee haki ukizingatia kuwa ni kweli hiyo makala (tahariri) imeandikwa na gazeti la serikali inatishia amani, hasa ukizingatia kuwa huu ndiyo msimamo wa gazeti la serikali," alisema Profesa Baregu.

Kikao hicho kilichoazimia kulishughulikia suala hilo kimefanyika wakati Dk Slaa akiwa ameshatoa msimamo wake akisema: "Hii inaonyesha kuwa serikali ina mpango mchafu ndio maana wametumia gazeti la serikali. Lakini nguvu ya Dk Slaa itathibitishwa kwa kushinda uchaguzi na kwenda Ikulu. Na kwa maana hiyo siku za mhariri zinahesabika."

Dk Slaa alitoa kauli hiyo juzi kwenye mkutano wake wa hadhara mkoani Kilimanjaro ambako pia mwenyekiti Freeman Mbowe alisema: "Tunataka uchaguzi huru na wa haki."

Alisema: "Vyombo vya umma vinatakiwa kutumika kwa ajili ya umma na si CCM. Tumesikitishwa na tahariri hiyo.Tunachotaka ni mhariri achukuliwe hatua haraka kwa sababu hiyo inaonyesha mkakati wa serikali si mzuri kwa wapinzani."

Akiongea na Mwananchi juzi, makamu mwenyekiti wa Nec, Jaji Omar Makungu alisema Nec itafanyia kazi suala hilo iwapo tu Chadema italalamika kuwa imeathiriwa na kuwasilisha malalamiko hayo kwenye chombo hicho.

"Sijalisoma hilo gazeti, lakini kauli hiyo inauma... inatakiwa walioumizwa walalamike. Wakikaa kimya, sisi hatuwezi kuchukua hatua. Kamati ya maadili ipo; Chadema au Dk Slaa akilalamika, tutawaita wanaolalamikiwa," alisema Jaji Makungu akisistiza: Tupo tayari kupokea malalamiko. Tuna kamati ya maadili, wakicomplain (wakilalamika), tutajadili na kutolea uamuzi."

Wakati Chadema ikitoa tamko hilo Jukwaa la Wahariri lilikutana jana jijini Dar es Salaam kujadili suala hilo kwa kina na kueleza kuwa litatoa taarifa yake baadaye.

Mwenyekiti wa jukwaa hilo, Absalom Kibanda aliliambia gazeti hili jana akisema: "Tunalitafakari hilo na tutalifanyia kazi na kulitolea msimamo bila kuingilia uhuru wa habari na utendaji wake wa kazi kwa kuzingatia kuwa Daily News ni mwanachama wa Jukwaa letu."

Kibanda alifafanua kuwa jukwaa hilo litaangalia iwapo kuna maeneo katika tahariri hiyo yaliyoingilia masuala ya kitaaluma.
"Tutaangalia kama maoni hayo yamegusa taaluma na kwenda kinyume. Daily News ni gazeti la serikali ni mdomo wa serikali, linapotoa msimamo katika uchaguzi wa rais ambaye ndiye mhariri wake mkuu, lazima lifanyiwe kazi kwa njia iliyo bora," alisema Kibanda.

"Tunajua maadili ya kazi zipo taasisi zinazosimamia uchaguzi, Nec ndiyo yenye mamlaka ya kutangaza matokeo yoyote ya uchaguzi, katika hilo sisi tutaangalia kama imegusa matokeo ya kura za urais."

"Tunaangalia kama wameingilia matokeo ya urais. Hili ni jambo linahitaji umakini, huwezi kulikalia kimya, lakini litafanyiwa kazi na kukusudia kumuumiza yoyote," alisisitiza.

Jana Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Joel Bendera aligoma kuzungumzia suala hilo akisema: sihusiki nalo. Mimi sio msemaji wa serikali."


Chanzo: Mwananchi wa leo Jumamosi.
 
Back
Top Bottom