Elections 2010 Daily News: Slaa will not be the fifth president of Tanzania!

Huyu mhariri anaongelea Raia Mwema ambayo imeongelea JF poll. Mara ya mwishi sample ya Synovate ilikuwa watu 2,000. Wakati so far poll ya JF wamepiga kura watu 7,459. Je, na kipima joto cha ITV, nacho kinasema uwongo au sample haitoshi? Na ile ya kwao waliyoitoa, je sample haikutosha? Raia Mwema ameongelea wanamtandao na sio watanzania wote!

Na kama watumiaji wa internet ni wachache kwa nini Mama Salma anatuma tweets, CCM wana website, Ikulu wana blog, Tanzania Government ina website, Daily News wenyewe wana website?
 
I can see print media taking cues from JF. Good looking out.

I recall that at the beginning of these campaigns, you too stated, with much confidence, that CHADEMA would not win the Presidency. Are you, by any chance, working in cahoots with these people?

I note, with much concern, that The Daily News has published its astounding editorial at the same time that we hear of a CCM letter intructing all DCs to make sure that it wins. Are we witnessing a coordinated attack on our democracy?

I predict, as I have every right to, that this den of vipers will not be able to defeat the masses. The multitudes that went willingly, without any material incentives, to meet and support Dr. Slaa in Arusha and Moshi are reason enough for us to declare that he is supported by the masses.
 
EDITOR, 23rd September 2010 @ 01:55,


The Chadema candidate has a lot of issues to settle, beginning at family level, from which he will need to practice leadership upwards. He will, indeed, garner some votes in October, just like Augustine Mrema in 1995, but that will be it, and the media behind the former priest can quote us on that.[/COLOR][/SIZE][/FONT]
Source: Dailynews Online

Ukisikia nchi zinaingia kwenye vita ya wao kwa wao chanzo ni matusi kama haya. Siku CCM ikitoka madarakani nitamtafuta huyu mhariri nimuulize vizuri hata kama itachukua miaka ishirini ijayo.
 
Katika majumuisho ya tahariri hiyo, gazeti hilo, The Daily News lilisema: "Na ukweli ni kwamba Dk Willibrod Slaa hatakuwa rais wa tano wa Tanzania."

Kauli hiyo ya gazeti hilo ambalo ni mdomo wa serikali limeibua hisia tofauti kutoka kwa wanasiasa, wasomi, wanaharakati ambao wamelaani na kutaka sheria ichukue mkondo wake.

Dk Slaa, ambaye anaonekana kuzoa mashabiki kadri siku zinavyokwenda, alisema: "Hii inaonyesha kuwa serikali ina mpango mchafu ndio maana wametumia gazeti la serikali.

"Lakini nguvu ya Dk Slaa itathibitishwa kwa kushinda uchaguzi na kwenda Ikulu. Na kwa maana hiyo siku za mhariri zinahesabika."

Kauli hiyo iliungwa mkono na mwenyekiti wake, Freeman Mbowe ambaye alisema: "Tunataka uchaguzi huru na wa haki. Vyombo vya umma vinatakiwa kutumika kwa ajili ya umma na si CCM. Tuumesikitishwa na tahariri hiyo.

"Tunachotaka ni mhariri achukuliwe hatua haraka kwa sababu hiyo inaonyesha mkakati wa serikali si mzuri kwa wapinzani."


Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana watu mbalimbali walioongea na Mwananchi walisema kitendo hicho cha gazeti la serikali ni cha kujaribu kuliingiza taifa kwenye machafuko.

Makamu mwenyekiti wa Nec, Jaji Omar Makungu alisema kauli kwamba Dk Slaa hataingia Ikulu, inaumiza lakini ni juu ya Chadema na Dk Slaa kuamua kulalamika kama wataona imemwathiri.

Jaji Makungu alisema Nec imesikia kauli hiyo lakini haiwezi kuifanyia kazi mpaka kuwe na mlalamikaji.

"Sijalisoma hilo gazeti hilo lakini kauli hiyo inauma... inatakiwa walioumizwa walalamike. Wakikaa kimya, sisi hatuwezi kuchukua hatua. Kamati ya maadili ipo; Chadema au Dk Slaa akilalamika, tutawaita wanaolalamikiwa," alisema Jaji Makungu.

"Tupo tayari kupokea malalamiko. Tuna kamati ya maadili, wakicomplain (wakilalamika), tutajadili na kutolea uamuzi.”

Meneja wa kampeni wa Chadema, Profesa Mwesiga Baregu amelitaka gazeti la Daily News kuutangazia umma wa Watanzania kuwa linamilikiwa na CCM badala ya serikali.

“Ni vyema Daily News ikawatangazia Watanzania kwamba wao ni gazeti la Chama Cha Mapinduzi (CCM) na sio la umma,” alisema Profesa Baregu.

....

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Fordia, Bubelwa Kaiza alisema Daily News ni gazeti la serikali kwa maana hiyo, mhariri na wenzake hawawezi kujituma bali wametumwa na chama au serikali iliyo madarakani.

“Kwa maana hiyo si tu kwamba amekiuka maadili ya taaluma ya habari, lakini, yeye na wenzake wote hawafai kuwapo hapo na kwa kashfa hii, wanapaswa kujiuzulu mara moja kwa kusimamia uovu,” alisema Bubelwa.

“Kama amekubali (mhariri) kutumika vibaya na maadili ya taaluma yake, ni kwamba amehongwa fedha au ameahidiwa cheo na kwa hiyo ni rushwa na ufisadi mkubwa wa matumizi mabaya rasilimali za umma.”

Kaiza aliongeza kusema: “Kwa vyovyote huyo anayesemwa (Dk Slaa) ni bora zaidi kuliko hao wasiosemwa, awe ni rais na waziri mkuu waliopo madarakani au aliyejiuzulu. Hatupendi kuzungumzia masuala ya ndani ya watu, lakini wote tunawajua ‘A’ to ‘Z’ (mwanzo hadi mwisho).”

Source: MWANANCHI.
 
mkumbwa ally anatafuta nafasi ya kuteuliwa kuwa mhariri mkuu wa magazeti ya serikali hivyo anajikomba komba ili ateuliwe katika nafasi hiyo kwa kuandika tahariri zisizokuwa na kichwa wala miguu.
 
Wakati wa Watanzania kukataa ghiriba hizi na Tupo Pamoja na Dr. Slaa na pia nenda hata kwenye page ya Ansert Ngurumo pia kuna maoni haya basi wafanya kura za maoni kama zile za kipindi kile
 
Katika editorial yao wameandika hivi (miongoni mwa mengine):



Yaani Dailynews wanahakika (au wanahakikisha) kuwa Dr Slaa hawezi kuwa raisi wa Tanzania.
Wao ni nani kujua na kutangaza hili? Wameambiwa nini na serikali ambacho wananchi wengine hawajui?
Je tume ya uchaguzi inafanya nini kuhusu hili? BTW- Dailynews ni gazeti la serikali ya watanzania wote.

Dailynews linaendeshwa kwa pesa za kodi ya watanzania wote na sio ccm pekee.
Kama DTV walifungiwa kwa kutangaza matokeo ya Zanzibar mwaka 1995 kabla ya NEC,
Mbona Dailynews wamefanya hivyo hata kabla kula zenyewe hazijapigwa? na ni kwa mamlaka yapi?

Serikali inabidi ichukue hatua mara moja kuhusu hili, na vyombo vingine huru vya habari nchini inabidi vikamate bango ili Dailynews wapate staili yao kwa hili.

Nadhani wanapaswa kufungiwa kama wamesajiliwa kama vyombo vingine... Tuone sasa serikali itachukua hatua gani.
 
Gazeti la Serikali la kiingereza la Daily News leo kupitia kwa mhariri wake limesema ni ndoto kwa Dr. Wilbroad Slaa kuingia Ikulu.

Hili si ni gazeti la Serikali ambalo linaweza kuwa chini ya CHADEMA baada ya oct 31? Hivi huyu mhariri anafikiri ataajiriwa na Uhuru baada ya 31 Oct? Je Dailnews wanajua tayari matokeo? Tume ya Uchaguzi inasemaje kuhusu hili? Kwani ni uongo kwamba Dailynews waliendesha online polls? Je Ni kwa nini walizisitisha?

Ni kweli lakini kaimu mhariri amekwishahakikishiwa kuwa Dr. Slaa hawezi kuwa rais wa Tanzania na hivyo hawana wasiwasi kueleza mtazamo wake binafsi kwenye tahariri ya gazeti la Serikali.
 
Hii Daily News mame- copy na -ku-paste toka Ikulu! Haiwezekani Gazeti la serikali likajiingiza katika ushabiki namna hii. Kama walikuwa na bifu na Raia Mwema wangegombana nao sio mambo ya ushabiki vile!!
 
Mkumbwa Ally afungwe, anatafuta vyeo kwa matumizi mabaya ya vyombo vya ummaaa
Huyu mhariri anastahili kupelekwa mahakamani na tume ya uchaguzi kama kweli ni tume huru.

Huyu mhariri anachochea vita, kwani yeye ni tume ya uchaguzi kutangaza kwamba dr slaa hawezi kuwa mshindi? Kama anataka kufanya kampeni si akaandike gazeti la uhuru chochote anachotaka???

Tunaomba asibezwe huyu mhariri na bodi yake watuambie wanajua siri ya ushindi au wanajua mpango mkubwa wa wizi wa kura uliopangwa na ccm ndio maana anasema hivyo, ama ameshrikishwa kuandaa mkakati wa mwingine wa kuhakikisha dr slaa hatangazwi mshindi hata kama akishinda.

Tunataka huyu mhariri na bodi yake atuambie ameotoa wapi ujasiri kusema Slaa hashindi na kwamba akashugukikie familia yake, je yeye ni nani kumwamuru dr slaa, hivi tukitaka kuongelea family issue je amewachambua wagombea wagombea wote kwa masuala ya familia kama gazeti la serikali?

Kodi za watanzania milioni 42 zinatumika kuliendesha gazeti, ccm wapo milioni tano tu, je anataka kutuambia kampeni zote zinazoendelea ni kiini macho? Ina maana mhariri anataka kutuambia anamjua rais kama msemaji wa tume???

Huyu mhariri ashauriwe akafungue gazeti lake, ni lazima tume kama tume ichukue hatua kali za kisheria vinginevyo tutajua tume hii ni sawa na huyu mhariri labda tume inaujua mpango wa mhariri, maswali ni mengi au wametudanganya kuhusu karatasi za kupigia kura?

Ama wamendaa wizi wa kura? Ama huyu mhariri amepewa rushwa na CCM? Jamani maswali ni mengi saana.
 
Mkuchika tena?achukue action kwa nani. umewahi kuona kesi ya nyani inapelekwa kwa tumbuli?


Ndugu zanguni nimelala kitandani masikio yako Tanzania .Jana usiku nikiwa hapa nimepata ttaarifa kwamba Kinana na CCM na sasa Daily News wana kila sababu ya kulia lia Wamefanya uchunguzi na kupigisha kura wenyewe CCM na Vyombo vya Serikali kabla na ha yawa wengine walio onywa kusema ukweli .

Ukweli toka ndani kabisa unasema hadi mua huu

Chadema na Slaa ni 45% CCM na Kikwete ni 41%

Kikwete rais wa Nchi kukimbia Mdaharo na baadaye chama chake wamejimaliza .Wanakimbia maswali wanahubiri tu kama kanisani na kuondoka .Watanzania si wajinga bwana .Wameamka na sasa wana imarisha mbinu za kuiba kura . Chadema msiweke wenye njaaa kusimamia wakati wa kura za majumuisho pale ndiyo CCM wanacheza ukienda hata kutema mate basi wanafanyaweli.So chagua watu wa maana kwenye kusimamiia yaani Mawakala.
 
tunao akina mkumbwa ally-mhariri aliapa kwamba hata kama dr slaa chaguo la wengi kwa kura za maoni akishindi hawezi kutanganzwa mshindi matokeo yatabadilishwa, piga ua garagaza hawezi kuwa Rais wa tano wa Tanzania,

Jamani gazeti hili linasomwa dunia nzima online, na Tanzania nzima kwa hard copy huyu mtimbwa ally na bodi yake wanayo siri nzito tunayotaka kuijua aiseme, tunayo haki kujua ni vema kumwamuru afafanue na achungunzwe na tume huru anamanisha nini, huyu ni mhariri wa gazeti la serikali kwahiyo anafahamu mambo mazito mengi, tunasikitika sana sana sana kwa serikali kupoteza muda wetu na bugudha za kampeni wakati teyari dealynews wanajua nani atakuwa rais wa tano, hii ni bahati kujua haya mapema huu ni mpango wa mungu kwa kutoa siri hii nzito, mkumbwa anajua kilichofanyika ndio maana amesema slaa piga ua hawezi kuwa Rais, amesema zaidi kwamba slaa akashugulikie familiy issue zake, na kushangaza umma wa watanzania kuna uhusiano gani?

Je amechambua familiy issue za wagombea wengine HUYU MHARIRI ANASTAHILI KUPELEKWA MAHAKAMANI NA TUME YA UCHAGUZI KAMA KWELI NI TUME HURU,HUYU MHARIRI ANACHOCHEA VITA, KWANI YEYE NI TUME YA UCHAGUZI KUTANGAZA KWAMBA DR SLAA HAWEZI KUWA MSHINDI?, KAMA ANATAKA KUFANYA KAMPENI SI AKAANDIKE GAZETI LA UHURU CHOCHOTE ANACHOTAKA???

TUNAOMBA ASIBEZWE HUYU MHARIRI NA BODI YAKE WATUAMBIE WANAJUA SIRI YA USHINDI AU WANAJUA MPANGO MKUBWA WA WIZI WA KURA ULIOPANGWA NA CCM NDIO MAANA ANASEMA HIVYO, AMA AMESHRIKISHWA KUANDAA MKAKATI WA MWINGINE WA KUHAKIKISHA DR SLAA HATANGAZWI MSHINDI HATA KAMA AKISHINDA, TUNATAKA HUYU MHARIRI NA BODI YAKE ATUAMBIE AMEOTOA WAPI UJASIRI KUSEMA SLAA HASHINDI NA KWAMBA AKASHUGUKIKIE FAMILIA YAKE, JE YEYE NI NANI KUMWAMURU DR SLAA, HIVI TUKITAKA KUONGELEA FAMILY ISSUE JE AMEWACHAMBUA WAGOMBEA WAGOMBEA WOTE KWA MASUALA YA FAMILIA KAMA GAZETI LA SERIKALI?

KODI ZA WATANZANIA MILIONI 42 ZINATUMIKA KULIENDESHA GAZETI, CCM WAPO MILIONI TANO TU, JE ANATAKA KUTUAMBIA KAMPENI ZOTE ZINAZOENDELEA NI KIINI MACHO? INA MAANA MHARIRI ANATAKA KUTUAMBIA ANAMJUA RAIS KAMA MSEMAJI WA TUME??? HUYU MHARIRI ASHAURIWE AKAFUNGUE GAZETI LAKE, NI LAZIMA TUME KAMA TUME ICHUKUE HATUA KALI ZA KISHERIA VINGINEVYO TUTAJUA TUME HII NI SAWA NA HUYU MHARIRI LABDA TUME INAUJUA MPANGO WA MHARIRI, MASWALI NI MENGI AU WAMETUDANGANYA KUHUSU KARATASI ZA KUPIGIA KURA? AMA WAMENDAA WIZI WA KURA?

AMA HUYU MHARIRI AMEPEWA RUSHWA NA CCM? JAMANAI MASWALI NI MENGI SAANA.

Watu kama mkumbwa wapo wengi wamewekwa kwenye vyombo vya umma kukandamiza haki za waliowengi na kutumia nafasi hizo kwa maslahi binafsi hii ni hatari na tutanyanyaswa mpaka tukome, leo hii mfumuko wa bei upo juu hakuna anaechukua hatua, leo hii matrition ya pesa yanapotea kwa misamaha ya kodi hakuna anayechukua hatua, leo hii tunasikia mafisadi wakitajwa hakuna anaechukua hatua leo hii huduma za jamii ni hafifu hatua zinazochukuliwa sio za karne ya 21, makatibu wakuu wa wizara wapo, wakurugenzi wapo, na watawala wengi wapo wanajua wanachotakiwa kufanya ni wataalaam lakini shida ni kwamba wanaweza kuwa upande wa mkumbwa ally tutendelea kuwa maskini, tunataka sheria kali ichukuliwe kwa mkumbwa ally na achungunzwe na tume huru ikiongonzwa na jaji kisanga aseme siri nzito aliyonayo.

nina hasira saaana na mkumbwa ally sina hasira na daily news.
 
Dear Editor,
Are you implying, no not implying, are you saying that the Independent NEC in collusion with CCM has already decided who will be the next president of Tanzania? I think this is called rigging, and you Mr. Editor your an accessory to it because in the third week of the campaign no editor can come up emphatically and delare a loser, endorsing yes, declaring a loser a big rigging.
 
This seemingly long post is not explicit. What is it that the author is complaining about? Come out and state clearly what the issue or issues are so that we get the picture. Please do not forget to state the source of the information. All the best
 
Tusubiri tamko la CHADEMA, Tume ya Uchaguzi na iyo inaitwa baraza la wanahabari,wizara ya harhari na Jukwaa la wahariri wakitoa matamko yao juu ya unyanyasaji mkubwa wa demokrasia. Huyu mhariri ni mse********ge kwa kwel.
Samaha mod usinifungie ni hasira tu ya huyu f******la muhariri kwa kwel kanikera ka nini.
Hawa si walifundishwa juz juz juu ya kuripoti taarifa za uchaguz na wasiwe na biased ktk kutoa taarifa zoa
 
Nimemsikia Kinana leo anawajibu waandishi wa habari kwamba hayo mambo ya daily news wakaulizwe wenyewe yeye hajui.

MY TAKE,
Kama CCM hawahusiki, wangekuja front fasta kujibu kama wanavyojibu makombora ya slaa. wangeikana tahariri ya daily news. lakini kwa kuwa wamekaa kimya basi hakuna definition nyingine zaidi ya tuliyoisema kuwa MHARIRI ni kada mtiifu wa CCM
 
Lakini ndugu zangu wa JF hebu tuache kidogo kumjadili Kaimu Mhariri wa Daily News Nd. Mkumwa badala yake tuangalie kama alichoongea kina mshiko wowote. Naepuka kuingia katika mtego wa kumshambulia Nd. Mkumbwa binafsi na kuacha kuangalia suala lenyewe kwa upana mkubwa zaidi unaostahili.

Naomba tujiulize je haya ni maneno yake binafsi Nd. Mkumbwa au yeye anatueleza tu mkakati maalumu uliopo wa kuhakikisha kuwa Dr. Slaa hashindi kamwe? Kimsingi siamini kuwa anachokisema Mkumbwa ni mtazamo rasmi wa gazeti la Serikali la Daily News ila naamini kuwa unaakisi mtazamo rasmi wa Serikali yenyewe ambayo ndiyo hasa mmiliki wa gazeti hili. Nionavyo mimi Mkumbwa amesaidia tu kutufungua macho kwa kutumia kalamu yake.

Mimi nadhani wapenzi, wanachama na mashabiki wa CHADEMA na wapinzani wengine wanatakiwa kujiuliza ni nini hasa kinampa jeuri huyu mtumishi wa umma kuutangazia ulimwengu mzima kuwa Dr Slaa hatashinda kamwe uchaguzi utakaofanyika tarehe 31/10/2010. Ni wakati muafaka sasa kwa CHADEMA na wapinzani wengine kujua (ama ku-anticipate) mikakati ya upande wa pili wa washindani wao. Kimsingi Serikali ya CCM ndiyo mshindani mkubwa wa CHADEMA na wapinzani na ndiyo inayompa Nd. Mkumbwa jeuri ya kuutangazia ulimwengu kuwa Dr Slaa na CHADEMA hawatashinda kamwe.

Mimi siamini kuwa Nd. Mkumbwa ni mbumbumbu kiasi cha kuropoka kuwa Dr Slaa hatashinda wakati hana jinsi yoyote anayoweza kuhakikisha kuwa mchakato wa uchaguzi unamweka madarakani kiongozi anayemtaka yeye. Na sidhani kama Mkumbwa anabahatisha anapojaribu kuufananisha uchaguzi huu na ule wa 1995 ambapo Mrema aliambulia patupu pamoja na kuwa alionekana kuvutia watu wengi wakati ule. Kuna jambo hapo!!!.

Kumbukeni kuwa ni mwaka 1995 ambapo CUF ilitangazwa kuwa mshindi wa uraisi Zanzibar (na Channel Ten baada ya kujumlisha idadi ya kura ya vituo vyote vya uchaguzi) na ikafikia mpaka CCM Zanzibar wakautangazia Ulimwengu kuwa hawatakubali matokeo. Lakini kilichotokea kila mtu anajua.

Naomba tutafakari kwa kina mambo yafuatayo:

  • Je serikali ya CCM haitafanya rafu tulizozizoea za ama kuharibu mwenendo wa uchaguzi ama kuiba kura pale mwenendo unapokwenda kama ulivyopangwa? Kwa wanaokumbuka vizuri mwaka 1995 hapa Dar es salaam matokeo yalifutwa na uchaguzi kurudiwa baada ya wiki mbili. Lakini kabla ya hayo tuliokuwepo Dar tulishuhudia makaratasi ya kupigia kura ama yakicheleweshwa kwa makusudi au kutokufika kabisa kwenye vituo vya kupigia kura.
  • Je wasimamizi wa uchaguzi ambao ni wakurugenzi wa miji wana ubavu wa kutangaza matokeo yasiyoifurahisha CCM ambayo kimsingi ni kwenda kinyume na matakwa ya mwajiri?
  • Je CHADEMA na vyama vingine wana uwezo wa kuweka waangalizi waaminifu wa kura kwenye kila kituo cha kupigia kura nchi nzima? je hawa waangalizi watakuwa na ubavu wa kuhimili vitisho vya makada wa CCM, wasimamizi wa uchaguzi, makamanda wa polisi, maafisa wa usalama wa Taifa, wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa etc?
  • Je CHADEMA na vyama vingine vina uwezo wa kusimamia na kudhibiti zoezi zima la ujumlishaji na utangazaji wa matokeo ya Udiwani, Ubunge na Uraisi nchi nzima? Kumbuka msimamizi wa uchaguzi akisha tangaza mbunge huna jinsi isipokuwa kwenda mahakamani. Kwa uraisi akishatangazwa na NEC ndio imetoka hiyo huwezi hata kwenda mahakamani kudai haki mpaka miaka mitano baadaye utakapojaribu bahati yako tena.
  • Je CHADEMA na vyama vingine wana ubavu wa kuhumili vishindo vya rushwa, ufisadi, ununuzi wa kadi za kupigia kura na mambo yanayofanana na hayo ambayo tunavyoongea tayari yanaendelea?
  • Je mpaka sasa tuna uhakika gani kuwa orodha ya wapiga kura iliyotangazwa na NEC ni ya kweli na kuwa watu wote waliotangazwa na watu hai na siyo watu hewa (fictitious) ambao wamewekwa kimkakati kuongeza idadi ya kura za wagombea wateule?
Haya ni baadhi tu ya mambo ambayo yananifanya nifikirie mara mbili kauli ya Nd. Mkumbwa kuwa Dr Slaa hatashinda kamwe na kuwa kitakachofanyika mwaka 2010 ni sawasawa na kilichofanyika kwa Mrema na Maalimu Seif Sharif Hamad mwaka 1995. Siamini kuwa kinachomfanya Mkubwa aamini hivyo ni kutokana matatizo binafsi ya kifamilia ya Dr. Slaa kama anavyoonesha kweye tahariri yake. Kwani tungetumia kigezo hicho anachokiongelea Mkumbwa kama sifa pekee ya kumchagua rais nadhani tungepata matokeo ya kushangaza sana ya urais.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom