Daily News na Habari Leo waendelea kuchakachua habari.....

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,172
Leo Daily News ina kichwa cha habari kisemacho............"Obama salutes JK, Shein........."

Na Habari Leo wao wasema Chadema yakubali yaishe na JK.........................sasa kuwatuma wabunge wake wakachape kazi Bungeni.........

Sote tunafahamu Obama alitupongeza watanzania wote kwa kuendesha uchaguzi wa amani na aliwapongeza Shein na Hamad lakini hakumpongeza JK...........kwa hiyo Daily News wamechakachua barua ya Obama kwetu........................................


Na Jana Chadema kupitia Mwenyekiti wao Freeman Mbowe alipokuwa anaongea na waandishi wa habari alitoa tamko kuwa wao hawamtambui JK na wale wote atakaowateua...........

.............habari hii imeungwa mkono karibu na magazeti yote.......Tanzania Daima imemnukuu Dr. Slaa akisema...................Hatutamtambua JK....................

The Citizen nalo limesema...............We don't recognize government, says Chadema.................

Majira nalo limesema....................................Slaa amkataa JK...........Chadema kutotambua uteuzi wowote wa JK..

Na gazeti la Mwananchi lina habari hiyohiyo...............................Sasa hawa wenzetu wa Habari Leo hiyo taarifa ya kuwa Chadema yakubali yaishe na JK wameitoa wapi?
 
Habari leo nimechukizwa na habari zake mpaka nimeamua kuliweka kwenye pipa la taka!!utadhani gazeti binafsi.
 
Unajua hivi vyombo tunavyosema ni vyombo vya habari vya umma inabidi vijiangalie utendaji wao wa kazi..Itafikia siku vitajizika vyenyewe..kwani huu upendeleo wa habari na kupotosha ukweli wa mambo sio haki kwa watanzania!
 
Hata mkiyaita magazeti mimi nawashangaa. Nadhani wanaJF inabidi tupendekeze majina mbadala ya haya madude (naogopa kuandika neno gazeti) yanayotufanya sie majuha tusiojua kitu. Kwanza yanaandikwa na makanjanja na pili ni ya serikali kwa maana ya kikundi cha wahuni fulani na sio wananchi kama inavyopaswa kuwa. Ingekuwa serikali kwa maana ya wananchi yangekuwa sauti yetu na sio ya wahuni kadhaa.

Natafuta jina ila sipati, ukipata muungwana weka hapa......
 
hivi si kuna wakati Habarileo lilipoanza mbona lilikuwa linakwenda vizuri na habari zilikuwa zinaandikwa kitaaluma? Nini kimetokea hapo katikati? Ile timu ya akina Kaguo, Athumani Hamisi, na bosi wao Mruma imeishia wapi?
 
Akina kingoba na mhariri wao walisha acha kanuni za habari tangu enzi zile walipoamua kudhalilisha miili yao(habari) na roho zao (maadili) kwa ajili tu ya vijisenti.wana jamvi njaa mbaya.tuyasusie magazeti yao
 
Hata kama walikuwa wanavutia watu wanunue nadhani hivi vichwa vyao vya habari vitafanya wasomaji wengi zaidi waliweke kapuni.
 
Fanya uchunguzi ujue ni nani anamiliki magazeti haya...! yote na mengine mengi yanamilikuwa na RA
 
Masikini JF, great thinkers wanatoweka kinaingia kizazi kipya ambacho they dont think beyond what they want. Kutofautiana ndio kumefanya JF iwe na mashabiki sasa watu wote wakiwa upande mmoja itakuwa sio poa.

Kubalini mawazo tofauti na yenu.
 
upuuzi tu.....sijui kwa nini serikali haifungii vijarida hivi vyenye maslahi ya m,afisadi?
 
Wale majamaa wa Synovate walitoa report ikisema haya magazeti mawili pamoja na Rai na Mtanzania wanalengo mbaya. Aise hapo for the first time wamepatia matokeo halali.
 
Hayo magazeti yataendelea kununuliwa na wanaokunywa maji ya kijani (Wana CCM) peke yako.
 
Masikini JF, great thinkers wanatoweka kinaingia kizazi kipya ambacho they dont think beyond what they want. Kutofautiana ndio kumefanya JF iwe na mashabiki sasa watu wote wakiwa upande mmoja itakuwa sio poa.

Kubalini mawazo tofauti na yenu.

Tatizo la kauli hii ni kubariki uongo kwa kivuli cha kuvumiliana...................Only the truth will set you free.....................
 
Back
Top Bottom