Kwakweli jambo usilolijua ni kama usiku wa giza...siku zooote tunaposikia misamaha ya kodi tunaelewa na ndivyo ilivyo there is some one who is paying that tax on behalf of the person who is exempted...sasa hili kwa upande wa Hospitali zetu nchini kumbe ni tofauti .... Mgonjwa anapopewa msamaha yaaani anatibiwa bure hakuna mamlaka yoyote serekalini inalipa au kufidia gharama za matibabu kwa Mgonjwa aliyepewa msamaha jambo ambalo Hospitali zetu nchini huduma zinazidi kudorora....chakusikitisha zaidi ni pale niliposikia kuwa hili swala la msamaha hata watu kama viongozi wa kisiasa kama wabunge mawaziri hupewa exemption Hospitali ya taifa Muhimbili.... Hii sidhani kama Ndiyo ilikuwa dhana mzima ya exemption kama ilivyowekwa na serikali....naamini kuwa sababu kubwa ya serikali kuweka utaratibu huu ni ili kusaidia watu wale ambao kwakweli hawana uwezo kabisa lakini kwa Hospitali ya taifa muhimbili ni mpaka mbunge anapewa msamaha jambo ambalo ni mzigo mkubwa kwa Hospitali zetu...gharama za matibabu ziko juu sana na endapo serekali isipokuwa makini itafikia mahali Hospitali zitashindwa kutoa huduma...kuna haja ya serekali kuuangalia utaratibu wa misamaha ya malipo ya tiba kwa upya kwasababu people abuse the system. Mtu kama mbunge au waziri kwanini atibiwe view?? Madawa na reagent za maabara zinazotumika kumpa tiba yanarudishwaje? Hata hao wafadhili wanaotusaidia jamani misaada ina mwisho. Kama mtu akipewa msamaha wa kodi kwa gari alilonunua haimaanishi kuwa ile kodi hailipwi kuna mamlaka inalipa kwa niaba yake...sasa inakuwaje kwa huduma za Hospitali??