Dah nimemkumbuka sana aliyekuwa mpenzi wangu!

Khan

JF-Expert Member
Dec 6, 2012
6,162
2,000
Poleni na misukosuko ya kusaka mkate wa kila siku hasa katika kipindi hiki ambacho asilimia kubwa ya rasilimali za nchi zinaelekea katika ujenzi wa miradi mikubwa!

Juzi niliona post bwana mdogo mmoja amepost kwamba ana demu wake wa miaka 20 anamfanyia kila kitu, kama kumfulia, kumpikia na kumdekia na mengineyo kadha wa kadha!

Nilimshauri kwa nafasi yangu though si lazima auamini sana, nilimshauri kutokana na uzoefu nilionao mwenyewe na mwingine kwa kusikia na kuona kwa wengine.. kizungu wanaita "experience".. je huu uzoefu wangu ukoje?

Nilikuwa kwenye mahusiano na binti wa miaka 20 i was 24 by that time, honestly nilikuwa na nia njema ya kumuoa na binti kwa mara ya kwanza alionekana kueleweka na tuliaminiana (though as a man sikuweka 100%)..kama wapenzi tulifanyiana mengi kiasi kwamba huwezi kuamini kama tungeweza kuachana.

baada ya kama mwaka na miezi 8 binti akaanza ku change mara babake hataki awe na mimi.. mara baba kamnyang'anya simu.. nikaanza kuona kama vile nachezwa though niliamini kwa kiasi flani huenda baba yake hataki awe na mimi but sikuamini siku mfanyakazi wa kwao na mdogo wake kwa nafasi tofauti waliponiambia baba yao wala hajafuatilia chochote kuhusu mahusiano yake.

toka hapo tukawa na mawasiliano dhaifu.. bila kumfanyia lolote baya kwa kuwa nilimheshimu kwa nafasi kubwa aliyoplay katika maisha yangu..

Basi one time nikaamua kumtext alikuwa na rensponse mbovu.. psychologically nilielewe she dont need me.. nikaamua kumpotezea up to date!
Kiufupi ni mwanamke ninaempenda na ni mwanamke ambaye ukimshape atakuwa mama bora sana na naweza kusema atakayependwa na yeye atakuwa na furaha na raha maishani mwake.. though mimi nilishindwa.

My take: Vijana wa kiume msiweke sana malengo kwa wanawake below 25, hao wengi wao wana mood swings.. bado umri wao unaruhusu kuchagua chagua.. bado akili na utashi wao ni mdogo katika kuchambua na kudadavua.. sisemi wote wapo hivyo lakini asilimia kubwa sana.. sasa siwezi kukupa guarentee ya wewe kuwa katika hizo asilimia chache za wataobahatika.

Narudia kamwe usiweke expectations kubwa kwa wanawake wa umri tajwa.. utakuja kunishukuru!

Vijana wa kike: wanaume wengi wakipenda ni ngumu sana kukuacha, mwanaume ana mapenzi ya dhati yanayodumu kuliko mwanamke.. mwanaume hawezi kumsahau mwanamke anayempenda hata siku moja.. anaweza kutoka na mwingine kwa sababu ya tamaa ila anajua kabisa mapenzi yake yapo kwa nani... Mheshimu sana mwanaume anayekupenda.

Mwisho: E nimekukumbuka sana, sifanyi jitihada zozote uwe wangu tena ila nashukuru kwa uwepo wako maishani mwangu.. Nimejua ni aina gani ya mwanamke nahitaji.. Namshukuru Mungu kwa kukuleta maishani mwangu.
 
Joanah

JF-Expert Member
Aug 14, 2016
15,252
2,000
Kwa taarifa yako umri kuanzia 20-25 ndio wana asilimia kubwa ya kuwa na akili kubwa kubwa

Halafu ushauri uende pia kwa wanaume...msipende kuumiza wanawake wanaoonesha kuwapenda kwa dhati,tulieni na mmoja basi
 
Mkuu mwanamke umri unavyokwenda ndivyo akili huongezeka hasa kwa sababu ya uzoefu.. kwa umri huo tajwa si kwamba akili ni nyingi.. la hasha bali ujuaji mwingi!

Btw: asante kwa ushauri!
 
Bill9

Member
Jul 21, 2019
39
150
Hii post imebeba feelings sana ,na inaonesha uhalisia mkuu kwel umeumizwa,,, we share the same story yani ulivoandika kwa uchungu hadi nmekumbuka jinsi nlivompenda yule mschana ,yan nilimpenda kushinda nlivojipenda ila mwisho Wa siku alienda, kaniacha na best lesson
 
Khan

JF-Expert Member
Dec 6, 2012
6,162
2,000
Hii post imebeba feelings sana ,na inaonesha uhalisia mkuu kwel umeumizwa,,, we share the same story yani ulivoandika kwa uchungu hadi nmekumbuka jinsi nlivompenda yule mschana ,yan nilimpenda kushinda nlivojipenda ila mwisho Wa siku alienda, kaniacha na best lesson
Kweli kabisa kiongozi..Mara pengine huwezi jua nini kesho imebeba kwa ajili yako.. huenda kesho itatuondolea maumivu ya leo!
 
godimpare

JF-Expert Member
Feb 10, 2014
2,789
2,000
Daah pole sana ila nami ndo ninalo li exipiriance now but nitazoea tu,ila mi kosa ni langu siwezi ku complain sana
alafu nilikua na ka binti nilikaachia namba ndo kana mature vyema leo anakuja nitafuta baada ya miak 2na nusu ana mtoto wa miezi miwili, anatamani nimuoe coz hana mwelekeo nawaza sana ila sitoweza
 
Mkuu watu kwa sasa hawatoelewa mpaka yawakute.. nenda mbele na maisha yako.. mtoto wake alee na bwanake
 
ommy15

JF-Expert Member
Jan 23, 2011
637
1,000
Mkuu watu kwa sasa hawatoelewa mpaka yawakute.. nenda mbele na maisha yako.. mtoto wake alee na bwanake
Nilitaka niseme hivi bro. Poleni wazee ndio maisha wanasema the first cut is the deepest
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom