Dah! Hili la kuwaua washukiwa wa ugaidi nawahapa hongera Tanzania

MK254

JF-Expert Member
May 11, 2013
32,238
50,411
Magaidi sio watu wa kuchekewa, akiua basi naye anafaa kufa, tena huko huko mbugani. Polisi wa Tanzania wametoa taarifa kwamba wameua magaidi waliohusika kwenye mauaji ndani ya msikiti Mwanza. Huo ndio mwendo sahihi, yaani hamna ni wala nini, kafie mbali tena kwa risasi.

Tatizo kwetu hawa wakereketwa wa haki za kibinadamu wanapenda kupiga makelele sana, yakifanyika kama hayo ya Tanzania utaskia mara oohh! Wanaonewa, mara ooohh!! Lakini wanapotuchinja hakuna anayesema.

CC: MOTOCHINI FaizaFoxy

Taarifa zaidi hapa
Terror suspects shot dead
 
hata huku bongo kunawajinga wanajifanya kuzijua sana haki za binadam hadi kwa majambaz na magaidi. ila mh. raisi alisha waagiza police kuwa ikitokea jambaz anasilaha wanatakiwa kumnyang'anya haraka kabla ya wao kunyang'anywa. "kill them b4 they kill u"
 
Hivi si mtaua watu wasio na hatia
"Mtuhumiwa " which means ma police hawana
Uhakika kama ni wao wenye kosa au La.

Kwa hili sikubali nalo.
 
ukishasema ni mshukiwa ina maana bado hana tuhuma sio sawa kumuua mpaka mahakama ithibitisshe tuhuma hizo

Sasa hapo aliyeuawa kwa kujibizana risasi na polisi ulitegemea nini, apewe chakula cha jela na kupotezea watu muda wa kesi kotini. Yaani ukinyanyua bastola na kuanza kuwafyatulia polisi risasi, hamna haja ya wewe kuishi tena. Wapigwe, tena risasi za kichwa na kuhakikisha wamekufa kabisa.

Mtuhumiwa sahihi ni yule anayejisalimisha kwa polisi kwa njia za amani. Ndio hapo utaeleweka na kupelekwa mahakamani ukawazuge watu na kesi zisizoisha na mawakili wachumia tumbo.
 
Hivi si mtaua watu wasio na hatia
"Mtuhumiwa " which means ma police hawana
Uhakika kama ni wao wenye kosa au La.

Kwa hili sikubali nalo.
ngoja nikwambie jana huku kwetu temeke mida ya saa mbili kulikuwa na kurushiana risasi kati ya hao magaidi na polisi,mmoja ameuawa mwingine kapigwa za miguu,niambie hapo bado unawaita hao ni watuhumiwa ??mtu anarushia polisi risasi bado akiuliwa unamwita alikuwa mtuhumiwa??
 
Huyo aliyepigwa mguuni, ingempata kifuani ingekua poa sana.
 
ngoja nikwambie jana huku kwetu temeke mida ya saa mbili kulikuwa na kurushiana risasi kati ya hao magaidi na polisi,mmoja ameuawa mwingine kapigwa za miguu,niambie hapo bado unawaita hao ni watuhumiwa ??mtu anarushia polisi risasi bado akiuliwa unamwita alikuwa mtuhumiwa??
Hayo ni maneno yako.
Je una uhakika gani ndio walio ua watu
Msikitini?
 
Hayo ni maneno yako.
Je una uhakika gani ndio walio ua watu
Msikitini?
hujanijibu swali langu na mimi,bado huyo mtu unamuita mtuhumiwa??
na hilo swali lako najua wangekuwa FBI ungewaamini lakini kwakuwa ni askari wa upelelezi wa bongo basi doubt kibao......
 
ngoja nikwambie jana huku kwetu temeke mida ya saa mbili kulikuwa na kurushiana risasi kati ya hao magaidi na polisi,mmoja ameuawa mwingine kapigwa za miguu,niambie hapo bado unawaita hao ni watuhumiwa ??mtu anarushia polisi risasi bado akiuliwa unamwita alikuwa mtuhumiwa??

Kapigwa mguuni? Hapo polisi waliharibu risasi bure, maana huyo alikua anajibizana na polisi moto kwa moto akiwa na nia ya kuwaua polisi. Wangempiga ya kichwa tu. La sivyo ahojiwe kwa kichapo hadi awaumbue na wengine waliojificha.
 
hujanijibu swali langu na mimi,bado huyo mtu unamuita mtuhumiwa??
na hilo swali lako najua wangekuwa FBI ungewaamini lakini kwakuwa ni askari wa upelelezi wa bongo basi doubt kibao......
Acha porojo wewe.
Police wenyewe wamesema ni watuhumiwa.
Watuhumiwa wa mauaji ya Mwanza, Tanga wauawa Dar
Kasome vizuri hiyo thread na angalia hiyo video ya you tube.

Kama unataka jibu langu "ndio ni wa tuhumiwa "
 
Sasa hapo aliyeuawa kwa kujibizana risasi na polisi ulitegemea nini, apewe chakula cha jela na kupotezea watu muda wa kesi kotini. Yaani ukinyanyua bastola na kuanza kuwafyatulia polisi risasi, hamna haja ya wewe kuishi tena. Wapigwe, tena risasi za kichwa na kuhakikisha wamekufa kabisa.

Mtuhumiwa sahihi ni yule anayejisalimisha kwa polisi kwa njia za amani. Ndio hapo utaeleweka na kupelekwa mahakamani ukawazuge watu na kesi zisizoisha na mawakili wachumia tumbo.

Wengine wanajisemea tu kwa kuwa ugaidi wanausikia kwenye Radio - siku moja wakiwahibukia ndio watajifunza kitu.

Ugaidi si lelemama au ngoma za mchiriku - wanapashwa kupigwa vita popote walipo hakuna cha kukamatwa na kuburuzwa mahakamani wala nini sijui - sumnary excution ndiyo lugha wanayo ielewa magaidi hakuna cha kuwachekea.

Mataifa yetu ya Africa specifically East Africa tunapashwa kuwa kitu kimoja linapokuja suala la Ugaidi, tusijidanganye no one is safe - waswahili usema ukiona wenzako wananyolewa na wewe kichwa kiweke /kitie maji.
 
kabla ya kutokomea gizani Alisikika akisema ''nakumbuka kisa uhasama ule waliokuwa nao police na wale wahalifu sababu ya maslahi na kuhifadhi siri endapo wangewekwa korokoroni pia nakumbuka ugomvi baina ya bosi wao na wale waliopewa jina la wahalifu ilihali walikuwa raia wema ndio maana waliamua kumaliza utata eneo la tukio kwa hyo wanangu kila tukio si kama linavyotangazwa ila wanavyoamua kuficha siri zao''
 
Back
Top Bottom