Dagaa kutoka Tanzania kuuzwa nchi za nje ikiwemo Ulaya

kidadari

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
8,647
9,595
Tanzania kuuza dagaa nje ya nchi

Dagaa waliokuwa wakidhaniwa kuwa ni chakula cha watu maskini, sasa wameboreshwa na kupata sokoDar es Salaam. Dagaa waliokuwa wakidhaniwa kuwa ni chakula cha watu maskini, sasa wameboreshwa na kupata soko nje ya nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati akifungua mashindano ya wachakataji dagaa yalioanzishwa na Jumuiya ya Ulaya (EU), Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Yohana Budeba, alisema dagaa hao watauzwa katika nchi za Ulaya, Zambia, Namibia, Malawi, Uganda na Zimbabwe.

Alisema vikundi vinavyoshiriki mashindano hayo ni 20 kutoka mikoa ya Mwanza, Kigoma, Geita, Mara na Kagera na kwamba Serikali imejipanga kutoa elimu ya kutosha kwa wachakataji na wavuvi.

Budeba alisema watazunguka katika mikoa hiyo kuwahamasisha wavuvi kutumia nyavu sahihi za uvuvi ili kuwalinda dagaa wasiishe kama ilivyokuwa kwa samaki aina ya Kamba.

Chanzo: Mwananchi
 
Una uhakika na hicho cheo? Katibu Mkuu wizara gani? By the way good news viva Tanzania
 
Last edited:
Kuna dagaa wa Zanzibar (Maji chumvi) nao sio haba japo sijaona ushiriki wa Zanzibar kwenye huo mchakato.
Ni hatua nzuri inayostahili pongezi.
 
Tusubiri watapanda bei maana bongo kilo itakuwa 20,000
 
Back
Top Bottom