Tume ya uchaguzi hufanya kazi kwa kuifurahisha CCM. CCM wanafahamu fika vijana waliotimiza miaka kumi na nane wote ni wafuasi wa CHADEMA na vyama vingine vya upinzani. Hivyo hiyo ni janja ya kuibeba CCM.
Nadhani unaongea kwa ushabiki tu. Tume ya Uchaguzi hufanya kazi kufuatana na sheria za uchaguzi. Uboreshaji wa Daftari la wapiga Kura nalo linalindwa na sheria zake. Kwa sasa sheria inawataka kuboresha mara mbili tu kwa kipindi cha miaka mitano, yaani kutoka uchaguzi mwingine hadi unaofuata. Sheria haisemi kuboresha wakati wa uchaguzi mdogo. Sasa hilo sio kosa la Tume labda useme sheria ni mbovu tu.
mkuu wangu lazima utambue kwamba ktk nchi hii sheria zinatengenezwa kusaidia watawala wabakie madarakani.
Je ikiwa ni sheria, hamuoni kuwa wataalamu wa sheria ndani ya serikali aidha ni wajinga katika suala hili au hawana uzalendo
na haki za watanzania. Kwanini wenyewe wasiwe wa kwanza kuliona hili?
Na Rorya pia wafanye hivyo hivyo haraka iwezekanavyo kwani tumemchoka mbunge yule ambaye hata siku moja hajawahi kukohoa bungeni!
Na hizi kata tatu tunapiga kura 02/10/11
1. Nyahongo
2. Mkoma na
3. Nyamtinga.