Dada zetu kuweni makini na madanga mnayopata sehemu za starehe

jerryempire

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
5,128
8,648
R.I.P inasikitisha sana

Huyu msichana anaitwa Barke, ameuliwa kifo vibaya sana anaishi llala mtaa wa utete na Pangani.

Inasemekana siku ya tukio tatehe 31, walichukuana na mwenzake wakaenda Tabata (Kitambaa cheupe) kwenye starehe zao huku wanakunywa akiwa na mwenzake na mbaba waliyempata hukohuko (Danga).

Sasa yule mwenzie na marehemu Barke akaenda chooni, anarudi anakuta mwenzie hayupo pale walipokuwa wamekaa anamuangalia hamuoni, anampigia Barke simu imezimwa, siku nne mfululizo. Sasa msichana inabidi ahadithie kwao kuwa nimetoka na Barke na ninampigia simu hapatikani siku ya nne sasa simuoni na nyumbani kwake hayupo. Wakaenda police na taratibu za kumtafuta zikaanza.

Kwenye kumtafuta wakaenda hospitali zote kufika Amana wakaambiwa "Bwana, hapa ililetwa maiti ya mwanamke tarehe 1, baada ya kukaa sana imechukiliwa imepelekwa Muhimbili" ndugu walivyoenda Muhimbili wakautambua mwili wa Barke na walipomchunguza wakakura ametolewa figo.

Pumnzika kwa amani dada inauma sana hii yote inatokana na umasikini kikubwa ni umakini, mtu humjui anaanza kukunywesha pombe kwa kigezo cha danga.

NB: Nimetoa picha baada ya kupata pm za wengi kuwa nifanye hivyo nami nmetoa kulinda faragha ya marehemu ila nmeacha thread kama funzo kwa dada zetu
 
Last edited:
Back
Top Bottom