Dada zetu kama mnajua hampo tayari kuwa Mama na hamuwezi kulea basi jichungeni

Mzukulu

JF-Expert Member
Feb 14, 2020
1,401
2,631
Katika hali isiyo ya kawaida kabisa Jana jioni katika Vichaka vya iliyokuwa Tanganyika Packers Kawe aliokotwa Mtoto wa kati ya miaka Miwili hadi Mitatu wa Kiume akiwa ametelekezwa hapo na Mama yake. Najua Polisi ya Kawe inayo tayari hii taarifa kwani Juhudi kubwa zilifanywa na Walinzi Shirikishi wa hilo eneo pamoja na akina Mama baadhi waliokuwa jirani hapo.

Wanawake ni Bibi zetu, Mama zetu, Dada zetu, Wapenzi wetu na hata Wake zetu pia na tunawaheshimu mno ila Mimi Mzukulu huwa kuna muda huwa siwaelewi halafu mnanipandisha Hasira kwa mnayoyafanya. Hivi kama unajijua kabisa uko tarehe mbaya za Kushika Mimba ni kwanini huwa mnakubali ' Kunyiriwa ' na Wanaume tena bila ya hata Kutumia Condoms?

Inaingiaje Akilini Mwanamke ambaye ulikubali Mwenyewe ' Kunyiriwa ' na Mwanaume kisha ukabeba Mimba yake halafu ukajifungua Mtoto mzuri tu ukamlea kwa miaka Miwili au Mitatu hiyo kisha bila hata Huruma wala Haya ( Aibu ) ukaenda Kumtupa Kichakani kisha Kutokomea hadi Wapita njia walipopita hapo na Kumsikia Akili ndipo wakamuokoa na Kuripoti Tukio hilo Polisi?

Kwa hili Dada zangu Leo nitawasema sana hata kama mkija na Utetezi wenu kuwa Sisi Wanaume nao huwa ndiyo tatizo katika huu Upuuzi Wenu.
 
ili uwaelewe wanawake vizuri ni lazima ufe kwanza brother.

wanatupa mtoto wananunua mdoli wa mtoto.

Ngoja waje.

Sadly they are very busy at night crying with their tedy bear’s na watoto wanatupa (baadhi yao)
 
  • Thanks
Reactions: p2k
Kumbuka baadhi ya wanawake huzaa kwa makubaliano na wanaume kuwatunza ila gia zikibadilikia angani ndipo mambo kama haya hutokea.

Wengi wao hushindwa kuwatunza watoto wakiwa pekee. Na kwakuwa Shetani naye huwatumia sana ke hujikuta wanafanya maamuzi hayo.

Pia wengine hurubuniwa na wapenzi wao wapya, kwa ahadi nyingi.

Lakini wengine huogopa aibu za u- single mother na wanakuwa wameshaongopa kuwa hawana watoto!

Point :
Shetani huwatumia sana wanawake kwa kiwango kikubwa. So wanaweza kuamua lolote.
 
Hiyo ni athari ya kufanya tendo la ndoa nje ya ndoa.

Ndiyo maana tunasisitiza, ndoa na tendo la ndoa viheshimiwe na watu wote na viwe ni kwa ajili ya wanandoa pekee.
 
Back
Top Bottom