Dada zangu na Kaka zangu please nisaidieni nipo kwenye Dillema.

Akilitime

JF-Expert Member
Dec 27, 2017
581
757
Ninafurahi kuwa sehemu ya jukwaa hili lililosheheni wataalamu, washauri waliojaaliwa hekima na busara.

Naamini kupitia jukwaa hili pasi nashaka nitaongezewa utambuzi kiakili na kifikra.
LENGO: Nina Girl friend ambaye takribani miezi 7 yapata tangu tuanzishe mahusiano ya kimapenzi,

Kutokana na ups and down za hapa na pale ambazo tumekuwa tukipitia kiukweli nimekuwa nikiona ni jinsi gani bidada huyu alivo na upendo wa dhati kwangu, Ilikuwa ikifika hatua yeye ndo ananitoa tukipanga kwenda out, muda wote hakupenda kuniacha mwenyewe kuingia gharama,

Nawaza sema amekuwa akinichukulia na kunicare kama mume wake na mimi nikimtunza kama mke wangu.

TATIZO: Mda wote wa mahusiano yetu, kamwe kaka yake hakupenda mdogo wake awe kwenye uhusiano na mimi,

Huyu kaka ni wa makamo na ana familia na watoto, Imefikia hatua simu ya Gf wangu kaiwekea track calls(spy) ili kunasa wawasiliano yetu, Katika hayo yote bado huyu dada anasisitiza hawezi niacha,

Imefikia hatua natishiwa kuuawa na huyu kaka, akidai kwamba mdogo wake bado mwanafunzi japo kamaliza kidato cha sita huu, na hakubahatika kupata nafasi ya chuo mwaka huu wa masomo,

Bidada tangu naye apokee vitisho kutoka kwa kaka yake hii ni siku ya pili simu yake haipatikani. Yeye anaishi Dodoma, me nipo morogoro. Katika hili bado nimeshindwa kung'amua. Kuachana naye ili kutimiza mapenzi ya kaka yake, au kuendelea naye na kutimiza malengo ya kuoana,

Ili hali nikichukiwa na kaka yake?
Naombeni ushauri wakuu na wataalamu wa jamvi hili.

Asanteeni
 
Miezi saba ni muda mchache sana katika kung'amua safari ya ndoa. Kaka mtu hapendi uhusiano wako na dada yake, maana yake ni kwamba huenda familia ina mkakati wa kimaisha kwa binti kabla hajaolewa.

Kwanza ni vizuri ukajitahidi kufahamu ni nini familia yao wanapanga juu ya binti yao kwa maisha yake ya baadae. Pia jipe muda wa kutafiti mambo mengine kwa huyo umpendaye. Yeye kukujali kwa namna ulivyoelezea bado haishawishi sana kwa uhalisia wa maisha.
 
hii mitoto ya siku hizi bana...yaani linafurahia kabisas kuhongwa na mwanamke na kuwa "MTAJI KIUNO" af bado unajiuliza kwanini kaka yake anakumind...hapo ukute wajua pandia kiunoni tu..shule zifunguliwe aisee mshatuchosha
 
Tukiwapa nafasi ya kutuomba ushauri kama kaka zenu mnaomba ushauri wa mapenzi!! Afu mnataka kesho Nchi yenu ndiyo Iwe inawapa wazungu Mitumba. Kweli dunia adaaa
 
hii mitoto ya siku hizi bana...yaani linafurahia kabisas kuhongwa na mwanamke na kuwa "MTAJI KIUNO" af bado unajiuliza kwanini kaka yake anakumind...hapo ukute wajua pandia kiunoni tu..shule zifunguliwe aisee mshatuchosha
Asantee mkuu, Lakini si wote waombao ushauri ni wanafunzi, Me nipo na kazi yangu tayari, pia ni mjasiriamali hapa mjini
 
Subiri kaka yake afe utamfaidi sana huyo manzi. Kulazimisha mapenzi wakati mwingine ni kujitafutia matatizo...inavyoonekana huyo kaka ni kama vile mzazi wa huyo manzi yani kila kitu jamaa ndiyo anasimamia.
 
Asantee mkuu. Ila kwa taarifa me sio mwanafunzi, nishamaliza kitambo, nipo na shughuri zangu hapa mjini
 
sasa boss unakazi yako halafu mwanaume unajitapa kua mtoto wa form six ndo anasimamia gharama..aibu kwa mtoto wa kiafrika
Sio kuwa mpenzi wako anapojitolea kukifanyia jambo fulani . Ndo wewe unakuwa huna uwezo nao mkuu
 
Back
Top Bottom