Dada yangu anasumbuliwa na kubanwa na pumzi na maumivu ya mbavu au mgongo

Frustration

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
3,095
4,059
Habari wanajukwaa hili la Afya.
Nina dada ambaye anasumbuliwa sana na hali ya kubanwa na pumzi na kushindwa kuongea. Mara ya kwanza alinitumia sms kuwa halu yake ni mbaya anashindwa kupumua na anahisi kunakitu kinatembea toka kifuani hadi mgongoni.
Hali hii ilikuja kutulia baada ya nusu saa.
Leo amenipigia tena simu ila nilisikia tu akihema kwa sauti ya juu bila ya kuongea chochote. Nimewahi na nimekuta analia kwa sauti ya chini,huku akilalama mbavu zinambana. Alikuwa hawezi kuinuka ila nilifankisha kumpandisha kwenye pikipiki hadi hospitali ya Rufaa ya Songea mjini.

Tumeenda kwa daktari na akashauri tukachukue kipimo cha X ray ila kwa ushauri wa mgonjwa kasema amewahi kupimwa mbavu na maumivu ya uti wa mgongo kwa X ray ila hakukuwa na injury yoyote.

Anasema awali alipimwa aliambiwa ana UTI sugu na kuna dawa aliambiwa atumie. Vipimo hivi walivichukua Tanga na aliandikiwa dawa na sindano. Gynazol tb ni dawa aliyoandikiwa ila sindano hatujui Kwa kuwa kadi yake ameiacha Tanga kwa kuisahau.
Hali hii inamtokea wakati hata akisukumwa kidogo tu.
Naomba msaada wenu
Ahsanteni
 
Bila shaka anatatizo la mfumo wa upumuaji akipata dawa ya asili inayoitwa lungwort. Kama uko moshi tembelea Luu Genesis Herb watakusaidia
 
Mpe pole, huenda akahitaji kuonwa pia na psychologist/psychiatrist kutokana na uchache wa dalili ulizotaja, pia unaweza kutujuza kuhusu kutoka jasho sana, mapigo ya moyo kwenda kasi, hofu kubwa na dalili zingine zinazoambatana.

Jaribu kueleza kwa kina pia kuhusu maisha yake kiujumla yaani kijamii, kiuchumi, afya yake kiujumla huko nyuma

It's GAD vs Panic attack.
 
Back
Top Bottom