Melki the Storyteller
JF-Expert Member
- May 3, 2022
- 5,699
- 9,777
Ni watoto wa baba mmoja ila mama tofauti, yeye ni kutoka kwa mama ambaye ni mke mkubwa wa baba yangu. Na mimi ni mtoto wa mke mdogo. Tunazidiana miezi miwili
Lakini ni miezi miwili sasa dada yangu kabadilika ghafla. Kwa mara ya kwanza tulikuwa sebuleni mida ya usiku tunaangalia taarifa ya habari muda huo nachat na my babè huku natabasamu, ghafla akaniuliza "unachat na nani anayekupa raha kiasi hicho?" nikatikisa kichwa kuonesha kukataa. Dakika chache nikaenda kukojoa. Niliporejea namkuta kashika simu yangu anasoma sms, ile kumnyang'anya akatia ugumu akakimbia nayo chumbani kwake.
Kesho yake mida ya saa 12 jioni wakati tumekaa sebuleni muda huo umeme umekatika akachukua simu yake na kumpigia babè, kumbe alichukua namba yake, na kuanza kuzungumza naye kunihusu mimi kama marafiki vile, huku kaweka loudspeaker na kucheka sana.
Wiki moja baadae, huyo babè kanipigia na kunambia kuwa dada yangu anamtukana sana na kusema aachane na mimi, ndipo kwa hasira nikamfuata na kumkalipia, dakika chache baadae nilimkuta kitchen akiwa analia.
Nowdays nikitaka kutoka out, anapatwa na ganzi, kitete, wasiwasi kisha kuuliza unaenda wapi? mara "twende wote", keshaninunulia fulana na raba za kutosha humu ndani. Nikiongea na simu nisipokuwa makini ataninyakua na kuzungumza nayo. Kuna kipindi aliingia chumbani kwangu ghafla akiwa kajifunga khanga mida ya asubuhi na kudai kuwa kajisahau ana mawazo mengi kisha kuondoka!
Tatizo hasa litakuwa ni lipi wanajukwaa?