Dada yake Joshua Nassari avuliwa udiwani, Wabunge 7 wapendekezwa kuvuliwa nyadhifa za kwenye chama

MLETA MADA KWA TAARIFA YAKO NI KUWA NASSARY NI UKOO MKUBWA KULE MERU, KWAHIYO USISHANGAE KUWA HATA HAWANA UNDUGU WALA NASABA NA JOSHUA NASSARI
 
Naam mambo yameiva!

Kamati ya utendaji ya Chadema Kanda ya Kaskazini imemvua uanachama diwani wa Viti Maalum wa chama hicho, Digna Nassari kwa makosa ya kinidhamu.

Arusha. Kamati ya utendaji ya Chadema Kanda ya Kaskazini imemvua uanachama diwani wa Viti Maalum wa chama hicho, Digna Nassari kwa makosa ya kinidhamu.

Kamati hiyo pia imependekeza Meya mmoja wa jiji anayetokana na chama hicho kuvuliwa uanachama kutokana na makosa ya kinidhamu na usaliti.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumanne Mei 21, 2019, katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Aman Golugwa amesema uamuzi huo umetolewa katika kikao cha kamati hiyo kilichofanyika Mei 18, 2019.

Amesema tayari uamuzi huo umepelekwa ngazi za juu za chama hicho sambamba na hatua za kinidhamu kwa wabunge saba.

Amebainisha kuwa kikao hicho kiliongozwa na Kaimu mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Joseph Selasini ambaye ni mbunge wa Rombo.

Chanzo: Mwananchi
Digna Nassari diwani viti maalumu na dada wa mbunge.

Sasa hii ingekuwa CCM ungeshasikia siku nyingi kuwa upendeleo na undungu. Hawa jamaa mimi huwa siwaelewi akili zao zimejaaa vitu gani. Nahisi huwaza kwa masaburi.

Kipindi kile Lissu alipiga kelele watendaji wengi kutoka kanda ya Ziwa na Magaharibi. Wakati huo huo anasahau yeye Lissu ni kiongozi Chadema na Mbunge na dada Lucy Luhwenya RIP akiwa mbunge viti maalumu. Huu ni upumbavuu wa hali ya juu. Wakifanya wao ni sawa lakini wakifanya CCM ni dhambi. Sawa na viti maalumu vingi Chadema ni Wachaga na sidhani hiki ikiwa na ajali.
 
Muwe mna ufahamu kuhusu jambo ndo post, lini Lucy Owenya kawa dada wa Lissu?.Buku 7 Work
 
Kuna watu mnaongea ongea tu bila ya kuwa na ushahidi, Hivi nikikuuliza ulete ushahidi wa nepotism ndani ya chadema, utaweza leta? Na hiyo nepotism haipo vyama vingine?

Muache kutufuatilia fanyeni mambo yenu.
sawa.. sisi tunaacha kufuatilia mambo yenu. na ninyi msije kutuomba kura. ha ha ha ha..... yaani ka umepanic vile
 
Nepotism imetawala sana Chadema siku ikitawala nchi hii tutegemee mababu na mabibi watapewa nyadhifa kubwa serikalini
Baba :Jakaya M Kikwete Rais mstaafu
Mama: Salama kikwete Mbunge viti maalumu (Former First lady)
Mtoto: Ridhiwan kikwete mbunge wa kuchaguliwa
Hii tuiiteje??
 
Chadema mlitakiwa msiwe na mfumo wa nepotism kama CCM ili muonyeshe mfano
naam! hilo ndo neno la msingi. ili kina sie tusiopenda nepotism tupate pa kukimbilia. sasa huku na kule mambo yale yale, twende wapi? mnaboa sana
 
Baba :Jakaya M Kikwete Rais mstaafu
Mama: Salama kikwete Mbunge viti maalumu (Former First lady)
Mtoto: Ridhiwan kikwete mbunge wa kuchaguliwa
Hii tuiiteje??
yote yale yale.. yaan ccm=cdm=ccm=cdm.... ndo tunasubiri mje kutwambia tuwachague ninyi badala ya ccm. tutawauliza kwa nini ninyi na sio ccm, hamtakuwa na la kusema sababu wote ni wale wale.
 
Chadema ilishafeli kuwa mfano bora! Kila jambo ukiuliza wao wanarukia reference ya MaCCM! Tunahitaji kurenew upinzani wa nchi hii! Sio huu mara ushabikie Lowasa mara Membe! Nape akiongea wanashangilia! Wapo wapo tu!
Zinazoshabikiwa ni hoja siyo mtu na ni vema kama kijana ukajikita katika hilo. Nape ,Bashe au Membe akiongea point ana haki kuungwa mkono na akiongea upumbavu ana haki ya kukosolewa tatizo ni kuwafanya maadui wote wanaoupinga ubadhilifu katika serikali hii..
 
yote yale yale.. yaan ccm=cdm=ccm=cdm.... ndo tunasubiri mje kutwambia tuwachague ninyi badala ya ccm. tutawauliza kwa nini ninyi na sio ccm, hamtakuwa na la kusema sababu wote ni wale wale.
Je ni haki kuchukua asiye na sifa eti kwa kuogopa kwamba ndugu kupata nafasi ni nepotism afu tuchukue mazumbukuku ili tu kubalance kwa mfumo wa undugu. Ni vema tukajikita katika kuupinga udhaifu wao kwa kuonesha kwamba kulikuwa na mwenye ubora na si kupinga kwa makelele ili hali aliyepo anafanya kazi. Aliyeondolewa kaondolewa si kama ndugu yake na Nassari bali kutokana na udhaifu wake vivyo hivyo hakuwekwa katika nafasi kutokana na undugu na Nassari bali uhodari wake. Tunachotakiwa kukubaliana ni kwamba kiwango kina kupanda na kushuka na kwa kuwa kimeshuka below cuttoff point kwahiyo hakukuwa na budi kupisha wengine
 
Chadema ilishafeli kuwa mfano bora! Kila jambo ukiuliza wao wanarukia reference ya MaCCM! Tunahitaji kurenew upinzani wa nchi hii! Sio huu mara ushabikie Lowasa mara Membe! Nape akiongea wanashangilia! Wapo wapo tu!
You need to know siasa is driven by Sera. It is not about particular individual. Kama kuna watu whether wako CCM au ACT, as long as wanatetea maslahi ya nchi hilo ndilo la msingi.
 
Kwahiyo kaka mbunge dada diwani? Hiiiiiiiiiiiiiii acha nicheke kijiwe jiwe

Mbona hushangai kuna rais alieteuwa mtoto wa dada kuwa paymaster general, na watoto wa dada zake lundo kwenye ukurugenzi na mchepuko wake kuwa waziri?
 
Back
Top Bottom