Dada yake Joshua Nassari avuliwa udiwani, Wabunge 7 wapendekezwa kuvuliwa nyadhifa za kwenye chama

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
15,099
2,000
Naam mambo yameiva!

Kamati ya utendaji ya Chadema Kanda ya Kaskazini imemvua uanachama diwani wa Viti Maalum wa chama hicho, Digna Nassari kwa makosa ya kinidhamu.

Arusha. Kamati ya utendaji ya Chadema Kanda ya Kaskazini imemvua uanachama diwani wa Viti Maalum wa chama hicho, Digna Nassari kwa makosa ya kinidhamu.

Kamati hiyo pia imependekeza Meya mmoja wa jiji anayetokana na chama hicho kuvuliwa uanachama kutokana na makosa ya kinidhamu na usaliti.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumanne Mei 21, 2019, katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Aman Golugwa amesema uamuzi huo umetolewa katika kikao cha kamati hiyo kilichofanyika Mei 18, 2019.

Amesema tayari uamuzi huo umepelekwa ngazi za juu za chama hicho sambamba na hatua za kinidhamu kwa wabunge saba.

Amebainisha kuwa kikao hicho kiliongozwa na Kaimu mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Joseph Selasini ambaye ni mbunge wa Rombo.

Chanzo: Mwananchi
 
mangatara

JF-Expert Member
Jul 6, 2012
14,403
2,000
Nepotism imetawala sana Chadema siku ikitawala nchi hii tutegemee mababu na mabibi watapewa nyadhifa kubwa serikalini
Nilikuwa napita mahali flani leo nikausikia ule wimbo wa injili wa zamani kidogo ukiimbwa; Toa kwanza boriti kwenye jicho lako, ndipo utaona kibanzi kwenye jicho la mwenzako'
Kuna chama kimoja kikubwa tu tena mahiri, tena chama kongwe. Leo hii bungeni Mtoto ni mbunge na Mama mbunge wa kuteuliwa. Sasa sijui nepotisim inakuwa CDM tuu au?
Mbona wengine baba kafariki mnawapa ubunge wa baba yao au nepotisim huko haiko?? Pole sana
 
Bowie

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
3,976

Chadema mlitakiwa msiwe na mfumo wa nepotism kama CCM ili muonyeshe mfano
 
shinyangakwetu

JF-Expert Member
Jun 25, 2015
1,710
2,000
Naam mambo yameiva!

Kamati ya utendaji ya Chadema Kanda ya Kaskazini imemvua uanachama diwani wa Viti Maalum wa chama hicho, Digna Nassari kwa makosa ya kinidhamu.

Arusha. Kamati ya utendaji ya Chadema Kanda ya Kaskazini imemvua uanachama diwani wa Viti Maalum wa chama hicho, Digna Nassari kwa makosa ya kinidhamu.

Kamati hiyo pia imependekeza Meya mmoja wa jiji anayetokana na chama hicho kuvuliwa uanachama kutokana na makosa ya kinidhamu na usaliti.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumanne Mei 21, 2019, katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Aman Golugwa amesema uamuzi huo umetolewa katika kikao cha kamati hiyo kilichofanyika Mei 18, 2019.

Amesema tayari uamuzi huo umepelekwa ngazi za juu za chama hicho sambamba na hatua za kinidhamu kwa wabunge saba.

Amebainisha kuwa kikao hicho kiliongozwa na Kaimu mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Joseph Selasini ambaye ni mbunge wa Rombo.

Chanzo: Mwananchi
We unafanywa ujinga, kama mtu ni msaliti aachwe aue chama, mbn huko lumumba kila uchao watu wanatumbuliwa nako kuna chuki???
 
mangatara

JF-Expert Member
Jul 6, 2012
14,403
2,000
Chadema mlitakiwa msiwe na mfumo wa nepotism kama CCM ili muonyeshe mfano
Ila hao waliochaguliwa hawakustahili hizo nafasi?? Asingelitumbuliwa mngelijua lini kuwa Nassari alikuwa na dadake aliyekuwa diwani?? Acheni hizo mambo za kipuuzi. Aliye karibu na kama ni mchacharikaji kwa ajili ya chama apewe nafasi bila ubaguzi
 
Jackal

JF-Expert Member
Apr 10, 2012
5,723
2,000
Halali Nasari ni jina la ukoo wa kimeru kama ilivyo Mollel Kwa wamasai. Unauhakika gani kama huyo ni Dada yake na Nasari?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom