Dada wa kazi za ndani afukuzwa na mdogo wa bosi wake kisa kudai mshahara wake

Kanungila Karim

Verified Member
Apr 29, 2016
16,603
2,000
REHEMA Ezekiel, mkazi wa Sinza- Mugabe jijini Dar ni msaidizi wa kazi za ndani (hausigeli) ambaye yamemfika mazito baada ya kutimuliwa ndani ya nyumba na mdogo wa bosi wake aliyefahamika kwa jina la Mama Rose, kisa kumdai mshahara, habari hii ni fundisho kwa wengine.

Kwa mujibu wa Rehema, alifikwa na mazito hayo baada ya kudai mshahara wake huo wa mwezi mmoja wa shilingi elfu hamsini na kujikuta hana pa kwenda kisha kubaki akirandaranda mitaani.

Tukio hilo lilijiri hivi karibuni ambapo Rehema alipewa shilingi elfu ishirini kisha kutupiwa begi lake la nguo na kuambiwa aondoke.

Akizungumza huku akiwa nje ya nyumba hiyo ya bosi wake maeneo hayo ya Sinza-Mugabe, Rehema aliliambia gazeti hili kuwa alitinga jijini Dar akitokea Pangani jijini Tanga kwa ajili ya kufanya kazi za ndani na amefanya kwa takriban miezi miwili na kulipwa shilingi elfu hamsini tu.

“Nilikuja hapa (Dar) kwa ajili ya kufanya kazi za ndani kwa dada mmoja anaitwa Mama Rose, lakini nina miezi miwili nyumbani kwake na tulikubaliana kila mwezi atakuwa ananilipa shilingi elfu hamsini, lakini amenilipa shilingi elfu 30 mara ya kwanza.

“Mimi nilipoona sipewi kile tulichokubaliana, ilibidi nimuage bosi wangu kwamba nahitaji kuondoka nirudi nyumbani kwa hiyo namuomba hela zangu zote, lakini kwa kipindi hiki yeye amesafiri nipo mdogo wake. Huyo mdogo wake alinipa shilingi elfu ishirini na kunifukuza, akiniambia niondoke.

“Nilimwambia nitaondokaje wakati bado nadai hela ya mwezi mzima? Akanipa shilingi elfu ishirini na kuniambia niondoke.

“Nilipomkatalia hadi nilipwe hela yangu yote ndipo akanitupia begi langu na kufunga mlango. Nilikaa uani hadi saa tisa usiku ndipo akanifungulia, nikaingia ndani kulala, akaniambia ikifika saa kumi na mbili alfajiri hataki kuniona.

“Mimi nilimwambia anipe hela zangu niondoke, lakini hakunipa hivyo ninashindwa kuondoka kwani elfu ishirini aliyonipa haiwezi ikanifikisha Pangani.

“Ilibidi niende Kituo cha Polisi cha Kijitonyama (Mabatini), nikaambiwa nirudi kwa mjumbe ili nimueleze tatizo langu.

“Kwa hiyo mpaka mpaka sasa sijajua nini cha kufanya kwa kuwa hii hela haitoshi hata nauli na sina pa kwenda,” alisema Rehema akiangua kilio asijue wapi pa kwenda.

Habari hii ni fundisho kwa wadada wanaotafuta kazi za ndani na kwa wazazi wanaoruhusu watoto wao waende mjini bila kujua huko waendako wataenda kuishije.
 
  • Thanks
Reactions: cmp

tozi25

JF-Expert Member
Aug 29, 2015
5,958
2,000
Halafu unashangaa wakoloni waliwezaje kuwafanya watu watumwa? Mama Rose mpatie Rehema haki yake kabla fimbo ya Mungu haijakufika.

Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Zogwale

JF-Expert Member
Jul 10, 2008
13,006
2,000
Ila pia wako mabinti mtambo. Kazi yake ni kuhama nyumba baada ya MWEZI au mwili. Ikizidi mitatu. Kazi itakuwa kukusanya Nauli tu. Na huwa wana kabisa watu wao wanaowatafutia kazi wakipata unaambiwa anatokea Tanga ndani huko tunahitaji 50,000 kumleta DSM. Ni kuomba Mungu tu.

Wengine ni network ya majambazi pia au wao wenyewe ni wezi. Wanaiba wanapeleka kwao Kijijini. Akifika huko wanaanza mchakato upya kurudi mjini na anabadili Mkoa.

Ni kumuomba Mungu akupe binti wa uhakika.

Ila pia wako boss wanyanyasaji mno mpaka chakula wanapewa tofauti au kusimangiwa.
 
Mine eyes

JF-Expert Member
Apr 11, 2016
5,309
2,000
Ila pia wako mabinti mambo. Kazi yake ni kuhama nyumba baada ya MWEZI au mwili. Ikizidi mitatu. Kazi itakuwa kukusanya Nauli tu. Na huwa wana kabisa watu wao wanaowatafutia kazi wakipata unaambiwa anatokea Tanga ndani huko tunahitaji 50,000 kumleta DSM. Ni kuomba Mungu tu.

Siku hizi madada wengi wa kazi ...
waangalie mara nne kabla ya kuwaajiri!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
SeliSelina

JF-Expert Member
Jun 27, 2014
216
500
KESI HII INGEKUWA IMETOKEZEA NCHI ZA KIARABU, NAONA KURASA ZINGEJAA SANA TUU JAMIIFORUM, KWA KULAANI, KUAPIZA, KUTUKANA, KUSEMA KILA YA AINA YA KASHFA.
ILA KWA VILE IMETOKEA DAR ES SALAAM, TANZANIA. BASI IMEKUWA INACHUKULIA KAMA KAWAIDA TUU.
TUWE NA MISIMAMO KWA JAMBO LOLOTE LINAPOTOKEZEA PAHALI POPOTE.
 
Kilele9

JF-Expert Member
Jun 1, 2017
1,147

Mama Rose ni mwenzetu usifananishe na hao Waarabu wako
 
Fall Army Worm

JF-Expert Member
Jan 8, 2015
8,027
2,000
KESI HII INGEKUWA IMETOKEZEA NCHI ZA KIARABU, NAONA KURASA ZINGEJAA SANA TUU JAMIIFORUM, KWA KULAANI, KUAPIZA, KUTUKANA, KUSEMA KILA YA AINA YA KASHFA.
ILA KWA VILE IMETOKEA DAR ES SALAAM, TANZANIA. BASI IMEKUWA INACHUKULIA KAMA KAWAIDA TUU.
TUWE NA MISIMAMO KWA JAMBO LOLOTE LINAPOTOKEZEA PAHALI POPOTE.
Ninyi Waarabu ni wakatili sana, msingeishia kumnyima haki yake tu!!!,Bali mngeweza hata kumfanyia unyama mwingine. Huo ndio Ukweli na Ukweli unauma. Na uwaume.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
IROKOS

JF-Expert Member
Aug 13, 2011
8,588
2,000
As long as kafanya kazi ampe haki yake amwache aende zake.
Ila pia wako mabinti mambo. Kazi yake ni kuhama nyumba baada ya MWEZI au mwili. Ikizidi mitatu. Kazi itakuwa kukusanya Nauli tu. Na huwa wana kabisa watu wao wanaowatafutia kazi wakipata unaambiwa anatokea Tanga ndani huko tunahitaji 50,000 kumleta DSM. Ni kuomba Mungu tu.

Wengine ni network ya majambazi pia au wao wenyewe ni wezi. Wanaiba wanapeleka kwao Kijijini. Akifika huko wanaanza mchakato upya kurudi mjini na anabadili Mkoa.

Ni kumuomba Mungu akupe binti wa uhakika.

Ila pia wako boss wanyanyasaji mno mpaka chakula wanapewa tofauti au kusimangiwa.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chrisvern

JF-Expert Member
Sep 8, 2011
2,306
2,000
REHEMA Ezekiel, mkazi wa Sinza- Mugabe jijini Dar ni msaidizi wa kazi za ndani (hausigeli) ambaye yamemfika mazito baada ya kutimuliwa ndani ya nyumba na mdogo wa bosi wake aliyefahamika kwa jina la Mama Rose, kisa kumdai mshahara, habari hii ni fundisho kwa wengine.

Kwa mujibu wa Rehema, alifikwa na mazito hayo baada ya kudai mshahara wake huo wa mwezi mmoja wa shilingi elfu hamsini na kujikuta hana pa kwenda kisha kubaki akirandaranda mitaani.

Tukio hilo lilijiri hivi karibuni ambapo Rehema alipewa shilingi elfu ishirini kisha kutupiwa begi lake la nguo na kuambiwa aondoke.

Akizungumza huku akiwa nje ya nyumba hiyo ya bosi wake maeneo hayo ya Sinza-Mugabe, Rehema aliliambia gazeti hili kuwa alitinga jijini Dar akitokea Pangani jijini Tanga kwa ajili ya kufanya kazi za ndani na amefanya kwa takriban miezi miwili na kulipwa shilingi elfu hamsini tu.

“Nilikuja hapa (Dar) kwa ajili ya kufanya kazi za ndani kwa dada mmoja anaitwa Mama Rose, lakini nina miezi miwili nyumbani kwake na tulikubaliana kila mwezi atakuwa ananilipa shilingi elfu hamsini, lakini amenilipa shilingi elfu 30 mara ya kwanza.

“Mimi nilipoona sipewi kile tulichokubaliana, ilibidi nimuage bosi wangu kwamba nahitaji kuondoka nirudi nyumbani kwa hiyo namuomba hela zangu zote, lakini kwa kipindi hiki yeye amesafiri nipo mdogo wake. Huyo mdogo wake alinipa shilingi elfu ishirini na kunifukuza, akiniambia niondoke.

“Nilimwambia nitaondokaje wakati bado nadai hela ya mwezi mzima? Akanipa shilingi elfu ishirini na kuniambia niondoke.

“Nilipomkatalia hadi nilipwe hela yangu yote ndipo akanitupia begi langu na kufunga mlango. Nilikaa uani hadi saa tisa usiku ndipo akanifungulia, nikaingia ndani kulala, akaniambia ikifika saa kumi na mbili alfajiri hataki kuniona.

“Mimi nilimwambia anipe hela zangu niondoke, lakini hakunipa hivyo ninashindwa kuondoka kwani elfu ishirini aliyonipa haiwezi ikanifikisha Pangani.

“Ilibidi niende Kituo cha Polisi cha Kijitonyama (Mabatini), nikaambiwa nirudi kwa mjumbe ili nimueleze tatizo langu.

“Kwa hiyo mpaka mpaka sasa sijajua nini cha kufanya kwa kuwa hii hela haitoshi hata nauli na sina pa kwenda,” alisema Rehema akiangua kilio asijue wapi pa kwenda.

Habari hii ni fundisho kwa wadada wanaotafuta kazi za ndani na kwa wazazi wanaoruhusu watoto wao waende mjini bila kujua huko waendako wataenda kuishije.
Mbona wanaotuhumiwa kufanya dhuluma hata hawajahojiwa??
Waandishi wa siku hizi kazi ipo!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom