Dada wa kazi: Mfanyakazi pekee yake ambaye akitangaza kuacha kazi bosi anatetemeka wengine tuliobaki wala

Kheri ya siku ya waajiriwa duniani lakini kwa hali ilivyo ni dada wa kazi tu ambaye akitangaza anaacaha kazi bosi anatetemeka wengine waliobaki wala
Hoja yenye mashiko hasa kwa kipindi hiki cha kuhemea ajira katika nchi yetu.
Ila Mungu anatupenda watanzania tutavuka
 
Huoni kama tayari ushatetemeka?...
Labda unatetemeka wewe,kwetu watoto wanapelekwa kwa bibi,dada anapewa chake aondoke.

Msiwanyenyekee sana wadada wa kazi,kama unamlipa vizuri atakuheshimu na atakwambia mapema siku ya kuondoka ila kama unamlipa vibaya atakuendesha atakua anatest mitambo ya kila aina huku akikutesea wanao vibaya mno
 
Hawa watu ni wa muhimu sana. Ndio ajira pekee iliyobakia ambayo mwajiri anampetimpeti mwajiriwa ili adumu muda mrefu na kukaa vyema na watoto.
 
Omba sana usipate HG kutoka Dodoma au Singida, ni washirikina sijapata kuona!
 
Mimi walinisumbua baada ya watoto kukua kidogo .Nina miaka mingi sina msichana wa kazi .Watoto wangu.niliwafundisha kujitegemea tangu wanamiaka saba mpaka sasa wengine wako chuo na sasa nimebaki na mzee tu hatuna dada.Tulichoamua ni kuhakikisha tuna vifaa vya kutusaidia urahisishaji wa kupika kama gas,pressure cooker nk ,kwenye kufua nk.Upande wa usafi tunafanya wenyewe na mara moja.kwa.mwezi tunatafuta mtu wakutufanyia usafi nje tu kwenye bustani.Yaani mimi binafsi nimeona raha sana no pressure ,tumepunguza garama sana na uzuri kwa mwaka jana nilikiwa nafanyia kazi nyumbani. Ila tuache uvivu ,watanzania tunapenda kujiendekeza na kuwaachia wadada sijui .Nikienda kwa mashoga zangu uko nje wanawatoto watatu na hawajawahi kuwa sijui na wadada.Dar wamama niwabivu sana aisee
 
Back
Top Bottom