Dada wa kazi anajua ratiba zangu kuliko Mke wangu!

Sir John Roberts

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
9,558
15,897
Habari za weekend!

Kama ilivyoa ada. Mimi ni mtu mzima kiasi nina mke na watoto wawili. Nyumbani mke wangu anajituma si kwamba ni mvivu la hasha. Anafanya mambo yote kama mke. Lakini kuna jambo moja linanishangaza, hivi karibuni tumepata msichana wa kazi hana muda mrefu ni kama miezi miwili lakini tangu amefika nimeona mabadiliko ya ghafla sana.

1. Haambiwi kitu huwa anafanya kabla hujamuuliza mf. nimezoea kumwambia mke wangu nitayarishie maji ya kuoga. Yeye kabla hujasema unakuta tayari ameshaandaa.

2. Hasubiri nimwambie nataka chai au chakula nikitoka tuu kama ni asubuhi tayari ameshaniandalia chai mezani hivyo hivyo nikirudi nyumbani ananiwekea chakula mezani. Mke wangu mpaka nimwambie. Nimeona tofauti kubwa sana ya mkewangu na huyu dada wa kazi.

Ni hayo tuu.
 
Jinsi tulivyo tukiamua kuchepuka hua tunatafuta vijisababu vidogo vidogo ili tuchepuke.

Sasa mtu kujua kuandaa chai au maji ya kuoga ni swala? Si ndiyo kilichomleta hapo?

Nimeishi na wadada wa kazi pia. Huo ni moto wa mwanzoni mwanzoni kuna mmoja alikua anaamka saa kumi alfajiri yaani nikiamka saa 12 nakuta usafi na chai tayari ni kwenda kutafuta vitafunwa tu.

Baadaye akawa miyeyusho
 
Ili wanaume muda mwingine tuna matatizo. Mfanyakazi kaletwa kuja kutimiza ayo majukumu ambayo uliona mke wako kipenzi yanamchosha na kumuwia ugumu.

Mkuu swala la kuandaliwa maji ya kuoga ni mambo ya kawaida ata kupakuliwa chakula ni maswala ya kawaida. Ata leo useme umuoe huyo utarudi humu kulalamika mke wangu mpya kabadirika na beki 3 anatimiza majukumu yake.

Ufunge na wewe Ata shower kupelekea maji bafuni sio kipimo cha upendo
 
Unatumia kinywaji gani mkuu, nikununulie jioni
 
Back
Top Bottom