Dada wa kazi adaiwa kummwagia mafuta ya moto mtoto wa miaka 5 kisha baba wa mtoto amtorosha mtuhumiwa

Inalipa

Member
Jun 30, 2022
63
77
Kibaha Pwani,

Binti wa miaka 14 ambaye anafahamika kama binti wa kazi amemwagia Mafuta ya kula ya Moto mtoto wa chekechekea mwenye umri wa miaka 5.

Baba mzazi wa mtoto anashikiliwa na polisi kwa kumtorosha mtuhumiwa.


=========

Mtoto wa kike (5) mkazi wa Soga wilayani Kibaha mkoani Pwani ambaye jina lake limehifadhiwa, amejeruhiwa vibaya na mfanyakaz wa ndani aliyejuljkana kama Rehema baada ya kumwagiwa mafuta ya moto sehemu mbalimbal za mwili wake na kisha mtuhumiwa huyo kutoroka kusikojulikana.

Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani Gregory Mushi, na kusema mtuhumiwa huyo alitenda jinai hyo majira ya saa 11:00 alfajiri na baada ya kutenda tukio hilo alifanikiwa kukimbia akipewa msaada wa baba mzazi wa mtoto huyo na kukimbilia kusikojulikana.

Hata hivyo jeshi la polisi limefanikiwa kumkamata baba mzazi wa mtoto huyo kwa kosa la kumtorosha mtu aliyemjeruhi mtoto wake.
 
Baba wa mtoto amemtorosha mtuhumiwa?

Juzi hapa huko Njombe jamaa alimbaka mama yake mzazi kisha baba yake mzazi akamuwekea dhamana na baadae mtuhumiwa akakimbia.

Matukio ya ajabu ajabu yanaongezeka kila siku.
 
Back
Top Bottom