Dada Shirima wa ustawi wa jamii makao makuu DSM unawakosesha watoto familia

Nov 15, 2017
12
45
Habari wana JF,

Kuna dada anaitwa Shirima yupo makao makuu pale Dsm ofisi zao zipo pale Kivukoni nyuma ya ghorofa la utumishi.

Huyu dada amekuwa mwiba kwa wale ambao wameshindwa kupata mtoto na kuamua KUASILI(ADOPTION)kama umeshawahi kufuatilia KUASILI MTOTO lazima utakuwa unajua hekaheka za huyu dada.

Mimi nimefatilia hili swala la kuasili mtoto toka 2015 mpaka leo bado sijafanikiwa huyu dada mara uje uambiwe faili lako limepotea.

Mara uambiwe documents zingine hazionekani yaani full matatizo sasa unauliza mbona sijafahamishwa kuwa faili langu limepotea au kuna documents hakuna wakati mawasiliano yangu mnayo ? Na kila ukipiga simu kuulizia unaambiwa lipo kwenye process,

Jibu utakolopewa hapo kama una roho ndogo unaweza kumpiga huyu dada, sijapata kuona dada anafanyakazi ofisi ya serikali jeuri kama huyu,huyu dada amesababisha watu wengi sana kughairi dakika za mwisho kuchukua watoto vituoni.

Mimi nimetembelea baadhi ya vituo kama Msimbazi, Mburahati, nia njema nk. Huko kote watoto wapo na kuna baadhi wana documents kabisa zinaonyesha wamepata familia na wametambuliwa mwaka mmoja nyumba lakini hawajaja kuchuliwa mpaka leo.

Tatizo huyu dada kwa sababu yeye ndo kiunganishi kati ya Kamishina na hizi ustawi za jamaii za wilaya yaani barua yoyote ya majibu au kutumwa kwa kamishina inayohusu kuasili mtoto lazima ipitie kwa huyu dada unaweza fuatilia huko kote labda imekuchukua miaka 2-3.

Vitu vyote vikapitishwa finaly ni ile barua ya polisi inayosibitisha mtoto uliemchagua hana wazazi au hakuna mtu anayemfutilia huko polisi barua hii polisi wakishaitoa inaletwa ustawi wilaya yako na Afisa wako anaipeleka kwa huyu dada ambako ndiko kwenye masijala na faili lako lilipo.

Huyu dada anatakiwa aitume hiyo barua kwa kamishina Dodoma kwa ajili ya kamishina kujilizisha kuwa huyo mtoto ulichagua hana tatizo hata ukipewa hapo ndipo watu hughairi dada atakusumbua eneo hili mpaka utashangaa mara kamishna hayupo, mara barua yako haionekani yaani full matatizo.

SERIKALI KUPITIA WIZARA HUSIKA HEBU TUPIENI JICHO KWA HUYU DADA ANAWAKOSESHA WATOTO WENGI MALEZI KWA WATU WANAOWAHITAJI, VITUO VINAELEMEWA MZIGO WA KUWALEA WATOTO WAKATI WAPO WATU WENYE UHITAJI NA WENYE VIGEZO KISHERIA
VILE VILE SERIKALI ANGALIENI
HILI SWALA LA KUASILI MTOTO KWA MTU ANAYEHITAJI LISICHUKUE MUDA MREFU KWA MTU ATAKAYETHIBITISHWA NA MAMLAKA HUSIKA KUWA ANAFAA.
 

Nyendeke

JF-Expert Member
Jul 21, 2013
1,398
2,000
Huyo Dada anacheo gani hapo? umejaribu kwenda ngazi za juu kwake ili kujaribu kupata ufumbuzi?
 

Consigliere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
11,539
2,000
Kwa hiyo kwake ni bora watoto watorokee mitaani na kuishia kuomba omba na kulala nje wakipigwa na jua na mvua huku wakila vyakula vya kuokoteza?
 

Numbisa

JF-Expert Member
Dec 12, 2016
176,996
2,000
Ungeandika jina lake lote atumbuliwe iwe fundisho kwa wengine wenye kulewa madaraka.
 

pangalashaba

JF-Expert Member
Jan 10, 2011
1,236
2,000
Kwa kuwa ushamchana hapa JF basi atajirekebisha au vinginevyo atatumbuliwa. Haiwezekani watu wajitolee kuchukua watoto yatima ili kwenda kuwapatia malezi bora then yeye awe kikwazo.
Hana muda mrefu huyo katika nafasi aliyonayo!!!! IF hata baba mwenye nyumba anapitaga.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom