Dada Regia Mtema naomba niendeleze ulipoishia

JoJiPoJi

JF-Expert Member
Aug 8, 2009
2,907
3,260
Salam ndugu zangu JF

Kwanza napenda nitumie fursa hii kumpongeza kwa dhati kabisa dada yetu Regia Mtema kwa kushiriki na kupambana hadi dakika ya mwisho kugombea ubunge katika jimbo la Kilombero kwa tiketi ya chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) na hakuna shaka bila kuwepo na uchakachuaji wa matokeo leo hii ungekuwa mbunge mteule wa jombo hilo, hongera sana.

Pili, kwa kuwa lengo letu sote kwa jamii ni kuleta maendeleo na hilo ndilo jukumu letu kama vijana wapenda mabadiliko sasa naomba nichukue fursa ya kukuomba niendeleze pale ulipoishia ili tuweze kulikomboa jimbo letu kutoka katika mikono ya chama cha mapinduzi ambacho tangu uhuru kimeshindwa kuleta maendeleo katika jimbo hili lililo na rasilimali nyingi kulinganisha na maeneo mengi katika nchi hii.

Jimbo la kilombero bado lina watu wengi ambao hawajui nini maana ya mabadiliko na hili ndio naona lililochangia sana tukapoteza hili jimbo, kwa mfano mdogo sehemu nyingi ambazo zina watu masikini sana wa elimu na hata kipato ndio mashabiki wakubwa wa ccm, ninaona sasa ni muda muafaka kabisa kuanza kuwa karibu nao na kuwaelimisha ninini madhara ya kuikumbatia ccm na faida ya kuachana nayo, hii ni pamoja na kufungua matawi mengi ili tupate wanachama wengi katika jimbo letu.

Hayo yote hayawezi kuwa kama sitapata ushirikiano na baraka kutoka kwako ambaye kwangu wewe ni zaidi ya mshindi.

Nichukue fursa hii tena na tena kukupongeza sana, kwa kuwa umeonyesha kwa namna gani ulivyo shujaa wa kupambana bila uwoga ili kuleta mapinduzi ya kweli kwa wana kilombero na tanzania kwa ujumla.

Nakutakia mapumziko mema baada ya kampeni ya muda mrefu,

JoJiPoJi

NAWASILISHA.
 
kwani aligombea na nani waccm na alipata kura ngapi na mpinzani wake alipata ngapi?
 
kwani aligombea na nani waccm na alipata kura ngapi na mpinzani wake alipata ngapi?
Aligombea na Abdul Mteketa wa CCM kwa kifupi tu mteketa ameshinda kwa msaada mkubwa wa wachakachuaji la sivyo angeshindwa vibaya
 
Gender Sensitive ananafasi ya kuwa mbunge wa viti maalum!! Itapendeza kama akiziba nafasi iliyoachwa katika ile list ya viti maalum baada ya Halima Mdee kushinda Kawe!!
 
Regia bado ana Nafasi ya kuliwakilisha lile Jimbo.Mgombea wa CCM kashinda kwa njia haramu,so kama atafungua case au hata wakaingia by election,basi the guy will be out.

Regia Mtema wa CHADEMA alipigana kufa na kupona kuliko hata wagombea wengine wanaume wazima.Jimbo la Kilombero anaweza kabisa kuliongoza kwa Mafanikio

Nawasilisha,and Iam out for today!
 
Yes,ulikuwa mpiganaji dada yetu.Asante kwa muda wako! RIP dada Regia Mtema!
 
Sio kwamba aligombea na Celina Kombani? Any way, that's not important nao, ila sasa namuonea wivu ameacha legacy, akiwa ameishi muda mfupi tu hapa duniani!!! Tumejifunza mengi kwa maisha yake. Raise on Regia Mtema!!!!!!!!!!!!!!
 
Sio kwamba aligombea na Celina Kombani? Any way, that's not important nao, ila sasa namuonea wivu ameacha legacy, akiwa ameishi muda mfupi tu hapa duniani!!! Tumejifunza mengi kwa maisha yake. Raise on Regia Mtema!!!!!!!!!!!!!!
Aligombea na Mteketa, Kombani ni mbunge wa mahenge ila alimsaidia sana mteketa kwenye kampeni japo bado walishindwa kama si kuchakachua.
 
Sina amani rohoni tangu nilipopata taarifa za msiba huu mzito.
Na sioni kama ni wakati mzuri wa kuzungumzia muhtahsari wa siasa za kilombero kwa sasa.
Mungiu aiweke roho ya dada regia mahali pema.
AMIN
 
Toka nilipopata taarifa ya msiba huu kiukweli nilijikuta machozi yanananitoka, Nlimpenda sana sana sana Regia Mtema kwa Moyo wangu wote binafsi nilikuwa na matarajio makubwa sana toka kwakwe kwa siasa za usoni, nikikumbuka alivyopambana kushinda jimbo la kilombero kwani alipata kura 43,500 hivi dhidi ya wa CCM 45,000

Mungu awatie moyo Ndugu ya wafiwa.
 
Back
Top Bottom