JoJiPoJi
JF-Expert Member
- Aug 8, 2009
- 2,929
- 3,331
Salam ndugu zangu JF
Kwanza napenda nitumie fursa hii kumpongeza kwa dhati kabisa dada yetu Regia Mtema kwa kushiriki na kupambana hadi dakika ya mwisho kugombea ubunge katika jimbo la Kilombero kwa tiketi ya chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) na hakuna shaka bila kuwepo na uchakachuaji wa matokeo leo hii ungekuwa mbunge mteule wa jombo hilo, hongera sana.
Pili, kwa kuwa lengo letu sote kwa jamii ni kuleta maendeleo na hilo ndilo jukumu letu kama vijana wapenda mabadiliko sasa naomba nichukue fursa ya kukuomba niendeleze pale ulipoishia ili tuweze kulikomboa jimbo letu kutoka katika mikono ya chama cha mapinduzi ambacho tangu uhuru kimeshindwa kuleta maendeleo katika jimbo hili lililo na rasilimali nyingi kulinganisha na maeneo mengi katika nchi hii.
Jimbo la kilombero bado lina watu wengi ambao hawajui nini maana ya mabadiliko na hili ndio naona lililochangia sana tukapoteza hili jimbo, kwa mfano mdogo sehemu nyingi ambazo zina watu masikini sana wa elimu na hata kipato ndio mashabiki wakubwa wa ccm, ninaona sasa ni muda muafaka kabisa kuanza kuwa karibu nao na kuwaelimisha ninini madhara ya kuikumbatia ccm na faida ya kuachana nayo, hii ni pamoja na kufungua matawi mengi ili tupate wanachama wengi katika jimbo letu.
Hayo yote hayawezi kuwa kama sitapata ushirikiano na baraka kutoka kwako ambaye kwangu wewe ni zaidi ya mshindi.
Nichukue fursa hii tena na tena kukupongeza sana, kwa kuwa umeonyesha kwa namna gani ulivyo shujaa wa kupambana bila uwoga ili kuleta mapinduzi ya kweli kwa wana kilombero na tanzania kwa ujumla.
Nakutakia mapumziko mema baada ya kampeni ya muda mrefu,
JoJiPoJi
NAWASILISHA.