Ufunguo
JF-Expert Member
- Aug 18, 2012
- 330
- 231
Nilikuwa na mpezi hapo nyuma ila baadae yeye alikosa uvumilivu na kuamua kuolewa na mtu mwingine. Sasa ni mwaka mmoja tanu aolewe na mimi niko katika mchakato wa ndoa japo mchumba wangu nae alikuwa na tatizo kidogo lakini naamini we will get along ASAP. Sasa huyu mpeenzi wangu wa zamani amekuwa kero kwangu, mpaka sasa ninataka nimweleze mme wake maana nimeshawaambia rafiki zake na huyu dada wamwonye kuhusiana na tabia hii lakini hataki kusikia. Kila mara ananiandikia text msg kudai eti tangu ameolewa na mme wake hapati raha ya ndoa kama tulivyokuwa pamoja na anataka angalau niwe nampa penzi hata mara moja kwa mwezi. Nimeshamwonya na kumwambia siwezi kufanya tendo hilo na kwasasa namheshimu kama mke wa mtu na pia nami najiandaa kuwa na familia na nataka kulinda heshima ya ndoa yangu. Siku moja nilimwambia kama ataendelea kunitumia msg za mapenzi na kunipigia simu za kunililia ntamwambia mmewe ila naona wala hajali kabisa. Sina mazoea na mme wake kabisa na wala sijawahi kukaa nae au kupiga nae stori. Sasa wana JF nimfikishie vipi ujumbe huu mme wake?.