Dada anataka kuwania ubunge jimbo la temeke, mna ushauri gani?

Dada mwenyewe nani kwanza? Watu wasije kuruka majivu na kukanyaga moto bure.
 
Tusimtoe kwa kashfa tumtoe kwa hoja!!! haya alete CV yake kwanza
 
Haya ndiyo mamabo ya kanyaboya za kuuziana mbuzi ndani ya gunia sasa.
 
Sasa ushauri unaweza kutegemea na dada ni nani, kuna mashauri tofauti kwa watu tofauti.

nimeshakupa profile yake kidogo, dada ni moja wa ma sista du wa town, anajulikana mijini. ila ni mke wa mtu na ni msomi vile vile ana miaka 33
 
Kama anataka kuanza kampeni sasa hivi ajitaje, otherwise asubiri mpaka muda atakaoweza kujitaja.

Ukiendeleza kutaka ku gauge vitu bila kutaja jina ndiyo biashara kanyaboya, na utakuwa humtendei haki hata huyo dada.

Kama kweli ni mtu mwenye uwezo watu watampa ushauri mzuri tu, kama ni mtu wa kuganga tutaona.

Mwambie aje hapa aandike kitu kuhusu the vicious cycle of aid dependency and how to break it for starters. Akishindwa challenge hii hana jipya.
 
Lengo nini,? CCM tulonao wanatutosha na kutuchosha nilifikiri atapitia upinzani vinginevyo kama ana kazi mwambie aendelee na kazi yake aachane na siasa. Na we mtazamo wako ni aje au ndo mwenyewe nini?
 
nimeshakupa profile yake kidogo, dada ni moja wa ma sista du wa town, anajulikana mijini. ila ni mke wa mtu na ni msomi vile vile ana miaka 33

Hiyo ndio shughuli yake kubwa inayomfanya ajulikane mjini?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom