Dada ambaye hujaolewa na kaka ambaye hujaoa, unakutana na changamoto zipi katika jamii yako?

Daah! Mimi dada zangu ndio vihelehele, ila mother anatetea kwa kuwa sijakuwepogo nchini miaka ile age mate wangu wengi wanaoa oa akidhani labda ningeshawishika kama ningekuwepo.

Age mate/marafiki wanauliza uliza,utasikia 32 years sasa.

Wengine uliopotezana nao muda mrefu uki meet nao, maswali yale yale nimeoa/kuolewa, nina watoto kadhaa.


Alexander The Great
 
Leo katika pita pita zangu kwenye mitandao nikakuta mtandao mmoja watu wanatokwa na mapovu si Me si Ke, ikabidi niulize kulikoni ndio naambiwa wamechoka kuulizwa "fulani utaolewa lini? Fulani utaoa lini? Daah! mpaka sasa huna mtoto umri unaenda, utazaa lini?"

Hasa wadada ndiyo wanaonesha wanashambuliwa sana na maswali ya utaolewa lini, utazaa lini?

Seriously jamii zetu za Kiafrica zina mambo ya kufatilia sana ishu za ndoa na kuzaa hivi hawajui wengine hawapendi tu kua committed na mtu, yaani ndivyo alivyo.

Mwingine anapenda a childless relationship; kelele za watoto kwake ni kero ingawa hawachukii watoto (Pediophobia).

Mwingine kubeba mimba na kuzaa anaogopa sana (Tokophobia) anahisi atakufa na yale mastory yao sijui mimba this uchungu that, anaona tobaaaa kifo kileee anakichungulia.

Wengine wanapenda vyote, ndoa na watoto, lakini hawajabahatika kupata wenza wa kuishi nao na kuanzisha familia.

Wengine wamejijua wana matatizo ya uzazi, labda tasa, anaamua kutokujiingiza kwenye ndoa kwa kuhofia kelele za mawifi za kujaza choo pia kumuumiza mwenzi wake pale atakapohitaji mtoto.

Sasa mtu kama huyu ukimwambia "haya kuolewa/kuoa hutaki basi zaa angalau katoto kamoja" anaumia na vile hawezi kukwambia hali yake.

Tuambie kama wewe unapitia changamoto hizo na unazikabili vipi.

Hapo pia kuna umaana sana.. all in all yote heri
 
Daah! Mimi dada zangu ndio vihelehele, ila mother anatetea kwa kuwa sijakuwepogo nchini miaka ile age mate wangu wengi wanaoa oa akidhani labda ningeshawishika kama ningekuwepo.

Age mate/marafiki wanauliza uliza,utasikia 32 years sasa.

Wengine uliopotezana nao muda mrefu uki meet nao, maswali yale yale nimeoa/kuolewa, nina watoto kadhaa.


Alexander The Great
mpango wa kuoa unao?

Hittin Blunts and Bustin Nuts
 
Mawazo ya wadada wengi hapa ni ya sikio la kufa;

Hebu miti izaayo mauwa na iwafunze maisha;

Ua haliwezi siku zote kubaki kama ua hata kama ukiendelea kulimwagilia maji na kutia mbolea muda utafika itabidi linyauke liwe tunda wenye kula matunda wale hatimae mtoto (mbegu) wazaliwe ili kuendeleza kizazi;

Thats a principle of nature! No one goes against it;

Wanaowauliza mna watoto au mtaolewa lini wanaona ni wakati wenu wa kuliwa na wanategemea mtoe matunda na mbegu ipatikane acheni ujinga they are very right,


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asee kuna the way nyuso za watu zinabadilika once nikiwajibu sijaolewa.
Mama yangu anapenda kuniforce ety niolewe ili nizae watoto watatu her argument is mwanamke akikaa kwenye nyumba yake she is a queen. . Nawaza hao watoto watatu atawalea yeye? Jee nikipata mume wa kunidunda, kunicheat etc bado ntakua queen tu au ntaishia kua single mother ?

Life is like poker, always make sure you have an Ace up your sleeve.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ogopa mwanaume wa kukudunda lakini
Usiogope mwanaume wa kukucheat.

Wahenga walisema mwanaume asiyecheat ni yule aliyelala kaburini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NDOA ni kitu kikubwa na cha thamani sana duniani aije mtu akasingizia usaliti sijui nn ayo yapo ila ndoa ni muhimu sana kwa binadamu yoyote ||•sijaoa na sina mchumba kiukweli wazazi wangu hasa mama anaumia sana ukizingatia mi ni mtoto pekee wa kiume kipa siku naitwa kwenye vikao wananisumbua kama umeshindwa tukutafutie mchumba na mahari tunakutolea mimi jibu langu BADO NATAFUTA •|• NDOA NI MUHIMU SANA NA IHESHIMIWE

Sent using Jamii Forums mobile app
Ipo siku watakulengeshea mdada
 
Kuoa na kuolewa ni suala binafsi kwa muhusika haipaswi kuingiliana ktk fikra juu ya hili jambo. Ifike wakati sasa mambo ya kale yarekebishwee maana n kunyimana uhuru wa maamuzi binafsi. Kwangu muda ukifika itakuwa hivyo kwa uwezo wake jah na sio watu wengine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ogopa mwanaume wa kukudunda lakini
Usiogope mwanaume wa kukucheat.

Wahenga walisema mwanaume asiyecheat ni yule aliyelala kaburini.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwahiyo na maandiko yaliyosema usizini au usiwe mwasherati au epuka zinaa ni uongo au hayana maana

Uovu ni uovu tu hata kama watu wote wanafanya haimaanishi inakuwa halali, wapo wanaume wanaojitambua sio lazima awe kalala kaburini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom